Matangazo ya Zanzibar Bwana utachoka mwenyewe!!

Hujakuta yale matangazo ya mtaani ambapo sentensi zimeunganishwa kutoa sentensi moja.
HAPATUNAUZASODANA MAJIBARIDI. huo ni fano, just visit mji mkongwe uchanike mbavu

hahaaaa tangazo limeniacha hoi hilo
 
Kipindi cha kampeni za uchaguzi nilikuwa nasikiliza maeneo yanayo tajwa kufanyika mikutano ya kampeni ya vyama, nilikuwa nashangaa majina ya sehemu hizo, utafiki mtangazaji alikuwa analitaja eneo hilo kwa jina la utani kumbe yuko serious 100%!
 
Nadhani hakuna kipya, kama kuna kingereza cha UK, USA, South Africa, Zimbabwe n.k , Basi na kiswahili ni hivyo hivyo kipo cha Dar, Mombasa, Zanzibar, DRC, nk kwa hiyo tofauti zitakuwepo !
 
hahahahaa! this is nice one, yani kwao wao, moshi ndo problem, basi wafuta bhange hapo ndo panawafaa, kwa mana wanameza moshi wooote kabisa.

sijaona tatizo nafkiri kwa wasomi wa psychology wanaweza wakasema huo ni moja ya mifano ya "positive reinforcement" nafkiri tangazo lipo straght forward kama unaweza USITOWE MOSHI
and sure moshi wa sigara ndiyo unao waathiri wasiovuta.. (wale wanaokuzunguka..)
 
Hiyo ndo zanzibar zaidi uijuavyo!!wanvituko waonehivyo huku wakiuza chips temeke na msasani!!
 
Yaani nyinyi wabara ambao mumejifunza kiswahili huko munakoita shuleni, ndiyo mumekuwa wabora kwa kiswahili kuliko wenyewe wenye lugha!

Ama kweli dunia imekwenda songombingo, kha!

Nina hakika hata hamujui maana ya hiyo mwembe mchomeke mutabaki kucheka tu.

kwenye red umekosea au ndiyo uandishi sahihi?
 
Nilifika Zanzibar mwaka 1992 nikapita eneo moja kulikuwa na shule moja karibu na soko, kibao cha utambulisho wa shule hiyo kilikuwa kimeandikwa "SKULI YA MARIKITI" Sasa nikajisemea si bora tu wangeandika kiingereza Market Primary School? Sijui kama bado inaitwa hivyo au wamabadilisha, sijaenda tena, mwenye taarifa anaweza kunijibu.
 
Hapa leo nimecheka kweli wakuu...kuna mtaa eti unaitwa mwembe mchomeke..:eek:....kunatendaka nini hapo wajameni?

Gaadeem wazenji wangu leo mumeliwa!

Kibunango yuko wapi aje kutetea huu wazimu!

Sasa wewe unadhani nimelitunga hilo jina, yaani hilo lipo, hebu cheki na hii orodha
1-MAKUNDUCHI
2- BWEJUU
3-KICHAKA PUNDA
4-KITOPE
5-KIBOJE
6-DARAJA BOVU UNASHUKA SKULI YA MTO PEPO
7-MTUNDANI
8-BINGUNI
7-KIEMBE SAMAKI
8-JIA LA UZI
9-MFEREJI MARINGO
10-TUNGUU
and so much more, ukiwa Zenj utacheka hadi ufariki maana kila kitu kwako wewe mbara ni kituko, cheki sentensi hii BWANA PANDU ABDALA SUDI KAMTOA MWANAE SKULI YA KIBONDENI KAMTIA DOLE- yaani mtoto kahamishwa kutoka shule ya kibondeni kapelekwa shuli ya dole kazi kwako sas, ktk gari ze2 zile mzuri nana maana mnatazamana mtu hushuka pale anapofika mlangoni kwake, utasikia WEYE KHEE NITIE HAPOOOO........................... inakutosha kwa leo
 
na ukitaka kucheka zaidi hebu tupia jicho TVZ au TV zuzu yaani taarifa ya habari inasomwa na makame usi, repoter faki makame faki, eneo la tukio mwembe mchomeke, wilaya ya magharibi mkoa wa kusini unguja

Nyani haoni kundule!!!
 
wameathirika na lugha yao ya kipemba...hata kiingereza huwa wanachanganya hivyohivyo. international(inteneshino) wao husema internashonal'i), chemical(kemiko) wao husema Kemikal'i) yaani wanashika ile elo/L ya mwishoni hawaachii. professional (profesheno) wanasema profeshenal'i).

Hivyo unajuwa hili la kuathirika na ndio maana una mgogoro kati ya "r" na "l"? After all Kiswahili si Kisukuma wala si Kihaya bali ni Kiswahili na chimbuko lake ni kwa hao unaowakejeli oops unaowakejeri (li)
 
Sasa wewe unadhani nimelitunga hilo jina, yaani hilo lipo, hebu cheki na hii orodha
1-MAKUNDUCHI
2- BWEJUU
3-KICHAKA PUNDA
4-KITOPE
5-KIBOJE
6-DARAJA BOVU UNASHUKA SKULI YA MTO PEPO
7-MTUNDANI
8-BINGUNI
7-KIEMBE SAMAKI
8-JIA LA UZI
9-MFEREJI MARINGO
10-TUNGUU
and so much more, ukiwa Zenj utacheka hadi ufariki maana kila kitu kwako wewe mbara ni kituko, cheki sentensi hii BWANA PANDU ABDALA SUDI KAMTOA MWANAE SKULI YA KIBONDENI KAMTIA DOLE- yaani mtoto kahamishwa kutoka shule ya kibondeni kapelekwa shuli ya dole kazi kwako sas, ktk gari ze2 zile mzuri nana maana mnatazamana mtu hushuka pale anapofika mlangoni kwake, utasikia WEYE KHEE NITIE HAPOOOO........................... inakutosha kwa leo

mchamba wima...mfenesi mazizi
 
Hapa leo nimecheka kweli wakuu...kuna mtaa eti unaitwa mwembe mchomeke..:eek:....kunatendaka nini hapo wajameni?

Gaadeem wazenji wangu leo mumeliwa!

Kibunango yuko wapi aje kutetea huu wazimu!

Akili za uzinzi uzinzi ndio zinazowaponza! Utajisikiaje kama hapo ni pahala ambapo abiria anachomekwa katika gari? Lipi la ajabu Muembe au kuchomeka?
 
Tatizo la Lugha sio la watu wa Zenj tu, ni watu wote wa pwani ya bahari ya Hindi wanaojifanya waswahili.
Mfano Wazaramo, utakuta wao wanadai wanajua Kiswahili lakini sikiliza maneno yao, anamwita mtoto '' we ntoto'' au mkono wa kushoto, ''Nkonomsosoto'' jingine ''we ntoto ng'onjwa'' Taaaaaaaaaaaaabu kabisa!!!:A S 109:
 
Nilifika Zanzibar mwaka 1992 nikapita eneo moja kulikuwa na shule moja karibu na soko, kibao cha utambulisho wa shule hiyo kilikuwa kimeandikwa "SKULI YA MARIKITI" Sasa nikajisemea si bora tu wangeandika kiingereza Market Primary School? Sijui kama bado inaitwa hivyo au wamabadilisha, sijaenda tena, mwenye taarifa anaweza kunijibu.

Tatizo kubwa usipojijua! Hepu waulize wenzio wakwambie hilo neno shule ni lako?
 
Sasa wewe unadhani nimelitunga hilo jina, yaani hilo lipo, hebu cheki na hii orodha
1-MAKUNDUCHI
2- BWEJUU
3-KICHAKA PUNDA
4-KITOPE
5-KIBOJE
6-DARAJA BOVU UNASHUKA SKULI YA MTO PEPO
7-MTUNDANI
8-BINGUNI
7-KIEMBE SAMAKI
8-JIA LA UZI
9-MFEREJI MARINGO
10-TUNGUU
and so much more, ukiwa Zenj utacheka hadi ufariki maana kila kitu kwako wewe mbara ni kituko, cheki sentensi hii BWANA PANDU ABDALA SUDI KAMTOA MWANAE SKULI YA KIBONDENI KAMTIA DOLE- yaani mtoto kahamishwa kutoka shule ya kibondeni kapelekwa shuli ya dole kazi kwako sas, ktk gari ze2 zile mzuri nana maana mnatazamana mtu hushuka pale anapofika mlangoni kwake, utasikia WEYE KHEE NITIE HAPOOOO........................... inakutosha kwa leo

Keko
kiwalani
msasani
sinza kwa wajanja
kunduchi
salasala
tangi bovu
kariakoo (nafikiri sahihi ni kaliakoo
Hebu tuelezeni uhodari wa majina haya hata kwa wenzenu muone vichekessho?
 
Back
Top Bottom