matatizo katika mtandao wa tigo

zombi

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,618
1,333
katika siku mbili zilizopita, kuna tatizo ambalo limenitokea mimi na wateja wengine wa matandao wa tigo, inatokea unampigia simu mtu anapokea mtu mwingine ambae siyo yule uliyempigia (sio wrong number scenario), inakua kama simu yako imekua diverted, nimeongea na watu wengine wawili ambao wanapata tatizo kama hilo. hii ni hatari kwani inaweza kufunja ndoa za watu sababu imetokea kwangu mke wangu alivyopiga amepokea mwanamke na kumuuliza we ni nani?, kama kuna mtu mwingine aliyeexperience jambo hili na ana taarifa zake na sababu ya kuwa hivyo, atumwagie hapa JF, nimeona ni muhimu kushare jambo hili hapa JF kwani inaweza kuwa imetokea kwa watu wengi zaidi.
 
Ndugu yangu, TIGO mimi sina hamu nao kabisa.Siku hizi wamekuwa na kila aina ya wizi. Pamoja na tatizo kama hilo ulilolielezea pia wana tabia za kuibia watu kupitia kupiga simu. Hii inatokea unapopiga simu huwezi ongea na simu hiyo kwa dakika mbili au tatu bila ya simu kukatika unapokuwa unaongea. Hii maana yake nini??? Kama una ujumbe wa muhimu itakubidi upige tena na simu ikiungwa tu unakatwa tena gharama nyingine ambayo kama isingekatika usingeilipa. Lakini pia wana aina nyingine ya wizi kupitia hii milio ya simu. Mfano jana mimi wamenitumia sms wakisema nimekatwa jumla ya shilingi 300 kkama gharama ya mlio niliochagua, wakati mimi sijawahi kuomba mlio wowote wa simu toka kwao. Hii ni aina nyingine ya wizi. Pia kuna wizi mwingine wa kila unapopiga simu, lazima simu hiyo haitakuwa na line ambayo ni clear saana bila kuwa na mikwaruzo, ambayo itakupelekea wewe kuikata simu na kuipiga tena. Ukifanya hivyo tu wenzio wanafaidika kwa kukuchaji bei mpyaa ya kukuunganisha. So I HATE HAWA TIGO!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom