Matangazo ya Biashara Yazua Balaa....!

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Mama mmoja mjamzito - ujazito wake ukiwa kama miezi minane hivi - aliingia ndani ya basi na kuketi tayari kuanza safari. Mara akamuona kijana mmoja (umri upatao miaka 20 hivi) anamwangalia sana, mama akakerwa na akahamia kiti kingine. Kijana akazidi kumwangalia, safari hii akitabasamu. Mama akahamia kiti kingine, mara hii kijana akaanza kucheka. Mama akahamia mbali kidogo, yule kijana kuona mama alipokaa akaangua kicheko kikubwa hadi machozi yakamtoka.

Mama akalalamika kwa dereva kwamba kijana amemdhalilisha kwa kumcheka bila sababu ya maana. Dereva akapeleka basi polisi, kijana akakamatwa na kesho yake akapelekwa mahakamani.
Hakimu kwa ukali akamwambia kijana ajieleze kwa nini alifanya ufedhuli kama ule kwa mama mjamzito. Kijana akamwambia hakimu:

"Mheshimiwa, huyu mama alipoingia ndani ya basi sikuwa na jinsi ya kukwepa kuona kuwa alikuwa mjamzito. Kiti cha kwanza alichokaa juu yake kulikuwa na tangazo linasema PIPI KIFUA PACHA ZIPO NJIANI, nikatabasamu. Akahamia kiti cha pili, nacho juu yake kulikuwa na tangazo linasema SALIMIA INGEPUNGUZA UVIMBE, nikajizuia kucheka japo kwa shida. Alipohamia kiti cha tatu juu yake kulikuwa na tangazo lililosema SOSEJI ZA FARMER'S CHOICE NDIZO ZILIZOMSHIBISHA na nikashindwa kujizuia kucheka. Alipohamia kiti cha nne tangazo lilikuwa SALAMA CONDOM INGEZUIA TATIZO HILI hapo ndio nikaishiwa na nguvu kabisa na kuangua kicheko cha nguvu".

Hakimu akaifuta kesi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom