Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Ndugu wanaJF, "Great Thinkers" nimeona ni bora kuweka hii thread ili tuweze kutoa kile kilichomioyoni mwetu. Najua hapa jamvini tuna kila aina ya kile nachoweza kukiita mwelekeo wa taifa letu.

Ngoja nisiwe kisiasa, ila natamani sana kuona Tanzania ikiwa katika hali zifuatazo, unaweza kuongeza kadri unavyoweza ili baadaye tutazikusanya na kuziweka maktaba yetu kwa ajili ya kumbu kumbu. kumbuka tu kuwa hii ni mwanzo, baadaye tutapita kwa kila pendekezo namna ya kufikia hapo. karibuni wanaJF.

1. Natamani kuona Tanzani yenye shule zilizo jaa vitabu kila shule, walimu wa kutosha, miundo mbinu safi ya shule.

2. Natamani kuona kila mkoa ukiwa na Chuo kikuu angalau kimoja.

3. Natamani kuona Tanzania yenye mazingira endelevu, yaani kijani kila sehemu mwanza - mbeya, kigoma hasi dar.

4. Natamani kuona ATCL, Mwanza airline, dar airline, Arusha airline nk zikilindima hadi alska, Hongkon nk.

5. Natamani kuona nchi inasehemu kama business centre ambazo wakulima, wenye viwanda wanaweza kuuza bidhaa zao bila shida.

6. Natamani kuona Tanzania tuna viwanda vikubwa vya kuzalisha bidhaa (Heavy manufacturing industries siyo hizi processing ind.)

Ni mwanzo, tuendelee kuzitaja.
 
Back
Top Bottom