matatizo ya meno

Joyceline

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
1,010
166
Nina matatizo ya meno yananiuma sana, hayajatoboka ni mazima kabisa yanauma tu na wakati mwingine nasikia yanatingishika nimeshamuona daktari akaniangalia angalia hapo, akanishauri dawa za kupigia mswaki lakini kila mara tatizo linajirudia mwenye kujua naomba anisaidie, pia nimeshatumia dawa ya maji za kupigia mswaki za gnld
 
Pole sana..tafuta mafuta ya mlonge (pure), kuna jamaa yetu alipata matatito kama hayo na fizi kutoa damu, akakutana na Doctor mmoja kutaka nairobi anatengeneza dawa za asili akampa hayo mafuta, yamemsaidia, unatakiwa kutumia dawa ya colgate na kunyunyizia mafuta kidogo na kuswaki kutwa mara tatu. Huyu Dr. huwa anakuja Dar anapatika nyumba ya sanaa Makumbusho. Jaribu kupita pale kumwulizia
 
Pole,
Daktari wa hospitali gani? Tatizo lako inaelekea kuwa la fizi...waweza google..periodontal disease/periodontal conditions...na linasababishwa na bakteria waliopo kinywani. Tiba ni kumuona dentist atakae kufanyia uchunguzi na kukupa tiba ambapo mara nyingi ni kuondoa "calculus" ambayo huwa inakuwa imejengeka kati ya fizi na jino na vile vile kuangalia hali nzilma ya usafi wa kinywa chako kwani watu wana "susceptibility" zinazotofautiana...na vile vile kuna magonjwa na hali nyingine ziongezazo kiwango cha ugonjwa..kama vile uja uzito na kisukari....
 
asante nitapita kulizia
 
asante kuna dokta wa meno yuko pale moroco karibu na hospital ya dr, masawe ndo alinifanyi uchunguzi akanisafisha akasema hamna kitu nitumie sensodaine dawa ya meno, kususu usafi wa kinywa nazingatia hilo sana pia fizi zinaniuma, ila sina ujauzito wala kisukari.
 
sensodyne works well for sensitivity,which occur when there is gum recession...and that is not what u r explaining,not to discredit the service you got...the problem with Tz is that for whatever cadre everyone is a doctor, and for the different cadres...how one approaches a condition might differ...if you still have painful gums i would stick to the above advice..you need to be seen by a dentist,for proper examination...diagosis and treatment planning...it is usually not a one sitting thing...try agakhan...
 
Pole sana. vile vile unaweza kusukutua na mwalovera unaukatakata vipande vidogodogo unaweka kwenye mji ya moto inakaa kama dakika tano halafu utumia kusukutua. hii inasaidia
 
Nina matatizo ya meno yananiuma sana, hayajatoboka ni mazima kabisa yanauma tu na wakati mwingine nasikia yanatingishika nimeshamuona daktari akaniangalia angalia hapo, akanishauri dawa za kupigia mswaki lakini kila mara tatizo linajirudia mwenye kujua naomba anisaidie, pia nimeshatumia dawa ya maji za kupigia mswaki za gnld

Pole sana, inaonekana tatizo lako ni la Fizi zaidi na tatizo hilo na mambo mengi lakini zaidi ni kutokana na Uchafu uliyokaa muda mrefu kwene kwnye meno hasa uchafu wenye vimengenya vya sukari, ambavyo hupenya mpaka kwenye fizi na kuanza kushambuali bones za kushikilia meno hivyo bones hizo kulegea na mara nyingi meno huanza kulegea.

Mara nyingi kama dalili zimeshafikia hatua ya meno kulegea ni vema ukapata matibabu ya kitaalamu kwani kuna dawa za kalsium na dawa ambazo zitaimarisha kwanza mifupa ya meno na ndipo waanze kusafisha na kuondoa uchafu uliyoganda.

Kunakliniki yameno ni nzuri sana kwa matatizo hayo ya meno , kama wewe ni mkazi wa dar wapo mtaa wa jamuhuri karibu na masumini au wapigie no hii 0753 077 076.
 
asante, haya matatizo ya meno yalinianza tangu 97 nikiwa mdogo, mama yangu alishanipeleka kwa madaktari mbali mbali nikatibiwa halafu sili vitu vya sukari tangu muda mrefu halafu meno yangu hayajaoza,ninapopata matibabu lianaisha lakini baada ya muda linajirudia. lakini nitazingatia yote mnayoniambia na nitayafanyia kazi.
 
asante kuna dokta wa meno yuko pale moroco karibu na hospital ya dr, masawe ndo alinifanyi uchunguzi akanisafisha akasema hamna kitu nitumie sensodaine dawa ya meno, kususu usafi wa kinywa nazingatia hilo sana pia fizi zinaniuma, ila sina ujauzito wala kisukari.
Pole sana,
Nashauri uzingatie yaliyosemwa na herikujua.

I am just curious...
Daktari alikufundisha namna ya kuswaki?
Alikueleza ni kila baada ya muda gani unahitaji kununua mswaki mpya?
Kitu gani kingine kipya umejifunza toka kwa huyo daktari?
 
Asali na mdalasini.

  • mdalasini kijiko 1 cha chai.

  • asali vijiko 5 vya chai.
Matumizi:
changanya na paka kwenye jino liumalo fanya hivi mara 3 kila siku hadi jino liache kuuma. ii. Asali na mdalasini.

  • asali kijiko 1 cha chai.
  • mdalasini kijiko 1 cha chai.
Matumizi:
changaya kwenye maji ya moto kisha sukutua kila asubuhi hii piahusaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomo.
Au Tumia Dawa hii hapa chiniKwa yule mwenye matatizo ya jino(kuuma), pokea maelezo yafuatayo kwa uwezo wa mwenyezi mungu litapoa.

MATAYARISHO
Chukua majani ya mtunda(muarubaini),majani ya mpera na magome ya muembe.Tia kwenye sufuria kisha chemsha kwa maji yaliyo safi kwa muda wa dakika 15 hadi 20.
Kisha chukua dafu kubwa lenye nyama, likate sehemu ya juu kwa lengo la kutengeneza mlango mdogo.Yatoe maji yote ya dafu kwa vile hayahitajiki na bakisha nyama tu.

MATUMIZI
Chukua maji yako ya dawa yaliyo moto na mimina kwenye dafu kiasi kwamba yakaribie kujaa.Kisha weka mdomo wako juu ya mdomo wa dafu kwa lengo la kuingiza mvuke wa dawa kwenye mdomo.Weka kisha ondosha kulingana na umoto wa maji ya dawa kwa muda wa dakika 3 hadi 5.
Kisha sukutua kwa maji ya dawa ambayo yameshapungua joto.
Endelea na zoezi hili asubuhi,mchana na jioni kwa muda wa siku tatu na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu utapoa.
 
kama unauwezo nenda kaoshe hayo meno
hasa kama upo dar nenda regency hosp.
wanasaidia sana.
 
pole sana. Vile vile unaweza kusukutua na mwalovera unaukatakata vipande vidogodogo unaweka kwenye mji ya moto inakaa kama dakika tano halafu utumia kusukutua. Hii inasaidia

sasa hiii makhirikhiri aka kakobe maarufu kwa wacheza pool table. Yaaani ya kubahatisha zaidi
 
pia waweza tumia DFP (DENTAL FORMULA POWER, MIMI IMENISAIDIA SANA, YAAN TANGU 2005 HADI LEO SIJAUGUA MENO TENA. INAPATIKANA PALE UBUNGO PLAZA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom