Matatizo ktk Ndoa

hovyohovyo

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
547
157
Wanajamvi, ktk utafiti wangu hapa Jf, nimegundua kuwa matatizo ktk ndoa yako mengi, na ama yalikuwepo siku zote au yanaongezeka au ni kwamba tu jf inatupa uhuru zaidi wa kuyaeleza. Haipiti siku hapa, hatujaona post, tena ya malalamiko kuhusu mke/mume/mpenzi, ama kuhusu tendo la ndoa, matumizi ya ndani, maamuzi, ndugu kuingilia ktk ndoa. Walau matatizo si haba. Hii crisis ya ndoa inatupeleka wapi? Tufanyeje ili ndoa ziwe mahali penye amani na upendo? Nini nafasi ya mume/mke ktk kuboresha ndoa? Ndugu/Jamaa wana nafasi gani au tuwape nafasi ipi ktk hili? TUJADILI
 
ngoja nikapike kwanza, niokoe ya kwangu
ntarud baadae kidogo .......lol
 
The human condition is a crisis.

Ukioa kuna matatizo ya ndoa.

Usipooa kuna matatizo ya kutokuoa.

Ukioa na kuishi kama hujaoa kuna matatizo yote ya kuoa na kutokuoa.

Usipooa na kuishi kama umeoa nako vile vile.

Namkumbuka Mbaraka Mwinshehe na wimbo wake wa "Shida".

Chakufanya ni kukubali matatizo yapo, kujaribu kuyapunguza kama inavyowezekana na kama unachagua ndoa, kuchagua mtu ambaye uko radhi kupata matatizo kwa ajili yake.
 
Wanajamvi, ktk utafiti wangu hapa Jf, nimegundua kuwa matatizo ktk ndoa yako mengi, na ama yalikuwepo siku zote au yanaongezeka au ni kwamba tu jf inatupa uhuru zaidi wa kuyaeleza. Haipiti siku hapa, hatujaona post, tena ya malalamiko kuhusu mke/mume/mpenzi, ama kuhusu tendo la ndoa, matumizi ya ndani, maamuzi, ndugu kuingilia ktk ndoa. Walau matatizo si haba. Hii crisis ya ndoa inatupeleka wapi? Tufanyeje ili ndoa ziwe mahali penye amani na upendo? Nini nafasi ya mume/mke ktk kuboresha ndoa? Ndugu/Jamaa wana nafasi gani au tuwape nafasi ipi ktk hili? TUJADILI

Hii crisis ya ndoa inatupeleka wapi?
Ndoa si sehemu ya matatizo au kutunishiana misuli, pindi utakapoanza kuona kuna shida basi ni vyema kujikagua binafsi kabla ya kunyosha kidole kwa mwenzi wako. Ni wazi kuwa matatizo yoyote katika ndoa mwisho wake ni kutokuelewana na hatimaye kutengana.

Tufanyeje ili ndoa ziwe mahali penye amani na upendo?
Ni kuepuka kufanya mambo yasiyo ya msingi ambayo hayana maudhui ya dhana nzima ya ndoa. Unajua kikristo huwa tunaamini ndoa ni tendo la kukamilisha utu. Hivyo unapoamua kuambatana na mwenzi wako ni hatua kuwa umejitambua.

Nini nafasi ya mume/mke ktk kuboresha ndoa?
Mume ni kichwa cha familia na Mke ni msaidizi wa kichwa cha familia. Pindi wanandoa wakijikita katika dhana hiyo basi mengineyo yatakuwa shwari.
 
Mara nyingi habari nzuri huwa si 'news'

Hivyo kuna mazuri mengi yapo lkn si interesting au challenging ndio maana hayaandikwi!

Lkn maisha kwa ujumla ni full changamotos.
 
Mara nyingi habari nzuri huwa si 'news'

Hivyo kuna mazuri mengi yapo lkn si interesting au challenging ndio maana hayaandikwi!

Lkn maisha kwa ujumla ni full changemotos.

full what? lol....
 
Nafikiri kwenye ndoa kuna mengi mazuri sn but ishu ni kwamba watu wanazungumzia magumu zaidi ili kupata utatuzi. La muhimu mume ampende mkewe kwa dhati, mke nae vile vile ampende mumewe pamoja na kumheshimu. Matatizo ya wanandoa yajadiliwe na wanandoa ili kupata ufumbuzi, changamoto ni sehemu ya mahusiano yoyote hata mahusiano ya ndugu na ndugu, watoto na wazazi n.k huwa yana magomvi kibao.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kwanza kabisa watu waache kumegana kabla ya ndoa. hapo tutakuwa tumesolve mambo mengi sana
 
Mleta mada kumbuka ndoa ni shule kila siku kujifunza..na pia matatizo ya ndoa ndio ndoa yenyewe!
Usitegemee wanadamu wawili waliokutana ukubwani wataishi maisha yao yote bila kukwaruzana..
Na isitoshe 'cases' zinazokuja hapa JF ni zile 'extremes'..lakini lazima ukubali pia kuna mazuri mengi tu kwenye ndoa..
Bado sijakubali kama hili limekuwa janga la kitaifa..
 
wawili hawa wamekua ktk familia na mazingira tofauti, mitazamo na fikra zisizo pacha. Kutofautiana ni jambo la kawaida tu. Mazur ni mengi sana kwenye ndoa haya hesabiki, na ndoa hutawaliwa na mazur mengi mno ndo mana hata baya kidogogo huonwa kama tatizo.
 
Mbona mie naona familia at large ndo changamoto zaidi? Ndoa ni watu wawili,its very easy to agree and to agree to disagree.
Kwenye familia kuna watu unatamani uwapime dna! Kha!
 
Hayo matatizo ndio yanasaidia kujua kama umedondokea panapokufaa au la, yanachangamsha akili na hisia bila kusahau kuwa yanaimarisha ndoa pale mnapoyashinda matatizo yenu.
 
Wanajamvi, ktk utafiti wangu hapa Jf, nimegundua kuwa matatizo ktk ndoa yako mengi, na ama yalikuwepo siku zote au yanaongezeka au ni kwamba tu jf inatupa uhuru zaidi wa kuyaeleza. Haipiti siku hapa, hatujaona post, tena ya malalamiko kuhusu mke/mume/mpenzi, ama kuhusu tendo la ndoa, matumizi ya ndani, maamuzi, ndugu kuingilia ktk ndoa. Walau matatizo si haba. Hii crisis ya ndoa inatupeleka wapi? Tufanyeje ili ndoa ziwe mahali penye amani na upendo? Nini nafasi ya mume/mke ktk kuboresha ndoa? Ndugu/Jamaa wana nafasi gani au tuwape nafasi ipi ktk hili? TUJADILI

haya yanayoandikwa humu sio kuwa ndoa zote zipo hivo,kuna MAMBO MAZURI SANA KWENYE NDOA !KWANGU MIMI NDOA NI BONGE LA RAHA BANA!
 
Wanajamvi, ktk utafiti wangu hapa Jf, nimegundua kuwa matatizo ktk ndoa yako mengi, na ama yalikuwepo siku zote au yanaongezeka au ni kwamba tu jf inatupa uhuru zaidi wa kuyaeleza. Haipiti siku hapa, hatujaona post, tena ya malalamiko kuhusu mke/mume/mpenzi, ama kuhusu tendo la ndoa, matumizi ya ndani, maamuzi, ndugu kuingilia ktk ndoa. Walau matatizo si haba. Hii crisis ya ndoa inatupeleka wapi? Tufanyeje ili ndoa ziwe mahali penye amani na upendo? Nini nafasi ya mume/mke ktk kuboresha ndoa? Ndugu/Jamaa wana nafasi gani au tuwape nafasi ipi ktk hili? TUJADILI

Ni kweli ndoa nyingi hasa za vijana wa kisasa zina matatizo sana... na hii yote ni kutokana na lifestyle ya ulimwengu wa sasa... vijana si wavumilivu tena, hawana mioyo ya uvumilivu, wana tamaa, na pia ongezeko la wanandoa kushiriki katika mitandao ya kijamii nadhani inaweza kuwa ni sababu moja wapo. Mke/Mme anablog siku nzima anajisahau maisha ya mitandao anarudi nayo nyumbani badala ya kuyaacha hukuhuku blogini. Asilimia kubwa ya wamawake ni rahisi sana kupotea.... kuna blog kama za kina Mange , that kind of lifestyle huwezi ishi kwenye ndoa na mwanamke anayetaka maisha ya vile, hivyo wanawake esp walioolewa wanajisahau wanaenda kudemand kwa waume zao wakikosa wanalazimika hupigwa miti nje ili wapate maisha ya juu kama yale.
Pia mke wa mtu mpaka usiku wa manane uko BBM au fesibuku unafanya nini huko? kuna vijana kazi yao ni kuwatongoza na kuwakaza wake za watu kwa kupitia kwenye hiyo mitandao.
Jamani tusijisahau kiasihicho hata sisi wanaume tuliooa lazima tuwe makini... usiingize mambo/ideas za kwenye mitandao kwenye ndoa au mausiano yako. Haifai kabisa tublog hapa na tuyaache hapahapa.
Aksanteni sana.
 
...Mkuu hata ukiziweka glass tupu jirani zitagongana sembuse binadamu waliolelewa katika malezi tofauti? Hakuna mahusiano ambayo hayana changamoto kila siku iendayo kwa Mungu. Kinachotakiwa kama ulivyosema ni kujaribu kuyapunguza au kuyamaliza matatizo hayo ili mahusiano hayo yawe ya furaha kwa wahusika wote.

Changamoto nyingine ni haya mambo ya utandawazi. Matatizo kidogo tu ndani ya nyumba mke/mume kishayaanika hadharani kule FB, JF na kwingineko labda kutafuta sympathy kwa aliyotendewa au ushauri na wakati mwingine huo ushauri anaoutafuta mtandaoni badala ya kujenga unabomoa.

Wazazi wetu enzi zao matatizo yao ndani ya ndoa walikuwa hawayaaniki hovyo hovyo kwa kila mtu. Walikuwa na taratibu zao za kuyashughulikia matatizo yao ambayo yalisaidia sana ndoa nyingi kudumu kwa muda mrefu sana na matatizo kujulikana na watu wachache sana ukilinganisha na ilivyo sasa.

The human condition is a crisis.

Ukioa kuna matatizo ya ndoa.

Usipooa kuna matatizo ya kutokuoa.

Ukioa na kuishi kama hujaoa kuna matatizo yote ya kuoa na kutokuoa.

Usipooa na kuishi kama umeoa nako vile vile.

Namkumbuka Mbaraka Mwinshehe na wimbo wake wa "Shida".

Chakufanya ni kukubali matatizo yapo, kujaribu kuyapunguza kama inavyowezekana na kama unachagua ndoa, kuchagua mtu ambaye uko radhi kupata matatizo kwa ajili yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom