Matarajio na Matamanio ya Mabadiliko; Kazi hazifanyiki maofisini

Ninakubaliana na wewe. Muda mwingi kwenye ofisi za serikali unatumika kujadili mustakabali wa nchi yetu. Wengi wana hamu 2015 ifike mapema ili uongozi uliopo uondoke. Kwa ujumla, watanzania wengi wamekata tamaa.
 
Alberto, inauma sana, pole. Lakini katika wajumbe wote wa kamati, ni wangapi unadhani waliumia roho Kama wewe? Nadhani wengi, hasa wa ccm walikuja tu kwa ajili ya posho, inawezekana hata ulipokuwa unauliza maswali waliona wewe mtu wa ajabu, mkorofi, utawasumbua kwenye kamati yao.

Haya ni matatizo makubwa central and local gov. Hata Kakalende hapo juu ameliongelea. Ni saratani mbaya kuliko ufisadi tunaopambana. Ni changamoto ya chama chochote kitakachoitoa ccm madarakani

hoja yangu ya leo ni hali hatari zaidi ambayo hata wale wachache na taasisi binafi hawafanyi kazi. Siyo kwa sababu ni wazembe au wavivu bali kwa sababu kuna mabadiliko fulani wanayatarajia ambayo hayajulikani ni gani na yatatokea lini.
 
Hiyo ipo sana. 'huyu mtoto anatusumbua' 'hawa wapinzani wanapinga'

Lakini binafsi sirudi nyuma. Mabadiliko yatapatikana kama wengi wetu tutaingia kwenye halmashauri na manispaa. Itasaidia sana sana! Mipango mingi sana inakwamishwa huko! Fedha nyingi sana zinaliwa huko! Wajumbe hawasomi kwa umakini makarabrasha! Wengine hawawezi kuyaelewa kutokana na elimu etc!

Vijana tuamke, twende kwenye uongozi wa serikali za mitaa! Vijiji na Kata! Thats my plea!
 
Wazo zuri mtoa mada. Tuhamasishane sasa kuanza kufanya kazi na kutafuta mabadiliko yetu as individuals so that we could be more powerful when combining forces.
 
mimi mwenyewe niko private lakini jamu ya kupiga kazi haipo natamani kitu kitokee labda maisha yatabadilika. Kuhusu utendaji wa halmashauri zetu huu ni ugonjwa sijui wa aina gani mimi sijui tutautibu na dawa gano. Waheshimiwa wabunge na madiwani wa upinzani wanayo kazi moja tu ya kuonyesha tofauti lasivyo wanancho watakasirika na kuwatoa waote.
Mbunge wetu mdee bado sijaanza kuona kama analeta mabadiliko ya mazoea ya ccm.ninahitaji kimwona akipiya mitaani akiwatia noyo watu washiriki kujiletea maendeleo.
Wananchi tuko tayari kushirikiana naye hata kufanya usafi wa mazingira yetu. Tegeta kwa mfanao ni shehemu yenye watu wegi lakini ni pachafu kwa sasbu hakuna utaratibu wowote wakuzoa uchafu. Watu wana viwanja vidogo hivyohawana eneo la kutupa takatak.
Lazima watu watiwe moyo na viongozi ili washiriki kwenye kutekeleza wajibu wao.
watanzania wapo tayari kufanya kazi na mtu wanayempenda. Mdee anapendwa na watu wa jimbo lake basi anauwezo wakushirikia na wananchi wake kwa urahisi. tunaomba aje tegeta atupatie mikakati ya namana ya kuusafisha mji wa yegeta maana ni mchafu sana.
 
Nadhani nitakuwa sawa kama nikisema kwamba Tanzania haijawahi kuwa na post election fever and enxiety ndefu kama hii ya wakati huu.

Kadri hali ya siasa za Tz inavyozidi kuchacha, hali ya kiuchumi inavyozidi kuwa ngumu, serikali inavyoshindwa kuongoza, upinzani unavyozidi kuimarika, basi wananchi wengi wanazidi kuwa na shauku ya ni lini mabadiliko yatatokea.

Wafanya kazi wa serikalini, mashirika ya umma na asasi zisizo za kiserikali, wote wanafuatilia siasa za nchi hii wakati huu kuliko vipindi vingine vyote awali katika nchi hii. Vyanzo vya habari vinatumika barabara, iwe magazeti, runinga, blogu, simu, au mijadala ya ana kwa ana. Tofauti na zama nyingine zote Tanzania, wakati huu, hakuna mwananchi asiyejua nchi iko kwenye tatizo gani. Most public servants are blogging against their government!!

kwa sababu hiyo, utaona kwamba watz wengi sasa wana hamu ya kuona nini hatima ya haya mambo, ingawa haiko wazi hatima inayotarajiwa ni ipi ilimradi kila mtu anatarajia jambo fulani kubwa litokee. Kuna wanaoamini tunahitaji kufanya kama Tunisia, sasa hivi. Kuna wanatamani utokee muujiza viongozi wa juu wa serikali wabadilike ghafula. Kuna wanaotamani 2015 ifike kesho. Kuna wanatamani uchaguzi mkuu urudiwe leo! Kuna wanaoamini kwamba Bunge litakomesha hii hali, litaleta mabadiliko.

La msingi ni kwamba, fikra za watz wengi ziko kwenye matarajio ya mabadiliko na wanatumia muda mwingi kufuatilia na kutamani kinachoendelea kuliko wanavyofikiri na kufanya kazi zao. Haina maana kwamba kazi hazifanyiki kabisa, lakini nadhani siyo kwa tija kama ambavyo hii hali isingekuwepo. Ni kama kusema watu wanalazimika tu kuamka asubuhi na kwenda kazini, hawajisikii. Muda mwingi kutwa wanafuatilia habari kwa njia mbalimbali.

Umenena jama zangu kiraninaye mpa jm wanatamanikukesha kuchambuwa loja
 
Hebu ngoja niende kule kijijini isokami nione kama na wao wanamuamko wenu?
Je sisi ni representative ya majority ya wa TZ kweli au nikasehemu? Wote humu mnakazi au ajira zinazowafanya muweze kuafford internet communication. Ni asilimia ngapi ya waTanzania wako kama sisi?

Semeni tu kwamba mabadiliko sio lazima yaletwe na watanzania wooooote, werevu wachache wanaweza. Lakini sio mseme a majority of Tanzanians want change.

Mkuu Nyamgluu, nashukuru kwa mawazo yako, nilichelewa kukujibu kwa sababu nilikuwa natafuta hii post ambayo nilibandika jana. Nadhani namba mawazo zaidi.

icon1.png
Ugali wa moto, mboga ya moto, pilipili kali, Machozi blublublublu

Yaani bado nacheka,

Niko kwenye foleni barabarani, amenifuata muuza icecreem (na baiskeli yake ya Azam, ananifahamu). Akaniuliza, "bro, mjengoni si tarehe 8 mwezi wa pili eh?"

nikamwabia ndiyo, akasema "hapo ccm walipo nakuambia bro, ugali wa moto mboga ya moto na pilipili kali. Yaani wanakula ndiyo lakini machozi machozi yanawamiminika blublublublu na makamasi juu. Wanatamani February isifife. Mi nasubiria tu bro, labda wazuie wabunge wa Chadema wasiingie bungeni."

nimefurahi jinsi huyu kijana alivyoweza kuwasilisha kwa upana kiasi hicho hali halisi ya siasa na uchumi wa nchi yetu kwa kutumia maneno machache hivyo. Huyu kijana hana uwezo wa kutumia internet wala kununua gazeti.

Lakini ana ufahamu kamili wa nini kinaendelea na matarajio yake kwa bunge na wabunge wa upinzani ni thabiti

je, wabunge wa Chadema watamfurahisha au kumkatisha matumaini huyu kijana? Matarajio makubwa namna hii na thabiti ni makubwa mno kwa wabunge wa Chadema kutekeleza?​
 
sitashangaa ukitoka waraka kutoka utumishi ukiwataka wakuu wote wa idara za serikali na mashirika ya Umma kuweka block kwenye server zao kuzuia access ya blogs na mitandao kama JAMIIFORUMS kwa wafanyakazi. NYIE SUBIRINI TU!

Thubutu!!!! Patachimbika!!!! Some of us are already addicted to JF. We can't even imaging life without it.
 
Thubutu!!!! Patachimbika!!!! Some of us are already addicted to JF. We can't even imaging life without it.

addiction is the word!!!

watendaji wengi wa serikali, ngazi mbalimbali wako hapa JF kama visitors au kama members wanashiriki mijadala na kuchukua mawazo hapa na kujadili one on one. Kuna mtu ameni PM kwamba hata wabunge wa ccm wako hapa wanaikandia ccm kwa kwenda mbele!!

siku moja nianzisha thread hapa nikiuliza je serikali itafunga JF, nikidhani kwamba wanajua kinachoendelea kati ya maafisa wao na JF pamoja na ccm na kwamba wanaweza kufunga JF. Hiyo thread ilipeperushwa ndani ya dakika chache sikuwahi kuiona hadi leo. Niliuliza mods wala sijapata jibu. Sidhani mimi naelewa ni kiasi gani JF iko safe from government attack.

JF ni kijiwe cha lazima kwa kila mpenda mabadiliko, na wato kweli tuko addicted kwa maana kwamba ikipita muda bila kutembelea hapa unasikia unakonda
 
Unachokieleza Mkuu ni kweli, kwani sehemu za kazi na vyuo kumekuwepo na mwamko mkubwa sana wakujua nini kinachendelea zidi ya Serikali yetu. Bado kitambo kifupi mambo yatakaa sawa kama Tunisia na sehemu nyingine. Kwa hali ilivyosasa hivi ukisema vijana waamuke watasema tupo tayari ! wafanyakazi watasema wapotayari ! wazee wetu wakiume watasema tupotayari! lakini tatizo litakuwa kwa akina mama wakitanzania watasema hawapotayari !. Kwa hiyo sasa hivi tuelekeze nguvu ya kuwaelimisha wanawake ambao ndiyo kwa kiasi kikubwa wanarudi nyuma. Tuwaambie waangalie mfano wa Tunisia wanawake wapo barabarani kudai haki zao.
 
Nashukuru kwa mawazo mkuu, kuhusu akina mama nadhani wanashiriki kwa njia nyingi sana. kwanza ujue wengi wana watoto, na wakati wanaume wanahatarisha maisha yao, wanawake wanakusanya watoto na kufikiria mwanaume akienda kuuawa huko atatunzaje watoto. na wakati wanaume wanakwenda kwenye maandamano bila kujua watarudi salama au saa ngapi akina mama lazima wahakikishe watoto wanakula nyumbani. Ikiwa mkeo atakuambia kwamba wewe ubaki nyumbani uangalie watoto ili yeye aende kwenye maandamano utakubali?

wengine wajawazito, wengine wako kwenye siku zao, wengine wanapeleka watoto hospitali, etc. etc. kazi ambazo wanaume wakiambiwa wazifanye hawatakubali.

kwa hiyo moyoni wanabeba mzigo mkubwa kuliko wewe unayejieleza kwa vitendo. Lakini kuna ambao wanafika front line kama hiyo picha hapo chini inavyothibitisha. na kuna ambao wanachangia mawazo na pesa! Akina mama, mkuu wangu, watafurahi sana kama tutathamini mchango wao kamili badala ya kuthamini tu mchango wa wale wanaojitokeza barabarani.

Big up Gurudumu.
Uchaguzi umekuewa wa hamasa kubwa wengi hawakuridhika na yaliyotokea, pia hawaridhiki ni hii serekali dhalimu iliyo nunua haki za watanzania.
CCM Walio wengi walijiweka wenyewe hawakuingia kwa ridhaa ya wananchi, aidha walitumia vyombo vya dola kuwa weka madarakani ou kwa kutumia mamlaka walizo nazo kwa nafasi zao. Wengi walipita bila kupingwa kwa kuhujumu na kudhulumu wapinzani kwa vigezo vya sheria au njama.
Wananchi waliuza uhuru wao hasa wa vijijini kwa kurubuniwa na pombe, khanga, kofi na vijisenti.
Walio tumia haki zao vizuri pia zimeporwa.
Hayo yote ndiyo yanayo leta hamu ya kujua kesho vyombo vya habari vitatoka na nini.
Uuzaji wa magazeti umeongezeka sana hasa yale yanayo toa habari za kweli ambayo serekali ina dhani ina mgogoro nayo.
TV diyo zina enea nchi nzima hata kama ni za kulipia kibandani lakini watu wanaingalia na kupembua.
Ni wale wenye maslahi ndiyo wana ona wanaonewa. LAKINI YOTE HAYO YATAKUWA NA MWISHO. CCM IKO ICU. 2015. WOTE WALIOSHINDA KWA HILA HASA MADIWANI NA WABUNGE NJAMA ZA UCHAKACHUAJI KWA MAENEO MENGI YAMEJULIKANA. MFANO 2005 ARUSHA NA UBONGO WALICHAKACHUA. MWAKA JANA IKAWA MWISHO. CCM WASAHAU MAJIMBO AMBAYO WALISHAPOTEZA KWA CHADEMA. MAANA CDM HAWA LALI MPAKA KIELEWEKE. MWAKA 2000 WALIPELEKA MASHAMBULIZI MAKUBWA KWA BAADHI YA MAKADHA MUHIMU KUHAMIA KARATU.
KULIKOMBOA JIMBO SASA HIVI NCHI NZIMA KILA KONA KUNA WAKA MOTO. NA MBAYA ZAIDI WAMESHA KOSA MIJI MUHIMU. LABADA WABAKIE VIJIJINI NI JUAVYO JOGOO LA SHAMBA ATAKUWA NA KAZI MJINI SUMU YA MAGEUZI YA KWELI IPO NDANI YA MIOYO YA WATU.
 
Mkuu, very powerful and touching!

Pia nimefurahi kuwa mtu wa kwanza kukupiga thanks kwa ID yako hiyo Hapa JF
 
Kuna vitu vingine vinauma sana ila nasema iko siku tu hakuna aliyetegemea hata siku moja kuwa Tunisia kutakuja kuwa na mabadiliko na Rais aliyetawala miaka 32 kukimbilia uhamishoni
 
Gurudumu, nchi yetu sio masikini. Masikini kwa sababu gani? Imekosa nini?

Nilikuwa najiuliza kwenye kikao, kila mchangiaji alikuwa anelezea kuhusu elimu duni! Nikajiuliza; ni nani huyu tunayemwambia kuhusu elimu duni ambaye yeye haelewi na haoni? Kwani yeye hakereki? Yeye ndiye anahamisha walimu, yeye ndiye halipi mishahara, yeye ndie hawezeshi walimu kufundisha katika mazingira mazuri! Haoni! Hajali!

Kwenye kata yangu, kuna shule haijanunua kitabu hata kimoja kwa mwaka mzima wa 2010! Hela ipo! Lakini anayetakiwa kusupply anadai uchaguzi ulimzuia!!

Mara moja nikataka kuchukua hatua....awajibike! Duh! Mkataba kasaini na Kamati ya Shule! Kamati ya shule is NOT a legal entity! It has no powers to contract! Nilipoangalia zaidi, mkataba ni wa mwaka mmoja! Haukusema vitabu vitapelekwa lini! Unamalizika Feb 11 so he still is not late 'technically'!

Nilipoongea na Afisa Elimu jibu lake 'mh we acha tu jamani, tuna matatizo mengi jamani'....sasa tatizo liko wapi? Hela zipo, mkataba mbovu! Ni uzembe au tatizo? Au uzembe ndio tatizo???

Kama kamati ya afya tunaongelea afya kinga...usafi wa mazingira! Taarifa ni kwamba kaya elfu 21+ zimekaguliwa! Nikauliza masoko? Hospitali? Misikiti? Makanisa? Hakuna vyoo vya public vilivyotembelewa! Does it make sense???

Lakini cha kushangaza na kukera ni choo cha halmashauri chenyewe! Ni kichafu na kinatia aibu!! Nikashindwa kujizuia! Inawezekanaje kuongelea vyoo vya wilaya nzima na usafi wakati hicho cha anayeoongea ni aibu!??? Hata hilo tunashindwa!

Jibu rahisi, mh tutalifanyia kazi mapema!

Tunashindwa kuweka mipango thabiti ya maendeleo. Elimu ya shule ya msingi tumeidharau. Hatuweki mkazo wa kutosha. Ni nini hii Gurudumu? Kuna haja gani ya kuhangaika na mabarabara na majengo mengine wakati elimu yetu ya msingi ni kituko? Eti naambiwa 'mh hatuna upungufu wa walimu....heri sisi ni mwalimu 1 kwa wanafunzi 45-50. Wengine ni 1 kwa 70..' kwa hiyo sio mbaya! Mwalimu ana vipindi 25 na ni mwalimu mkuu!! Aandae somo, afundishe, asahihishe na afanye kazi ya utawala!

Tufike mahali tuache kila kitu. Kila kitu tuwekeze kwenye elimu ya msingi na sekondari tu!!

Bado sijajikusanya mawazo yangu vizuri ila....

Mapato ni 39+ billion.

Mishahara ni 22+ billion

Miradi ni 10+ billion

Matumizi mengine ni 6+ billion

Unategemea nini hapo?? Bado natafakari!!

hapo we lilia audit ya maafisa watendaji ndo utakapoona madudu ya kukutia wehu!... usichoke kupambana ndugu yangu!
 
Unafaa kuwa mganga wa kienyeji maana unayajua yaliyo moyoni mwa mgonjwa. Hakika bila kupata taarifa mpya huwa siwezi kula. Big up! Lakini lini mabadiliko yatatokea,nchi haina viongozi, CCM wenyewe kwa wenyewe wanalumbana. Matumaini ni kwa CDM tu. Lakini 2015 ni mbali, DOWANS itamwondoa JK, Amen

They keep saying freedom is coming tomorrow. When is tomorrow?
 
mimi mwenyewe niko private lakini jamu ya kupiga kazi haipo natamani kitu kitokee labda maisha yatabadilika. Kuhusu utendaji wa halmashauri zetu huu ni ugonjwa sijui wa aina gani mimi sijui tutautibu na dawa gano. Waheshimiwa wabunge na madiwani wa upinzani wanayo kazi moja tu ya kuonyesha tofauti lasivyo wanancho watakasirika na kuwatoa waote.
Mbunge wetu mdee bado sijaanza kuona kama analeta mabadiliko ya mazoea ya ccm.ninahitaji kimwona akipiya mitaani akiwatia noyo watu washiriki kujiletea maendeleo.
Wananchi tuko tayari kushirikiana naye hata kufanya usafi wa mazingira yetu. Tegeta kwa mfanao ni shehemu yenye watu wegi lakini ni pachafu kwa sasbu hakuna utaratibu wowote wakuzoa uchafu. Watu wana viwanja vidogo hivyohawana eneo la kutupa takatak.
Lazima watu watiwe moyo na viongozi ili washiriki kwenye kutekeleza wajibu wao.
watanzania wapo tayari kufanya kazi na mtu wanayempenda. Mdee anapendwa na watu wa jimbo lake basi anauwezo wakushirikia na wananchi wake kwa urahisi. tunaomba aje tegeta atupatie mikakati ya namana ya kuusafisha mji wa yegeta maana ni mchafu sana.

ndugu yangu, Watanzania tunahitaji kubadilika sana mtazamo wetu juu ya kundi la viongozi. mtu anapokuwa kiongozi sio kwamba anakuwa anajua kila kitu na si kweli kwamba ataweza kufanya kila kitu, yeye anakuwepo kusaidia kuonesha njia na wakati mwingine kusaidia kuweka utaratibu wa kupita njia iliyooneshwa na wengine, tukikaa tukategemea mtu mmoja awe na majibu ya matatizo yanayowasumbua watu zaidi laki moja tunakosea sana.

mapendekezo yangu kwako ni kwamba kwa kuwa umeliona tatizo la uchafu katika eneo unaloishi nakushauri uandae mapendekezo ya namna gani unadhani tatizo hilo linaweza kukabiliwa na kisha umtafute mbunge wako na kuwasilisha pendekezo hilo kwake, umoja ni nguvu ndugu yangu!...
 
Hii ndio hatma ya nchi yetu, for the first time in our history watanzania tumeerevuka. CCM fikra zao bado ziko miaka ya '80 ambayo ilikuwa ukivaa rangi ya kijani wewe ni kila kitu, zidumu fikra "sahihi" za mwenyekiti wa chama. Siamini kama CCM ya leo ina wananchama mil. 5 kama ilivyokuwa kabla ya uchaguzi. I wish Makamba na Kikwete waendelee kukiongoza chama chao mpaka 2015 ili waikabidhi Chadema nchi "kiulaini"
 
They keep saying freedom is coming tomorrow. When is tomorrow?

iyo siku iko karibu kuja hakuna mda maalum ila utaona. wewe jaribu kumbana paka kwenye kona then hakuna mahala pa kutokea utaona matokeo yake. kwa sasa watu wamebabnwa kwenye bei ya vyakula ,usafiri, maji shida ,umeme shida na dhamani ya fedha kuporomoko ndo hapo watakapojaribu kutoka utaona
 
addiction is the word!!!

watendaji wengi wa serikali, ngazi mbalimbali wako hapa JF kama visitors au kama members wanashiriki mijadala na kuchukua mawazo hapa na kujadili one on one. Kuna mtu ameni PM kwamba hata wabunge wa ccm wako hapa wanaikandia ccm kwa kwenda mbele!!

siku moja nianzisha thread hapa nikiuliza je serikali itafunga JF, nikidhani kwamba wanajua kinachoendelea kati ya maafisa wao na JF pamoja na ccm na kwamba wanaweza kufunga JF. Hiyo thread ilipeperushwa ndani ya dakika chache sikuwahi kuiona hadi leo. Niliuliza mods wala sijapata jibu. Sidhani mimi naelewa ni kiasi gani JF iko safe from government attack.

JF ni kijiwe cha lazima kwa kila mpenda mabadiliko, na wato kweli tuko addicted kwa maana kwamba ikipita muda bila kutembelea hapa unasikia unakonda

ni kweli, lakini si umesikia walichokifanya misri? vuguvugu la mabadiliko limeanzia kwenye mtandao, kama ambavyo JF inafanya kwetu hapa, na serikali zetu za kiafrika kama tunavyojua siku zote zenyewe ni reactive never proactive, so usije shangaa likitokea la kublock JF, isitoshe haitakuwamara ya kwanza!
 
Back
Top Bottom