Mwiyuzi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 845
- 429
Habari zenu wanajamvi,
Katika familia yetu mimi ndo nilifanikiwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu, wengine waliishia std 7 na wengine form four, japo kwa sasa wengine ni wajasiriamali na wengine ni ma day worker viwandani.
Nilimaliza chuo na kukaa muda mrefu bila ajira, lakini nikabahatika kupata kazi ya tempo ambayo ni ya miez mitano. Baada ya kupata kazi nilimpatia mama hela kama zawadi akashukuru, baada ya mwezi akaniomba nimkopeshe laki moja ili alipe deni kwani anadaiwa, nikaamua nimpatie hiyo laki moja bila kumkopesha, Baada ya miezi kama miwili akaniambia nitoe mchango kwa aliyekuwa rafiki yangu wa primary aliyekuwa akitarajia kufunga ndoa, nilikataa kutoa huo mchango kwani mtoto wa shangazi yangu alikuwa akihitaji ada kwa ajili ya kwenda shule, kwa hiyo nikampatia kiasi yule wakusoma, mama akaniambia kuwa kama nimeshindwa kutoa mchango wa harusi ya yule rafiki basi nimchangie hela ya zawadi atakayoitoa kwani huyo rafiki huwa anamsalimia vizuri...kusema ukweli sikumpatia hiyo hela.
Juzi kanipib nikapiga akaniambia nimpunguzie vocha, nikampunguzia vocha ya elfu tano lakini nikashangaa kuona kimya wakati vocha imeenda, kumpigia simu akasema kuwa hakurespond kwani alijua niko kanisani lakini kabla sijakata simu akasema kuwa sakafu ya nyumba yetu imebomoka na rangi ya nyumba imepauka so inabidi nigharimie.
Sasa mimi nikajiuliza kwamba hivi huyu mama kwa nini hataki kuelewa kuwa kazi niliyonayo ni tempo tu? Mshahara wangu ni mdogo lakini anademand kiasi hiki...hivi anataka mimi nifanyeje? Na kwa nini asiwaambie pia kaka zangu na dada ili nao wachangie kwa kuwa mimi bado sijasettle kimaisha? Je anafanya hivi kwa sababu mimi peke yangu ndo niliyesoma kwenye familia?
Kwa kweli simuelewi mama yangu! Manake nimeona kuwa ukiwa umesoma kwenye familia ndo unakuwa kwenye wakati mgumu wa kulaumiwa kupita wote...kwani ukimpatia mtu leo hela anakushukuru kwa mikono miwili lakini siku ukimwambia sina utasikia lawama kibao! Hivi na wazazi wengine wako hivi?