Matapeli wa internet

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
MATAPELI WA INTERNET.

Kuna email inatumwa ikiwa na subject ya "Yahoo Update" au "Gmail Update" au "Hotmail Update". Hii Email inauliza User Name, Password, Birth Date, na Country. Tafadhali usijaze wala kuijibu email hiyo. Ni watu wanaofanya biashara ya utapeli. Ukijibu email hiyo, hutaweza tena kufungua email account yako tena. Password yako itabadilishwa, na email account yako itapata mmiliki mpya ambaye ataanza kuifanyia biashara za kitapeli. Rafiki zako watatumiwa email kwamba umekwama nchi fulani, na unahitaji msaada wa kifedha. Tafadhali kuwa makini sana . Eneza ujumbe huu kwa rafiki zako wote. Forward email hii kwa rafiki zako wote. Kwa sababu za kiusalama na unyeti wa taarifa hii, tafadhali usibadili lugha ya email hii. Iforward kama ilivyo.
Ahsante.

.................................................................
TAHADHARI

Usipende kujiregister katika mitandao usioelewa wanamadhumuni gani, especially wanaotoa offer za vitu au pesa, ni geresha tu na wanajua mwishowe wakikuomba password utatoa ile unayotumia katika mail address yako, msidanganyike!!
 
Utapeli huu pia unatumika katika kuwatapeli watu wenye huduma za online banking kwa kuwaambia wafanye updates katika security details halafu wanaingia kwenye account yako na kuchota mapesa... tujihadhani mno ndo watu wanatesa kwa miondoko hii.
 
Back
Top Bottom