Matatizo ya kibofu yanaweza kutibika kwa chakula

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Matatizo ya kiafya katika kibofu cha mkojo yamekuwa

mengi hivi sasa, hasa kwa wanaume wenye umri kuanzia

miaka 50. Kazi kubwa ya kibofu ni kusaidia ukuaji wa

mbegu za kiume, kama kibofu kikiwa na matatizo, uzalishaji

wa mbegu za kiume nao hupungua sana na tatizo

lisipotibiwa haraka, husababisha ugumba. Aina nyingine ya

matatizo ya kibofu husababisha uvimbe sehemu za

siri.Inaelezwa kuwa matatizo ya kibofu mara nyingi huwa ni

ya kurithi, ingawa kuna sababu nyingine pia.


Ugonjwa unaweza kusambaa ukoo mzima, kutoka kizazi

kimoja hadi kingine. Sababu nyingine zinazosababisha

ugonjwa huu zinaelezwa kuwa ni kukaa kwa muda mrefu,

kuvaa nguo zinazobana, ukosefu wa choo na maambukizi.

Kupenda kujamiina sana nako kunaelezwa kuwa ni sababu

moja wapo. Pamoja na ukubwa wa tatizo hili ambalo

husababisha kansa pia, kuna habari njema kuwa matatizo

madogo ya kibofu yanaweza kutibiwa nyumbani kwa kula

vyakula na kufuata kanuna kadhaa na mtu akapona kabisa

au akazuia isimpate, lakini iwapo tatizo limeshakomaa na

kuwa sugu, unashauriwa kwenda hospitali na kuonana na

daktari haraka iwezekanavyo.



UTAJUAJE UNA TATIZO?


Dalili moja wapo ya mtu mwenye tatizo la kibofu ni kusikia

maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo. Dalili nyingine ni

kushindwa kukojoa kabisa licha ya kuhisi kubanwa na

mkojo. Dalili nyingine ni kusikia maumivu chini ya mgongo

na kwenye ‘hips’. Kwa kuwa mtu huwezi kujipima kama una

tatizo hilo, ina shauriwa kwenda hispitali kupima. Saratani

ya kibofu ni miongoni mwa matatizo yanayoweza kujitokeza

na inaweza kuuawa!



DONDOO ZA TIBA MBADALA..


Tiba mbadala ya matatizo ya kibofu hufanyakazi vizuri na

imeonesha mafanikio makubwa kwa watu waliowahi

kujaribu. Mbegu za maboga ni miongoni mwa tiba mbadala

za kutibu matatizo ya kibofu. Pondaponda kiasi cha mbegu

15 hadi 20 za maboga na changanya kwenye mlo wako wa

kila siku.Utaona mabadiliko ya haraka ya unafuu ndani ya

wiki mbili hadi tatu. Vitamini E ni kirutubisho muhimu sana

katika kutibu matatizo ya kibofu. Aidha, mboga za majani

rangi ya kijani, mayai na bidhaa zitokanazo na maziwa nazo

zina kiwango kikubwa cha vitamin E, hivyo viliwe kila

siku.Dawa nyingine mbadala ya matatizo ya kibofu ni


enema ya maji ya uvugu.


Enema ya aina hii ifanywe mara mbili au tatu kwa wiki ili

kurejesha utendaji wake wa kawaida. Uvutaji sigara na

unywaji pombe hauruhusiwi kabisa wakati wa kufanya tiba

hizi, hali kadhalika vyakula vilivyoungwa sana. Mwisho,

inashauriwa sana kuacha kunywa vinywaji vyote vyenye

‘caffeine’, hii ni pamoja na chai na kahawa, kwa sababu

huzalisha matizo zaidi. Mazoezi ya nusu saa ya kukimbia au

kuendesha baiskeli yatasaidia zaidi. Kwa kuwa baridi ni

miongoni mwa sababu zinazochangia maradhi ya kibofu,

mgonjwa anayeishi sehemu yenye baridi anashauriwa

kuhamia sehemu yenye joto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom