Matapeli wa mapenzi humu JF

ki ukweli kuna mtu humu alinisaidia sana simjui hanijui.ila simtoi shukurani.kwa hiyo watu wema wapo
 
Wandugu!
Tafadhali Chukueni tahadhari na watu (wanawake kwa Wanaume) wanaotangaza kuwa eti wanataka wake au waume huku jamiiforums kumbe wana agenda ya siri nasema haya kwa sababu yamenikuta jana nilimpata mdada humu humu Jamiiforums tukawa tunawasiliana na jana mwanzoni tulikubaliana tukutane MLIMANI CITY baadae akabadilisha akasema tukutane pale MWENGE (Maryland Bar) mi nikakubali akaja kweli muda tuliokubaliana saa 10:30 jioni (Maryland Bar Mwenge ghafla nikavamiwa na group la vijana wapatao wa 4 wanadai ati kwa nini namsumbua kwa kumtongoza kila siku mke wake duuh! kilichonisaidia ni mbio zangu maana jamaa walishuhudia vumbi tu! labda walichofaidi ni bia niliyokuwa nimebakisha hapo mezani lakini kama ndo mpango wao wanipore wamenoa!! KWA HIYO TAFADHALINI kuweni makini,vinginevyo MTALIA SIKU MOJA




Na je hii umepata kuisikia?

Kuna kijana mpevu wa Kitanzania kaenda New York. Yupo katika kijiziara cha muda mfupi watu wanamplia gharama zake full board. Hivyo anakaa katika Hoteli moja bomba.

Huyu kijana kazoea moja moto moja Baridi maeneo ya Getaways. Sijui kama msomaji ulikuwapo wakati Getaways inawika pale makutano ya Mtaa wa Uhuru na Bibi Titi Mohamed. Huyu kijana mpevu hajui afanyeje jioni hii pale New York na yeye ana kiu aina mbili. Ana kiu ya Bia na kiu ya ile sehemu. Kiingereza anajua, kwa hiyo hakuna tatizo la mawasiliano. Kuuliza uliza kaelekezwa sehemu panauzwa bia, na wale binadamu wenye ile sehemu wapo.

Mtoto wa kitanzania katoka taratibu hadi kwenye ile jointi. Pale kakutana na wanywaji wenzake, akiwapo mdada mmoya wa kinyu yok. Katia leather shoes zake safi, rangi ya ngozi ni mweusi yeye utazani wa Zinza Mori. Kijana toka Bongo hakupoteza muda. Kamuongelesha binti yule kwa kiingereza wakaelewana wataondoka wote--lakini kwanza wanywe.

Usiku ukiwa unakaribia kuwa mkuu, kijana wa kitanzania akamwomba sasa huyu mtoto wa kinegro watoke kuelekea kwenye ile hoteli ya kifahari alikofikia. Mtoto kakataa: "No I don't sleep in hotels." (Tafsiri? Mi silali mahotelini, akasema). Kijana akaanza kujisikia hovyo. Nadhani unajua inakuwaje unapokuwa umejiandaa kumpa mtu kitu kisawasawa halafu picha inakuwa kama inaharibika.

Ila pakawa na bahati kidogo kumbe. Yule binti akamwambiaje? We kama una hiyo kiu? Twende kwangu. Eti huyu kiijana wa Kitanzania kakubali baada ya kuambiwa si mbali sana kutoka bale baa. Yule binti kaanza kuongoza njia kuelekea kwene uchochoro fulani una kijigiza hivi. Mara zikatokea njemba. Mijibaba minne. Kijana kakwidwa.

"Search him fast," njemba mmoja anaamuru apekuliwe mifukoni haraka. Kwa bahati mbaya fedha zote alizotembea nazo zikawa zimeishia baa. akawa kabakisha dola moja tu. Yule alokuwa anampekua akahamaki: Unataka binti wa New York kwa dola moja? Una akili wewe? Katika majibizano lafudhi ikaonesha huyu kijana si Mwamerika.

"Where you from?" Njemba moja likauliza.
"Tanzania," kijana akajibu.
"Where is that?" Njemba jingine likauliza kwa kutokujua Tanzania ndo wapi.
Maelezo yakaonesha huyu kijana katoka Afrika.

Wakamzaba kofi na kuamuru, "get lost...." Nasikia na ile dola moja haikurudishwa.
 
kinachonifurahisha kuhusu MMU watu wanajadili story za kutunga .. na wanakuwa busy kweli :lol:
 
Umejitakia mwenyewe unatong'oza mtu ambaye hujawahi kumwona je kama ni mdogo wako unaenda unamkuta ndo uliyemtong'oza inakuwaje wangekupa wangekulawiti ungeenda kumshitaki nani ?:)
 
Mkuuu funguka bwana, ulichat na ID gani humu JF, hio KUSEMA BILA KUMLIPUA MUHUSIKA SI DAWA! Ukute big name!!!! LOL! Sipati picha ukaona umejipatia BONG YA SHORIIIII!BURE BURE! USHAJIPANGA KUMUONJAAA!!!!LOL! Ndo dawa yenu waonjaji!!!!! Pale Maryland kuna guest kibao karibu ikiwamo Raibow Hotel Na Kebbys Hotel! Sijui ulilipia chumba ipi? LOL! Anyway siku zote BLIND DATES ni mbaya unaweza chat na mtu kumbe Mama/Dada yako, bora wewe mke wa mtu!! LOL!

gesti za mjii huu zote wazijua? lol
 
Jamni alichoandika huyu jamaa ni cha kweli mwaka janaa mwezi wa sita dada yangu alitapeliwa na kijana aliyemkuta humu sh milioni mbili bahati nzuri to cut it short jamaa alijitia nafanya kazi tume ya mipango viwanja vinatolewa sister ampe pesa akampa 2m mnajua tena watoto wa kike sasa sisiter kamkamata yule jamaana full contact anazo nshamwabia mara kibao tumtamngaze humu anasema tuvute muda kwanza kozi mambo yapo police nawaambieni kuweni makini humu hasa kina dada

Kosa ni la dada yako, wewe utampaje mtu hela usiyemfahamu? Ukitumia mitandao ujue pro & cons zake. kwa jinsi hiyo dada yako anaweza kutapeliwa hata na mpita njia, hivyo don't blame JF bali uzembe wa dada yako.
 
Kosa ni la dada yako, wewe utampaje mtu hela usiyemfahamu? Ukitumia mitandao ujue pro & cons zake. kwa jinsi hiyo dada yako anaweza kutapeliwa hata na mpita njia, hivyo don't blame JF bali uzembe wa dada yako.

subiri na we huyo alikuvisha pete akuache ndo utajua kosa la nani
 
Kosa ni la dada yako, wewe utampaje mtu hela usiyemfahamu? Ukitumia mitandao ujue pro & cons zake. kwa jinsi hiyo dada yako anaweza kutapeliwa hata na mpita njia, hivyo don't blame JF bali uzembe wa dada yako.

Halafu soma elewa ndo uandike nani kalamu jf/nitahadharisha watu we unaongea kulaumu?kumbe aliyekuvisha pete umemtoa humu?bora huyo dadangu aliyetapeliwa pesa si inatafutwa tu?utakachotapeliwa wewe ndo utajua kutapeliwa hakuna mwenyewe
 
ID itasaidia nini na wakati mtu anaweza kubadilisha na kuja na ID mpya pengine hata yumo humu na kuchangia hoja anachangia

Nakubaliana na wewe sioni sababu yakumtaja uyo mwanamke unless kama ni premium memba mwenye reputation yake!:photo:
 
Halafu soma elewa ndo uandike nani kalamu jf/nitahadharisha watu we unaongea kulaumu?kumbe aliyekuvisha pete umemtoa humu?bora huyo dadangu aliyetapeliwa pesa si inatafutwa tu?utakachotapeliwa wewe ndo utajua kutapeliwa hakuna mwenyewe

Siwezi kutapeliwa kirahisi mitandaoni. Ulinivisha wewe hiyo pete? mbona umenivalia njuga mkuu? nimekuibia mume nini?
 
hahahahaaa, unajua nilipokuwa nasoma huu uzi,nlikuwa namhurumia kweli ila hapo mwisho pakanivunja mbavu....
hilo ni fundisho bwana ukitaka kudate humu hakikisha una mbio za kutosha.....

chezeya JF alaaaa...............

Saivi mtu mkishapeana appointment unaenda na bodaboda tena ikiwa silence, kikinuka tu.. Vumbii..
 
Kwahiyo mbio zako ndio zimekusaidia amasivyo yangekukuta makubwa,pole lakini punguza kuzoeana na watu na nakutaka kuonana nao wengine sio watuuuuuuuu!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom