Matapeli wa Kisiasa

Mtz wa A-town

New Member
Aug 17, 2012
2
0
Binadamu tofauti na wanyama wengine ana uwezo wa kutambua mema na mabaya. Mema yanaweza kuwa ni mambo mazuri yanayokubalika katika jamii au dini . Kwa mfano kusaidia maskini na heshima kwa wenye umri mkubwa. Mabaya yanaweza kuwa ni mambo ambayo yanakatazwa na jamii au dini. Kwa mfano mauaji na ujambazi. Mara nyingine sheria inatoa muongozo wa mambo mema na mambo mabaya.

Tunapaswa kufuata mambo mema na kuacha na kukemea mambo mabaya ili jamii yetu iwe na amani, umoja, ushirikiano na upendo. Jamii ambayo haitaweza kuondoa mabaya haitakuwa na maendeleo. Kwa mfano, nchi ya Nigeria inapitia machafuko ya kisiasa kutokana na kundi linalojiita Boko Haram. Somalia wapo Al Shabaab ambao wanatishia amani. Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo haina amani kutokana na waasi wa M 23. Inasemekana kwamba, kama Kongo itatumia vizuri rasilimali iliyo nayo, itakuwa ni nchi tajiri kuliko zote duniani. Nigeria inachimba mafuta lakini bado wananchi wake wanaishi kwenye hali duni. Inawezekana fedha nyingi zinatumika kupigana na Boko Haram. Na nchini Somalia, shughuli za maendeleo zinakwamishwa na mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na Al Shabaab.

Hapa kwetu Tanzania kuna chama kimoja cha kisiasa ambacho sielewi madhumuni yake halisi. Sitakitaja hiki chama kwa jina lakini naomba nikiite chama ‘Fulani. Wakati bajeti ya wizara ya ardhi inasomwa bungeni, nilimsikia mbunge mmoja wa kike wa chama hiki akitamka bungeni kwamba anawaruhusu wananchi wa jimbo lake kuchukua sheria mkononi iwapo jeshi la polisi halitatoa ushirikiano kwenye migogoro ya ardhi. Kuna mbunge mwingine wa chama hiki, ambaye alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, alitoa albamu inayoitwa ‘Anti virus’ ambayo imejaa lugha ya matusi dhidi ya kampuni ya Clouds Entertainment na wafanyakazi wake. Pia kuna mbunge mwingine wa chama hiki alitolewa bungeni kwa kosa la kutoa lugha ya dharau dhidi ya rais na kukataa kufuta kauli yake. Hii ni mifano michache tu. Makosa mengi ya kuvunja kanuni za bunge niliyoyashuhudia yanafanywa na wabunge wa chama hiki. Sijaribu kutetea chama tawala au chama chochote kile kwasababu mimi sio mwanachama wa chama chochote cha kisiasa.

Je, wabunge si watu wa kuheshimika ndio maana wanaitwa waheshimiwa? Kama ni waheshimiwa kwanini wabunge wa chama Fulani hawana maadili bungeni na kwenye jamii? Kwanini wanatumia lugha ambazo zinachochea fujo na ukosefu wa amani? Wengine wanadhani kwamba bunge linaendeshwa kidikteta lakini wamesahau kwamba Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Kama kungekuwa kuna udikteta kusingekuwa kuna vyama vya upinzani au uhuru wa vyombo vya habari. Kungekuwa kuna chama kimoja tu, gazeti moja tu la serikali, na shirika moja tu la utangazaji wa redio na runinga. Pia kungekuwa na kampuni moja tu ya simu na mtandao. Taarifa zote za simu na mtandao zingekuwa mikononi mwa serikali. Serikali ingechuja mtandao wa intaneti kuhakikisha kwamba hakuna taarifa ambayo serikali haitaki wananchi waipate.

Hata kama wabunge wa chama hiki wanaonewa na serikali, kwani kufanya fujo ndio suluhisho? Hata kama wabunge wa chama tawala wanapindisha sheria, kwani kuvunja sheria ndio suluhisho? Hata kama wananchi wanaonewa na kudhulimiwa na serikali, kwani wakipigana na kuuana watapata haki zao? Hata kama haki ikipatikana kwa kufanya fujo, je wale walioathiriwa na fujo hizo hawatalipiza kisasi miaka ya baadae? Uchaguzi hufanywa kila baada ya miaka mitano. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 chama tawala kilipata asilimia sitini ya kura zilizopigwa. Wengine wanadhani kwamba chama tawala kiliiba kura. Hata kama ni kweli waliiba kura, kuna kikomo cha uwizi wa kura. Kwa mfano, kama asilimia tisini ya wapiga kura wakiamua kukipigia kura chama cha upinzani, chama tawala kitahitaji kuiba asilimia hamsini za kura zilizopigwa ili waweze kushinda. Je inawezekana asilimia hamsini na kura zilizopigwa kuibiwa? Uwizi wa kura unazidi kuwa mgumu na wakati mwingine hauwezekani pale ambapo kuna tofauti kubwa za kura walizopata wagombea.

Kawaida ya chama Fulani ni kutoa shutuma nzito dhidi ya viongozi wa serikali. Eti wanadai wanapiga vita mafisadi. Ukitaka kuzuia malaria inabidi uondoe vyanzo vya mazalia ya mmbu na utumie chandarua chenye dawa. Huwezi kuzuia malaria kwa kupigana na wagonjwa wa malaria. Vivyo hivyo, ukitaka kupambana na ufisadi toa mapendekezo ya kuziba mianya ya ufisadi badala ya kutoa shutuma zinazofanana na hadithi za sungura na fisi. Ni heri kupigana na maadui wakubwa wa nchi hii ambao ni ujinga, umaskini na maradhi kuliko kupigana na watu wanaodaiwa kuwa ni mafisadi. Kwasababu wafuasi wa chama Fulani wanapenda sana shari, wakikosa mtu wa kupigana naye watapigana wenyewe kwa wenyewe. Wanasema wanaleta ‘vuguvugu ya mabidiliko’ au M4C. Mabadiliko gani wanayotaka kuleta? Hayo mabadiliko ni ya maendeleo au? Wanakusanya fedha za nini? Je, ni za kujenga zahanati na visima vya maji? Je ni za kununua vifaa vya hospitali? Je ni za kununua vitabu, madawati na kujenga shule kwenye majimbo yao?

Kuna kitabu kinaitwa Makuadi wa Soko Huria. Sijakisoma kitabu hiki. Labda makuadi hawa ni watu wanaotumia soko huria kama fursa ya kujinufaisha bila kujali mtanzania mwenye kipato cha chini. Inasemekana na inaonekana kwamba baadhi ya watu hawa wapo serikalini. Tumesikia baadhi ya kesi zinazohusisha makada wa chama tawala. Upande wa upinzani pia kuna watu ambao sio wazalendo. Hatutakosea kama tukiwaita Matapeli wa Kisiasa. Watu hawa wanatumia umaskini wa mtanzania kumfanya mtanzania achukie serikali yake. Matapeli hawa ni viongozi wa chama Fulani na wanafanya hivyo ili kupata madaraka watakapogombea kwenye uchaguzi ujao. Lakini sio viongozi wote wa chama Fulani ni matapeli. Matapeli hawa wanataka watanzania waamini kwamba serikali yote ya chama tawala haifai, imeoza, na ni ya kifisadi. Hii si kweli hata kidogo. Ni kweli kwamba serikali yetu ina mapungufu lakini kuna baadhi ya viongozi wa chama tawala ambao ni wachapakazi.

Bila kujali chama, kila mwananchi anapaswa kuheshimiwa kwasababu ni haki yake ya msingi kama binadamu. Ili Tanzania iendelee itabidi tuwe wamoja, tuheshimu tofauti zetu na tuishi kwa amani. Kila mwananchi ana haki sawa na mwingine ya kumchagua kiongozi anayemtaka. Itakuwa vyema kama vyama vya upinzani vikishindana na serikali ya chama tawala kwenye maswala ya utendaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Watanzania tusisikilize kelele za jazba bali tuangalie utekelezaji.

Ibara ya 20 (1) (c) ya katiba ya sasa inasema “haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa” kwahiyo serikali inabidi ichukue hatua za haraka kuilinda nchi yetu dhidi ya maadui wa nje, na hasa wa ndani.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Back
Top Bottom