Hii nimeikuta kule kwa MICHUZI, nikaona niilete hapa ukumbini!
Habari za mishughuliko,
najua hii ni blog ya jamii,nina swali langu napenda niliweke kwenywe blog hii pendqa.
Tangu niolewe huu ni mwaka wa 13 kwa kweli kwa sasa haya mambo ya unyumba siyapendi hata kidogo,na mambo mengine kuyauliza naona tabu,lakini nimeamua niyaulizie kwako.
jee jambo kama hili linawakumba wanawake wengine wowote au ni mimi ndie nina matatizo. Kwani kwa kweli huyo mume kwa sasa namuona kama ni rafiki wa kawaida tu. na hayo mambo ya unyumba miaka nenda miaka rudi natamani yawe na mwisho wake.
Jee kwa walio oa jambo kama hilo linawatokea kwa wake zenu?. Na kwa upande wa mwanamume, mwisho wake ni umri wa miaka mingapi mpaka hiyo hamu imuondoke?.Umri wangu ni miaka 35,na tumejaaliwa kupata watoto 3.
Najua kuna watu watanikandia lakini kwa kweli nipo serious na hili swali. Na natamani tungekuwa kama mwanzo wa ndoa yetu,kwani mwanzo nilikua napenda,na kwa upande mwengine namuonea huruma kwani yeye anataka lakini mie sitaki hata kusikia jambo hilo.
{tafadhali nakuomba usitoe email yangu.}
nasubiri mchango wenu.
Mdau<LI id=916072341549569755>Tarehe May 11, 2009 11:44 AM, Mtoa Maoni:Anonymous
Aiseee hii yako nafikiri ni saikolojiko tatizo lakini linatibika kama upo tayari kuirudia hali yako ya mwanzo......i knw the way you feel about it.Mbije,A-kafanabo
<LI id=8062171788590111254>Tarehe May 11, 2009 11:45 AM, Mtoa Maoni:Anonymous
...Kupoteza hamu ya tendo la ndoa na mumeo kwa umri wa 35 yrs in maana unatembea nje ya ndo na kijana mdogo zaidi ya mmeo, nakushauri uache mara moja hiyo tabia then penzi lako na mumeo litarudi kama kawaida.
<LI id=7113467863878173430>Tarehe May 11, 2009 11:59 AM, Mtoa Maoni:Anonymous
Je endapo kama wewe hujisikii, hutaki kabisa kusikia hiyo ishu kutoka kwa mumeo, upo tayari aende kuchapa nje?
Upo tayari achape nje, kwa siri bila kuathiri mahusiano yenu ya ndoa? Bila kuwepo dalili zozote za kukudhalilisha?
Upo tayari kutoanza kufuatilia nyendo zake za nje? mfano simu, etc?
Kama majibu ya maswali haya yote ni ndiyo, basi tatizo utakuwa umelitatua.
Kama una jibu mojawapo ambalo ni hapana, basi itabidi ujitahidi kumridhisha mumeo.
<LI id=5259257100471048627>Tarehe May 11, 2009 12:37 PM, Mtoa Maoni:Anonymous
Pole sana, lkn kwa informal research findings, most marriages ends-up or start problems at the age of ten to thirteen yrs. Chanzo kimojawapo ni ukomo kwa tendo takatifu na mambo yahusianayo na mahaba. Wewe sio wa kwanza jipe moyo zungumza na mwenzio mjue sababu kuliko kuishi kama 'juma na roza'
<LI id=3749657591061151649>Tarehe May 11, 2009 1:12 PM, Mtoa Maoni:bonge
pole dada[mama],ukweli hayo usemayo yapo na yanaumiza sana kwa m.mme ambaye anampenda mke wake;(only feeling with his wife), lakini inakuwa ni mateso sana kwa mume,mimi nimeoa na mtoto mmoja ndani ya ndoa miaka 2,mke wangu hana feeling na mimi kabisa naumia sana,na sio kama yeye ni muhuni kama mchangiaji mmoja alivyosema,ila kabla ya ndoa tulikuwa tunapendana sana na alikkuwa na feeling kweli .pia mimi kama m.mume sijui cha kufanya, ila ningeshauri tulichukulie positive hili tatizo na tuweze kupata msaada sisi waume tunaoteseka na tunawapenda wake zetu,michuzi pia na wewe ufanye utafiti kwenye hili