Matamshi ya Pinda yanapoitwa makubaliano

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
eti mojawapo ya makubaliano kati ya madaktari na serikali ni ongezeko la call allowance!huu ni uongo mwingine wa Pinda kwa sababu amesahau kiwango hiki alikiweka yeye pale CPL bila kujadiliana na madaktari.

on call allowance.jpg
 
madaktari komaeni mpaka mpewe chenu acheni maneno ya wanasiasa wanaokaa kwenye viyoyozi huku ninyi mnasota na harufu za madawa mahospitalini
 
Huku habari za mgomo zikishika kasi na madaktari wakiwa wamejiandaa vilivyo nimeweza ona tangazo hili hapa chini

403524_427163087328223_273504788_n.jpg

Pia nimepata sehemu ya barua ambayo ndiyo imeitwa makubaliano na madakatari kwa hakika nimeshangazwa kwani nilijua serikali imekaa na madaktari kumbe imewaandikia kipande cha karatasi kama nilivyofanikiwa kukinasa hapa chini.Kama serikali ilikiri waziwazi kuwa madai yao ni ya msingi na watayashugulikia kigugumizi hiki kinatoka wapi?Madaktari wanakana katika madai yao hawajawahi kuomba nyongeza ya uchunguzi wa maiti(postmortem) je hii propaganda yakusema wameongeza kutoka elfu kumi hadi laki moja ni kuwafanya watu wasioelewa waone kuwa wao ni wema au?Tujiandae na uchungu mkali ambao unaweza kuwa tiba ..............kweli uzaifu.

MAT.PNG

Linganisha na hii ya mwaka 2010

545540_374225125973599_795674788_n.jpg

250775_374408232621955_1908721227_n.jpg
 
Hii bajeti haina maana kabisa, Madaktari gomeni!

Shetani kaa pembeni kipindi hiki cha mgomo usije ukaleta kiherehere chako!

Lema komaa na M4C wakati wenzako wako mjengoni!
 
Kudhihirisha walivyo dhaifu na waongo, ona serikali legelege wamekimbilia mahakamani kuweka pingamizi (zuio). Hawana akili kujua kuwa huwezi lazimisha punda kunywa maji!

Kama walikuwa na makubaliano, watupe nakala ya hayo makubaliano kati ya pande mbili husika.

Naomba kujua lile la kutokuwa na imani na Pinda (serikali) limeishia wapi, ni muhimu kuitoa ccm madarakani haraka,
 
makubaliano ni lazima yaridhiwe na pande zote zinazopingana na si vinginevyo.
 
wapendwa,

japo siungi mkono mgomo wa madaktari, lakini hii habari ya 25,000 kwa wataalam bingwa, 20,000 na 15,000 KWA SIKU ni DHIHAKA, HAIKUBALIKI!

jamani kweli hii nchi yetu ngumu!

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
mliongea nini jk ule mgomo wa mwanzo..wekeni hadharani kwanza..

tatizo la jk ni kucheka cheka na nyie eti hat bugando wanagoma
 
mliongea nini jk ule mgomo wa mwanzo..wekeni hadharani kwanza..

tatizo la jk ni kucheka cheka na nyie eti hat bugando wanagoma

suala la kwa jk ilikuwa ni baada ya kutaka mawaziri watoke ndipo mazungumzo yaendelee. Kilichokubaliwa pale ni mazungumzo yaendelee aafu mawaziri atawawajibisha ila asiwekewe kitanzi shingoni! Sasa inaonekana amepita mlango wa nyuma na kuhujumu mazungumzo kupitia wawakilishi wa serikali kwani jamaa walikuwa na kiburi isivyo kawaida. Kila dai walikuwa wanapanga majibu wanavyotaka wao badala ya kujadiliana.
 
alidhani maDr ni wasahaulifu kama yeye nini?
 
Back
Top Bottom