Matatizo Shirika la Reli TRL na Wahindi

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Matatizo ya shirika la reli wasafiri kila mara wanalala Station hadi lini

Check hii

5505d1249558978-a-kamishna.jpg


Mmoja wa abiria waliokwama katika Stesheni ya Dar es Salaam, Bw. Shadrack Mwami akijibizana na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli, Kamishna Msaidizi Ruth Makelemo wakati abiria hao walipomlalamikia kuhusu Shirika la Reli Tanzania (TRL) kushindwa kuwasafirisha kwa takribani siku tatu sasa. Bw. Makelemo alikuwa akisubiri treni ya kwenda Kigoma
 

Attachments

  • KAMISHNA.jpg
    KAMISHNA.jpg
    13.6 KB · Views: 185
kwa mtazamo wangu hii Reli Serikali yetu iingoe na kuweka balabala adha hii tumeichoka
 
Jamani msisingizie wahindi au mmsahau kuwa reli tulivyoirithi baada ya kuvunjika kwa EAC? Reli ya TZ ndiyo ilikuwa inalipa kweli na tulisaidiwa sana kuiimarisha lakini matokeo yake tuliiua wenyewe. Huwezi kuamini lakini kama mashirika mengine ya SU yalivyokwisha basi na reli ni hivyo hivyo. Enzi za EAC ilikuwa vigumu sana kuiba hata senti 5 maana ilikuwa ni kufukuzwa na kupoteza haki zote.
Baada ya kuwa yetu ubadhirifu uliongezeka wafanyakazi waliajiriwa karibu mara 2 kuliko ilivyokuwa wakati wa TRL matokeo tuliua mtaji ndiyo maana ikatushinda.
Ilivyotangazwa tenda kila aliyekuja na kuona hali ilivyo alichomoa ndiyo maana tukapata hawa ndugu zetu wa india. Huwezi kuamini hata wafanyakazi wenyewe ndiyo wahujumu wakubwa unadhani kuna kitu hapo?????
Hili ni fupa ambalo sijui nani ataliweza maana ni WIZI MTUPU kuanzia kwetu wazalendo hadi wageni hawa. Jee nani wakulaumiwa? kama sisi wenyewe tumekosa uzalendo nani atakua nao?
 
Back
Top Bottom