Matatizo ya wabunge wa kuteuliwa!

Kuchaguliwa kwa Makamba kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais sio zaidi ya kuwakilisha chama na kuwa msimamizi wa wabunge wa CCM ndani ya bunge!

Kama katibu mkuu wa chama endapo itatokea sitofahamu kati ya serikali na wabunge! Then Makamba kama mbunge na Katibu Mkuu wa chama anatakiwa ku-play part! Hakuna zaidi ya hilo!

Thats why tunamuona Makamba sio mchangiaji katika ukumbi wa bunge!
 
Makamba akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, alionyesha uwezo mkubwa ktk kutoa mawazo na kusimamia shughuli za maendeleo. Labda hakuna haja ya nafasi hizi, kumbuka ni nafasi 10. Ukipiga mahesabu ya posho, mshahara na marupurupu mengine kama Mbunge ni pesa nyingi.

We ndugu Nziku naomba uniambie ni maendeleo gani ambayo Makamba aliyasimamia Dar es salaam na mawazo gani makubwa aliyotoa yaliyosaidia kuleta maendeleo. Dar es salaam ni moja kati ya miji mikuu iliyokumwa na kipindupindu cha mara kwa mara alipokuwa RC, na ujambazi, vibaka, na mambo mengi ambayo huwezi kusema unampa mtu credit.

Kama hujui RCs wa miji ambayo ni capital wanavyofanya basi unaweza kumsifu Makamba, lakini kama unajua basi unaweza hata kujiuliza mwenyewe.
 
Uliona wapi kofia mbili zikavaliwa katika kichwa kimoja? Ninavyoelewa mimi,kazi kubwa ya bunge ni kutunga sheria za nchi, hivyo kazi ya mbunge ni kutunga sheria za nchi.

Na mbunge huchaguliwa ili awakilishe wananchi bungeni...sasa unapomteua Makamba awe mbunge sidhani kama unategemea akawakilishe chama kama wanavyodai vipofu wengine. Na unapomchagua awe katibu mkuu ndio usahau lile jukumu ulilompa la kuwakilisha wananchi. Kinachofanyika ni kujilimbikizia madaraka tu kwa tabaka la viongozi ilhali wakina kabwela wanalia njaa.

Sioni sababu ya Makamba kulipwa mshahara wa ubunge na kupata chauchau za ukatibu mkuu wa chama. Wengi hudai Tanzania kuna amani lakini ukweli ni tofauti kwani asilimia kubwa ya watanzania hawana amani mioyoni mwao kutokana na unyonyaji wanaofanyiwa na viongozi wetu.
 
Kimsingi nafasi kumi alizonazo Rais zilikuwa kwa ajili ya makundi maalum katika jamii ambayo hayawezi kuingia moja kwa moja katika siasa na kugombea ubunge kupitia vyama vya siasa. Kwa mfano makundi ya walemavu, viongozi wa dini na mengine ambayo kwa kupewa mwakilishi kupitia uteuzi wa Rais yangeweza kuwakilishwa moja kwa moja ndani ya bunge. Kwa mfano kwa sasa tunatatizo la mauaji ya albino, tatizo la ukimwi. Pengine nafsi hizo kumi zingepewa kwa makundi hayo wangeweza kuchangia na kuwakilisha matatizo yao moja kwa moja kwenye chombo cha kutunga sheria kuliko kumpa mtu kama Makamba ambaye sina hakika kama amewahi kuchangia chochote.

achangie wapi??? yanamuhusu hayo?
 
Kikwete soma hapa na ninaomba uzingatie. Wabunge badilisheni kipengere cha kanuni cha nafasi kumi za Rais kifafanuliwe na kiwe wazi.
 
achangie wapi??? yanamuhusu hayo?

Ninaamini tunazungumzia Bunge, hivyo tunatarajia atoe mchango wake wamawazo ndani ya bunge lakini kwa bahati mbaya hafanyi hivyo. Kama hayamuhusu anatafuta nini ndani ya bunge????
 
Tanzania inahitaji kuondokana kabisa na mifumo isiyo na tija, au isiyoendana na hali halisi ya nchi katika wakati tulionao. Tunapaswa kuwa na upambanuzi na mipaka iliyo wazi kati ya mihimili mikuu mitatu ya dola. Sio mambo ya watu walewale ndio watendaji(serikali) na watu wale wale ndio wahakiki wa kazi za serikali(Bunge).Natamani ingewezekana(maoni yangu)Mawaziri wakawa mawaziri basi, na wabunge wakawa wabunge fullstop, bila watu fulani hapa kuvaa kofia mbili,tatu, n.k ambazo zinapaswa kukaguana na kuhakikiana.

Linaloambatana na hilo, sioni haja ya watu kuteuliwa kuwa wabunge, maana hapo dhana ya mbunge kuwa mwakilishi wa wananchi inakuwa imedhohofishwa kwa namna fulani.
Ni wazi kwamba Mhe.Makamba ukatibu wake wa chama unamfunga gavana fulani katika nafasi yake ya ubunge wa kuteuliwa, laiti angelikuwa huru bila hofu juu ya atakachokisema bungeni kitatafsiriwaje kulingana na nafasi yake katika chama. Akisimama kuihoji serikali Bungeni atakuwa anaihoji serikali ya CCM, na hivyo anaihoji CCM yenyewe, tofauti kidogo na wabunge wengine wa CCM wa kuchaguliwa maana angalau wao wanawasemea wananchi wa majimbo wanayoyawakilisha.
Mzee mmoja katika busara zake akaniambia; Huwezi kupiga penalti,halafu wewe mwenyewe ukawa golikipa wa kuidaka
 
Maneno haya JK kwanza hataki kuyasikia maana yeye akili yake yote ni urafiki na CCM then madaraka hawezi kukubali hata siku moja na inatakiwa Watanzanai kutunga sheria za namna ikiwa ni pamoja kuondoa watu 10 wa rais kwamba ni mali yake kuwapeleka bungeni .
 
Makamba akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, alionyesha uwezo mkubwa ktk kutoa mawazo na kusimamia shughuli za maendeleo. Labda hakuna haja ya nafasi hizi, kumbuka ni nafasi 10. Ukipiga mahesabu ya posho, mshahara na marupurupu mengine kama Mbunge ni pesa nyingi.

Nafikiri kuna jinamizi la uwajibikaji unapokuwa na Cheo Mkoa wa Dar es Salaam hasa kwa nafasi ya Ukuu wa Mkoa, U-mwaibula na Tume ya Jiji.

Hebu tumwangalie Charles Keenja wa Tume ya Jiji kisha kumtazame Keenja wa Mjengoni. Mtu yuleyule lakini utendaji tofauti kabisa. Makamba pia ni muathirika wa jinamizi hili. Yahitaji tafiti ya kina hapa!
 
Makamba ni kama Waziri anapokwenda bungeni

Na Zephaniaanjela

KATIBU Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba ameingia kwa kishindo katika Jambo Forums. Baadhi ya wachangiaji wakiwemo wachanga na wazoefu wanahoji ubunge wake wakidai hachangii katika vikao vya bunge.

Wanajaribu kuwasadikisha watu ili waamini eti hafai kuwa Mbunge na kuhoji uhalali wa kuteuliwa kwake kiasi cha wengine kutaka Rais Jakaya Kikwete atengue uteuzi wake kwa vile hauna faida yoyote.

Wanataka kila Mbunge asikike akizungumza bungeni iwe kwa kuuliza maswali ama kuchangia miswada kwa kusimama na kuonekana akighani mashairi yake huku "akirushwa" moja kwa moja ama vinginevyo na vituo vya televisheni.

Wanadhani ubunge ni kuzungumza sana, kuuliza maswali au kupinga hoja za serikali ili kutafuta sifa hata kama unachopinga hakina maana. Mimi nasema Makamba anafanya kazi nzuri kwa asilimia 100.

Akiwa Katibu Mkuu wa chama kinachotawala, Makamba ni sehemu ya watawala na viongozi waandamizi wa umma ambao kazi yao ni kupokea matatizo na kero za Watanzania, kuzifanyia utafiti wa kina kwa kuzifuatilia kwa karibu, kuzitafutia ufumbuzi, kusimamia utekelezaji wa mahitaji ya kero hizo na hatimaye kupeleka majibu kwa wananchi kuhusu nini kimefanyika katika lipi na kwa namna gani.

Mbunge kama Zitto Kabwe na Wilbroad Slaa wa
CHADEMA, John Cheyo wa UDP, Anne Kilango - Malecela au Christopher ole Sendeka wa CCM, Mohammed Mnyaa wa CUF na wengine kama hao hawamo katika orodha ya watendaji na viongozi wa umma na ndiyo maana wanasikika sana wakipiga kelele bungeni.

Kama ilivyo kwa Wabunge ambao pia ni Wakuu wa Mikoa kama Dk. James Msekela (Mwanza), Monica Mbega (Ruvuma), Mohammed Abdulaziz (Tanga), Dk. Christine Ishengoma (Pwani) au Waziri Mkuu, Mawaziri au Naibu Mawaziri, kazi ya Makamba bungeni kamwe si kuuliza maswali au kuipinga serikali.

Wasiojua siasa hawafahamu kuwa kazi ya Makamba anapokwenda bungeni akiwa Mbunge ambaye ni Katibu Mkuu wa chama kilichopo madarakani kwa maana ya kuwa mtendaji wake mkuu ni kusikiliza matatizo yanayotolewa na Wabunge kama akina Zitto, Slaa, Anne Malecela na kadhalika na kuyatafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri, Mawaziri au Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kama ana mchango anaotaka kuishauri serikali kupitia wizara moja ama nyingine anafanya hivyo kama ilivyo kwa Wabunge ambao pia ni watendaji wa dola kama vile Mawaziri, Naibu Mawaziri, Mawaziri au Waziri Mkuu wanaochangia kwa njia ya maandishi.

Hivyo ndivyo Mbunge Yussuf Makamba anavyofanya na ndiyo maana si lazima kila kikao aingie ukumbini maana anaweza kuchangia namna hiyo akiwa ofisini kwake na kupeleka mchango huo kwa Spika, Naibu Spika au Mwenyekiti wa Bunge kwa njia ya barua.

Mbali na hilo, wanaodhani kwamba Makamba amekuwa akilipwa posho hata asipokwenda bungeni nao pia wana upeo mfupi wa masuala ya utawala na uongozi wa kisiasa.

Posho wanazolipwa Wabunge wanapokuwa katika shughuli za bunge hazitolewi kama zawadi, hivyo hakuna hata mmoja anayeweza kulipwa chochote huku akiwa katika shughuli zake mwenyewe au za chama chake kama ilivyokuwa mwezi uliopita wakati baadhi ya Wabunge wa CCM na
CHADEMA walipokwenda Kiteto kufanya kampeni za uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge katika jimbo hilo.

Kwa hiyo, hata wanaohoji ilikuwaje Mbunge huyo wa Kuteuliwa akaenda Kiteto na kuacha Mkutano wa 10 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiendelea mjini Dodoma wote hawako makini, vinginevyo inawezekana hawana upeo mpana wa masuala ya kisiasa.

Kama ilikuwa haramu kwa Makamba kwenda huko ili kumfanyia kampeni aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Benedict ole Nangole; inakuwaje iwe halali kwa Zitto, Slaa na Grace Kiwelu na kuliacha bunge na kwenda kusaidiana na Mbowe kusaka ubunge kwa aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kutoka CHADEMA?
 
Makamba is senile anyway, why waste a palriamentary seat on him?

The only reason was to make sure that CCM and more important Kikwete has more loyalists in that august house.

I did and do not expect much from Makamba, his constituency is supposed to be Tanzania but it actually is Kikwete.I am more surprised by Mwanakijiji and his likes who still have faith in this misleadership than the misleadership itself.
 
Wanataka kila Mbunge asikike akizungumza bungeni iwe kwa kuuliza maswali ama kuchangia miswada kwa kusimama na kuonekana akighani mashairi yake huku "akirushwa" moja kwa moja ama vinginevyo na vituo vya televisheni.

Wanadhani ubunge ni kuzungumza sana, kuuliza maswali au kupinga hoja za serikali ili kutafuta sifa hata kama unachopinga hakina maana. Mimi nasema Makamba anafanya kazi nzuri kwa asilimia 100.

Akiwa Katibu Mkuu wa chama kinachotawala, Makamba ni sehemu ya watawala na viongozi waandamizi wa umma ambao kazi yao ni kupokea matatizo na kero za Watanzania, kuzifanyia utafiti wa kina kwa kuzifuatilia kwa karibu, kuzitafutia ufumbuzi, kusimamia utekelezaji wa mahitaji ya kero hizo na hatimaye kupeleka majibu kwa wananchi kuhusu nini kimefanyika katika lipi na kwa namna gani.

Mbunge kama Zitto Kabwe na Wilbroad Slaa wa Chadema, John Cheyo wa UDP, Anne Kilango - Malecela au Christopher ole Sendeka wa CCM, Mohammed Mnyaa wa CUF na wengine kama hao hawamo katika orodha ya watendaji na viongozi wa umma na ndiyo maana wanasikika sana wakipiga kelele bungeni.

1. Kati ya kazi kuu za mbunge ni uwakilishi! na ukiwa mwakilishi basi ni budi useme kwa niaba ya unaowawakilisha,na nzr zaidi pale unaowawakilisha watakusikia!!iwe unauliza swali au kuunga mkono hoja au hata kutoa nyongeza ya jambo lolote linalozungumzwa!! haya yapo kila siku wakati wa vikao vya bunge!!

2. Kuzungumza bungeni si kupiga kelele, acha kupotosha maana halisi ya vile wabunge wanavyopaswa kufanya bungeni!

3. Makamba anapoingia bungeni si katibu wa ccm, ni mbunge anawajibika kama mbunge, huo ukatibu anakuwa nao anapotoka nje ya bunge.
 
Huyo muandishi kalipwa tu.

Moja ya kazi za mbunge ni kuhakikisha wananchi wanapata habari za mipango ya maendeleo.Ndiyo maana mara nyingine wabunge huuliza maswali halafu katika majibu utamsikia Waziri anaongelea mikutano aliyofanya na mbunge huyo huyo, nia ni kuwa na transparency na kuwapa wananchi info.

Tatizo linakuja watu kama Makamba wanajisikia kama hawana a specific constituency kwa hiyo wanajisikia hawana haja ya kuongea.
 
NI MTAZAMO WANGU TU!!!!!.

Mtazame Kingunge: Wa kuteuliwa na Mh Rais!!!

Mtazame Simba: Wa kuteuliwa na Rais! Au siyo? Kama analo jimbo mnijuvye!

Tazama michango ya busara zao hewani! Hapo Mhhhhh. Sisemi wote wa kuteuliwa ni wabovu, lakini tujaribu kutathimini juu ya wabunge wa jinsi hii. Wengi ni watu ambao hata kusimama mbele ya wananchi na kunena na wananchi hawawezi vyema!. Sasa, hao ndiyo tunawakabidhi uheshimiwa, kisha tuna watundika uwaziri nk. Unataka nini hapo?

Mimi ninapendekeza, mawaziri wawe wanatokana na wabunge waliochaguliwa na wananchi. Sehemu kubwa ya ho, tutapata wanaoweza kutumia vinywa vyao vizuri, kwa kuwa wanapo mahali pa kusuribiwa wakileta longolongo!.

Mtu kama Kingunge, Sophia anapovurunda, anakata kona kiaina na kuyamaliza na aliyemteua tu!. Lakini angekuwa ni wa kuchaguliwa na wananchi, angepaswa asawazishe kaupepo haka akifika kwenye jimbo lake! Lakini huyu, anakula good time!!!!!!.

Anachosubiri atoe rushwa apitepite kwenye ngazi ya chama, hapo wakubwa wanamwona!. Ghafla tunamwona kaibukia bungeni!
 
Constitutionally it is wrong because the legislature is supposed to be an elected body and giving power to the head of the executive to appoint non-ex-officio members to the House is contrary to the doctrine of separation of powers. Furthermore it is done in a manner that is non-transparent and usually it is used as a political gift by the President. It is legally wrong and gives the Executive power over a legislative deadlock where he/she can appoint up to 10 members at any time to swing a vote in his faivour (should the partisan politics of Tanzania ever develop to a point warranting such action).

Even the UK House of Lords is undergoing a re-vamp including possibly abolishing a non-elected HoL. The democratic process is suppressed by this kind of patronage based system. Surprisingly we appear to be moving in the opposite direction. Tunawazawadia makada wa Chama Chetu Maridadi..lol
 
Mimi nashauri mawaziri wasiwe wabunge! ila mawaziri wateule wapitishwe na bunge!
 
Back
Top Bottom