Matangazo la Fataki yanadhalilisha?

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Kuna haya matangazo ya Bwana Fataki yanaelekea yanadhalilisha kuna lingine linasema unaweza kumnunulia kabinti chips na soda kazi kwisha na lile lingine fataki anaambiwa akimnunulia gagulo la mtumba ni tosha kumpata mtoto yaelekea Fataki ni baab kubwa kwenye masuala ya mahusiano au nyie mwaonaje?
 
Mimi naona yanasaidia sana awareness hasa ya wazee wamelo kama fataki...ma binti wawe makini sana maana mafatakiwamezidi...na nawaasa sanadada zetu wasiwe na tamaa yavitu vidogo vidogo kama simu,vocha,nguo etc...wajitahidi sana kuepuka vishawishi.
 
Yes kama yanasaidia lakini watoto wa siku hizi wanapenda sana simu na nitumie vocha watasalimikaje kwa hao Mafataki
 
Ni kweli hawawezi kukwepa,maana siku hizi chips,vocha na lift vimewakaa sana kichwaniwatoto wa kike.
Ukizaa mtoto wa kike siku hizi akikua tu ukae nae haswa mambo ya ubize uyasahau la sivyo utakuta Fataki kamaliza kazi na kaacha ukimwi.
 
watoto wengi huwa wanapenda kupokea hizo chips na vijisimu,yes,sometime kwa kutikujua kuwa ni mitego ya kuwanasa.kwa kutumia matangazo ya fataki unawaweka aware kuwa mambo hayo si mazuri na yanaweza kuwaambukiza maradhi ya zinaa,naona waweke na yanayowalinda watoto wa kiume sasa,coz kuna mafataki wakike pia wengi tu!
 
Kwa bahati mbaya Ngomanzito haukusema yanamdhalilisha nani, lakini iwapo yanamdhalilisha Fataki nadhani ni jambo la kheri kwani lengo haswa ni hilo na pia kuwahimiza watu wengine waacha tabia za Fataki. Lakini pia iwapo linawadhalilisha wasichana wanaouza utu wao kwa chipsi na Magaguro pia ni heri kwani tabia hii haistahili pongezi hata kidogo. Sina kabisa tatizo na matangazo haya ya fataki hasa ya redio lakini kama mtu amebahatika kuona matangazo haya kwenye mabango(hospitali ya Magomeni barabara ya Kawawa na kituo cha afya cha Palestina barabara ya Shekilango) yanapotosha kwani picha iliyochorwa ni ya mtu mnene kupindukia na mwanafunzi. Hatari ya hii ni tafsiri kwamba Fataki ni lazima awe mnene hivyo kupoteza maana ya awali( watu wataangalia umbo na sio tabia) na wanaotakiwa kukingwa na Fataki ni wanafunzi tu.
N.B
Katika kufikisha ujumbe kwa picha msisitizo huwa unaweza kunesha kwa utofauti au kuongezea chumvi mazingira. Katika picha ya Fataki msanii kamfanya fataki kuwa mnene mno na hivyo kuufanya ujumbe wake kusisitiza unene wake na si tabia zake.
 
Ni kweli hawawezi kukwepa,maana siku hizi chips,vocha na lift vimewakaa sana kichwaniwatoto wa kike.
Ukizaa mtoto wa kike siku hizi akikua tu ukae nae haswa mambo ya ubize uyasahau la sivyo utakuta Fataki kamaliza kazi na kaacha ukimwi.

KATABAZI KATABAZI, ukizaa mtoto wa kuime usilemae, mafataki wako wengi tena hata wa KIKE vivulana vidogo vinatongozwa ni balaa, KEEP YOUR EYEZ OPEN.
 
Kuna haya matangazo ya Bwana Fataki yanaelekea yanadhalilisha kuna lingine linasema unaweza kumnunulia kabinti chips na soda kazi kwisha na lile lingine fataki anaambiwa akimnunulia gagulo la mtumba ni tosha kumpata mtoto yaelekea Fataki ni baab kubwa kwenye masuala ya mahusiano au nyie mwaonaje?

Kaka hayo matangazo hayadhalilishi yeyote, ni hali halisi iliyo huku kwetu... na kwa kusema ukweli, FATAKI ni character aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa ku-raise awareness ya mahusiano hasi kati ya wazee na watoto wa shule [hali ndugu yangu ni mbaya sana hapa nyumbani - baadhi ya watoto njaa imezidi na baadhi ya wazee kiu imezidi, kwa hiyo ni tamaa tupu]

Kama kwa namna yoyote kutakuwa na udhallishaji (ambao mimi siuoni), basi utakuwa kwa wale wanaodhalilisha jamii yetu na hiyo tunasema "HONORS EVEN"
 
KATABAZI KATABAZI, ukizaa mtoto wa kuime usilemae, mafataki wako wengi tena hata wa KIKE vivulana vidogo vinatongozwa ni balaa, KEEP YOUR EYEZ OPEN.

Hivi Mbona hayo matangazo hawaelezei vijana wa kiume wajikinge na mafataki wa kike ambao siku hizi wamekuwa wengi??
 
Mugabe ana miaka 86 mke wake ana miaka 46, kawawa ana mika 82 mke wake ana miaka 39 na malecela ana miaka 80 mke wake ana miaka 44 !!!! Je na hao pia ni MAFATAKI?
 
Mugabe ana miaka 86 mke wake ana miaka 46, kawawa ana mika 82 mke wake ana miaka 39 na malecela ana miaka 80 mke wake ana miaka 44 !!!! Je na hao pia ni MAFATAKI?
Kawawa inafaa ashitakiwe kwa sheria za Tanzania, 82-39 = 41 amemzidi mkewe kwa miaka 41.
 
4000d1238136173-matangazo-la-fataki-yanadhalilisha-kpleo11.jpg
Kawawa inafaa ashitakiwe kwa sheria za Tanzania, 82-39 = 41 amemzidi mkewe kwa miaka 41.

Check Kp leo haya mambo yapo
 
Attachments

  • kpleo11.jpg
    kpleo11.jpg
    16.7 KB · Views: 64
Back
Top Bottom