Matamu na machungu katika tuzo za mwaka 2011 kwa wana-habari

babykailama

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
251
243
Kupitia Television nimeona,:cool2:



1. Kazi nzuri ya walioandaa Majaji, Mc's makini, ukumbi uliopambwa vyema na zawadi zinazofaa.


2. Kwa ujumla, hotuba nzuri ya Mgeni rasmi, Mh. J. Kikwete, Rais wa JMT, imegusa maeneo nyeti juu ya Tasnia ya habari.


3. Maelezo Rais katika hotuba, yanayohusu barabara ipitayo hifadhini na ujenzi Airport Mugumu katika hotuba hayajitoshelezi. Hakika Rais angekuwa ame adress hayo siku nyingi waziwazi katika jukwaa lingine na si kusubiri katika TUZO kwa Wana-habari. Kusifu Mzee wa Kikombe wakati kuna maumivu makubwa yaliyowapata Wananchi kuhusu utapeli huo si sahihi. Aidha ameweza kufanya tufikiri kuwa kumbe sababu za vyombo vya Umma na Wizara ya Afya kuanza kushabikia (kutoa support) ya miundo mbinu katika huduma ya huyo Babu haraka haraka bila upembuzi wa Kisayansi ilikuwa kumbe ilikuwa ni issue ya ku-draw attention juu ya barabara ipitayo hifadhini!!


4. Maandalizi hafifu ya utaratibu wa utoaji tuzo jukwaani (mara anayeitwa si aliyepo pale, mara anayetakiwa kutoa zawadi hajafika na zaidi ya yote, niliwahurumia wale nominees wengine ambao hawakupata tuzo kuachwa wanateremka toka jukwaani kama hawakufanya kazi yoyote ya maana. Kama huna cha kuwapa (runners) usiwapeleke jukwaani period!


Otherwise, ni tukio la kuigwa katika Taaluma / Tasnia nyinginezo pia .
 
Unaweza kututajia walioshinda tuzo? Si wote tuliofanikiwa kutazama tv!
Mkuu Maranya kuna uzi wa Byabato ulikuwa unatoa matukio live na wote waliopata tuzo wapo pale. Ningekuwekea uzi hapa ila natumia kasimu ka mchina.
 
Pamoja na mapungufu anayoyaainisha babykailama, hiyo hafla ilifana na ni historia. Naipongeza MCT na wadau wote walioiandaa bila kusahau washindi na nominees wote. Keep it up!
 
Hivi websites/blogs kama jf,michuzi,mwanabidii,bongostaz etc sio vyombo vya habari? Kama jibu ni ndio kwa nini sina kina bishanga hatujawa nominated?
 
Back
Top Bottom