Matamko ya BAKWATA na UAMSHO ni dalili ya serikali za CCM legelege

Status
Not open for further replies.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
​​​​Mwalimu nyerere katika kitabu chake cha Uongozi wetu na hatima ya Tanzania aliwahi kuandika, Chama legelege huzaa serikali regelege. Nami nasema, kama hiyo ikitokea hata vikao na maamuzi mbalimbali serikalini yatakuwa pia ni legelege.Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia matukio mbalimbali yanayotokea ya watu fulani kujaribu kuigawa jamii katika misingi ya Utaifa, Udini na tofauti za kiitikadi lakini Serikali yetu iko kimya bila hata kukemea wale wanaoendekeza hulka kama hizi. Na ukimya ni kiashilia cha kuwa labda serikali inakubaliana na haya yanayotokea au haijui nini cha kufanya.
Serikali yetu inakuwa kama MAJIVUNO kwenye riwaya ya Shaaban Robert. Shaaban Robert anamuelezea Majivuno kama Waziri mkuu mwenye haiba kubwa na uhodari mwingi lakini anakosa utashi katika utekelezaji wa majukumu katika serikali yake mpaka inafikia katika hali tete.

Serikali yetu kwa kiyafumbia macho matatizo madogo madogo ambayo Mwalimu Nyerere aliyaita nyufa ndiyo imepelekea kufikia hapa tulipo ambapo inakuwa ni vigumu sana kukabiliana na hili tetemeko la ubaguzi wa kitaifa, kidini na tofauti za kiitikadi.

Itakuwa vizuri tukijikumbusha nini Mwalimu Nyerere alisema katika maswala haya ya Ubaguzi kwa misingi ya taifa, Kidini na kiitikadi za kisiasa na athali zake katika jamii.

Unaweza pia ukakataa kukubaliana na mawazo ya "Baba wa Taifa".

Last edited by a moderator:
Baba wa taifa ni kiongozi mkubwa aliefanya makosa makubwa,moja wapo ni kila alichosema yeye ni sahihi.mawazo mgando hufikirii tena kwasababu ameshasema.
 
Baba wa taifa ni kiongozi mkubwa aliefanya makosa makubwa,moja wapo ni kila alichosema yeye ni sahihi.mawazo mgando hufikirii tena kwasababu ameshasema.

Kwetu sisi waisilamu hatuna baba mwengine isipokuwa yule tu alie kuzaa ndio anastaili kuitwa baba wengine sema Mzee fulani yatosha kaka
 
Nyerere kwa miaka 24 kaifikisha hii nchi kuwa ya mwisho kwa umasikini duniani, bado tu mnamuona wa maana?
 
Baba wa taifa ni kiongozi mkubwa aliefanya makosa makubwa,moja wapo ni kila alichosema yeye ni sahihi.mawazo mgando hufikirii tena kwasababu ameshasema.

Walau alisema, kama ni right or wrong hayo ni mengine, lakini alisema na hivyo unajuwa yuko upande upi. Hawa sasa ni bubu, au ni upepo?
 
Baba wa taifa ni kiongozi mkubwa aliefanya makosa makubwa,moja wapo ni kila alichosema yeye ni sahihi.mawazo mgando hufikirii tena kwasababu ameshasema.
whatever is true and convicing:spy: from him is quoted for the best interests of our nation
 
Baba wa taifa ni kiongozi mkubwa aliefanya makosa makubwa,moja wapo ni kila alichosema yeye ni sahihi.mawazo mgando hufikirii tena kwasababu ameshasema.

Nashindwa kuelewa kama umechangia bila kuuelewa vizuri ujumbe wangu au hutaki kutambua alichokisema Mwalimu Nyerere
 
Nyerere kwa miaka 24 kaifikisha hii nchi kuwa ya mwisho kwa umasikini duniani, bado tu mnamuona wa maana?

Record ya utendaji wa Mwalimu Nyerere haihitaji kukutewa kwa vile mwenye macho na hakima anaiona na kutambua. Kumbuka hakuna binadamu aliyemkamilifu katika dunia hii and the fact is, you can't please everyone, no matter what you do.
 
Nitajie kimoja alichokifanya ambacho tunaweza kusema ni "record" njema mpaka sasa. Ukishindwa kukitaja hapa ujuwe hana, ila unaaminishwa tu iwe hivyo.

"Record" nnayoijuwa mimi ni kuwa kakaa miaka 24 kwenye madaraka lakini hana kimoja cha maana alichoifanyia Tanganyika wala Tanzania.
 
Nyerere alitupa elimu ya bure. Wa Morogoro alipelekwa kusoma Moshi wa Moshi Mtwara na kadhalika. Yote hii kwa kodi zetu. Sishangai uchumi uliyumba lakini kazi ya kuondoa udini na ukabila ilifanikiwa. Acheni udini na ukabila.
 
Nitajie kimoja alichokifanya ambacho tunaweza kusema ni "record" njema mpaka sasa. Ukishindwa kukitaja hapa ujuwe hana, ila unaaminishwa tu iwe hivyo.

"Record" nnayoijuwa mimi ni kuwa kakaa miaka 24 kwenye madaraka lakini hana kimoja cha maana alichoifanyia Tanganyika wala Tanzania.
Alipotaifisha shule za Kanisa ili watu kama wewe mpate kusoma.
 
Kweli kabisa udini uliopandikizwa na ccm ndio matokeo ya haya yote.

Leo hii mtu ana toa tamko la kuwakataza watanzania kushiriki kwenye sensa na ana fumbiwa macho na bado ana linga mtaani.

Serikali nayo ina bidi itoe tamko kwa hili sidhani kama waislam wote wanaunga mkono tamko la BAKWATA.

Serikali legele nichanzo cha matamko yasiyo na maana wala tija kwa wananchi.
 
Alipotaifisha shule za Kanisa ili watu kama wewe mpate kusoma.

Shule za kanisa zilipotaifishwa lilikuwa changa la macho, cheza na Nyerere wewe?

Badala ya kutaifisha shule ambazo zipo makanisani, kwanini asinge jenga mpya? nje ya makanisa.
 
kweli kabisa udini uliopandikizwa na ccm ndio matokeo ya haya yote.

Leo hii mtu ana toa tamko la kuwakataza watanzania kushiriki kwenye sensa na ana fumbiwa macho na bado ana linga mtaani.

Serikali nayo ina bidi itoe tamko kwa hili sidhani kama waislam wote wanaunga mkono tamko la bakwata.

Serikali legele nichanzo cha matamko yasiyo na maana wala tija kwa wananchi.

udini umepandikizwa na nyerere. Kamsome dr. Sivalon (mkatoliki msomi) utaliona hilo.
 
Shule za kanisa zilipotaifishwa lilikuwa changa la macho, cheza na Nyerere wewe?

Badala ya kutaifisha shule ambazo zipo makanisani, kwanini asinge jenga mpya? nje ya makanisa.

Neno zito umelisema zomba
 
Last edited by a moderator:
WAISLAM WANAUMIZANA WENYEWE. Nchi hii haina Ushenzi Wanaoufikiria

USHAHIDI HUU HAPA
Hakika inashangaza;

  1. Chama tawala Tanzania ni CCM na mwenyekiti wake ni Muislaam,
  2. Tanzania tunao Raisi wawili na wote ni Waislaam.
  3. Anayeunda serikali na kuiongoza ni Muislaam
  4. Anayewateua watendaji wakuu pamoja na Waziri Mkuu ni Muislaam.
  5. Tanzania tunao Makamu wa Raisi watatu na wote ni Waislaam.
  6. Jemadari Mkuu wa majeshi Tanzania ni Muislaam.
  7. Mkuu wa polisi Tanzania ni Muislaam.
  8. Mkuu wa Usalama wa Taifa ni Muislaam.
  9. Mkuu wa Mahakama Tanzania ni Muislaam.
  10. Ardhi yote ya Tanzania ni mali ya serikali inayoongozwa na Muislaam.
Katika hali kama hii, mfumo Kristo unawezekanaje? Je, hali ingekuwaje kama mambo yangekuwa tofauti? Kama pamoja na huu ukweli bado mfumo Kristo umeweza kushamiri,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom