Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Status
Not open for further replies.
Na MoU ya EPA,au Malipo kwa Dowans yataenda Msikitini?

Haziendi msikitini wala hazitapokelewa msikitini

MoU ya kanisa na Serikali kuchota hela za umma kuendesha miradi ya kanisa bila shaka ni ufisadi mbaya pia? au siyo
 
Niambie ni halali kuchota pesa na kupeleka kwenye miradi ya kanisa? pesa za umma through MoU? kama huo ni wivu mkuu basi sijakusoma!

Mbona nyinyi mnakataa mahakama ya kadhi kulipiwa na serikali si ndiyo wivu au nini? tumeshtuka wala hutishi mtu..every muslimu will know and decide!

Achana na aliyekataa Mahakama ya Kadhi,just ask yourself NANI ALIYEWAAHIDI MAHAKAMA YA KADHI?Sio Kikwete na Makamba?Je hao ni Wakatoliki?

We certainly know what you will decide: KUONGEZA IDADI YA WIVES,kisha majukumu ya kifamilia yakiwazidi mtakuja tena hapa kuondolea frustraion zenu
 
Haziendi msikitini wala hazitapokelewa msikitini

MoU ya kanisa na Serikali kuchota hela za umma kuendesha miradi ya kanisa bila shaka ni ufisadi mbaya pia? au siyo

Na hospitali zilizojengwa na makanisa kutokana na MoU kama hiyo zilihudumia wakristo pekee?Waislam wenye akili walibaini mapema kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.Wakasoma pasipo kujali nani anayemiliki shule husika,just like mgonjwa asivyojali mmiliki wa hospitali inayomtibu.

Endelea kulalama
 
Ruidi kusoma tamko between the line tumekupa ushahidi, si serikali wala kanisa wanapinga ok..(MoU) million of money za umma zinapelekwa kwenye miradi ya kanis kutoka serikalini ok.

Haya mamilioni yanatumika kujenga makanisa, nyumba za maaskofu au hospitali, shule, vituo vya afya, miradi ya maji, n.k.? Na je, hii miradi inayojengwa na makanisa kwa kutumia hayo mamilioni inahudumia waTanzania wa dini zipi? Watumishi je? How can you be this myopic?
 
Nni kwamba, usipoteze muda wako humu kwenye key board. Hebu tekeleza hili unalosema hapa:

Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.

na hapa:

Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao
 
Ndugu zangu hebu tuzungumze matatizo ya kweli yanayo tukabili,Mnaonekana bado hamjafahamu tatizo linalo tukabiri.Waafrika tatizo Kubwa linalo tukabiri ni UMASIKINI,Kupitia umaskini ndio tunapata matatizo haya yote .Ndugu zangu nawaomba tuangalie jinsi gani tunaweza kumuondoa huyu adui umaskini.Inabidi tuungane ili tuweze kuutokomeza umasikini.Kwenye Umasikini hakuna upendo,hakuna kumcha mungu,hakuna kitu chochote kizuri bali majungu, uadui na mambo mengine mabaya kama haya.

Tukiweza kuuondo umasikini nazani tutakuwa tumemaliza matatizo haya yote.Ndugu zangu njaa mbaya ,njaa inadumaza hata uwezo wa ufanyaji kazi wa akili.Kwa hiyo ndugu zangu hebu tujadiri mambo yanayo weza kuitoa jamii yetu hii kwenye umaskini.
 
Wacha wakejeli tu hili tamko. Nilichofanya ni kuli save kwenye hard disk yangu kisha kuli-email kwa watu wengi niwezavyo, maana najua hii mada haita dumu itafungwa tu. From there tutapita nyumba kwa nyumba tukieleza dhambi hizi wanazofanyiwa waislamu ndani ya nchi yao.

Hili litafanyika contonously kama lilivyoasisiwa na jumuia ya Warsha ya Waandihi wa kiislamu miaka ileeeee ya mwanzoni mwa 80's. Lengo ni vizazi vijavyo vijue dhulma hii na viamue juu ya mustaqbali wa maisha yao katika nchi hii inayodaiwa ni huru.
 
Nimesoma mara mbili hili tamko la ndugu zangu wa damu lakini nimegundua kuwa hili tamko linajipinga lenyewe na limekosa dhana na mantiki au maudhui yenye uhalisia, na tamko lenyewe limejengwa kwa dhana dhaifu zenye kufikirika kinadhadharia (fiction).

Kwa mfano, wanapo ongelea kuwa historia ya kuja wakoloni na kuleta dini ya kikristo Tanganyika wanasahau kuelezea upande wa pili kuwa dini ya uislamu ililetwa na wakoloni wa kiarabu ambao waliwatumikisha mababu zetu na kuwauza kama bidhaa na kuwachapa mijeredi na viboko bila kuwapaa maarifa yoyote, hivyo dini zote mbili zililetwa na wakoloni wa kikiristo na wakoloni waki arabu, kabla ya hapo watanganyika na wazanzibari walikuwa wapagani. huo ndo ukweli sio tamko lao linalo onesha kuwa watanganyika walikuwa waislamu kabla ya upagani,

hivyo basi wakoloni wa kikristo walikuja na strategy tofauti ya kuweza kuwafanya watanganyika waweze kuwatumikia kwa uadilifu na kwa maarifa ndo maana walianzisha mission school ili kuweza kuwavutia watanganyika kwenye dini yao, je hilo ni kosa kwa wakoloni wa kikristo kutoa elimu na maarifa kwenye mission school na baadae kuwapatia ajira watu wenye maarifa? ndugu zangu waislamu swali la msingi la kujiuliza wakoloni wa kiarabu kwanini walipotuletea uislamu hawakutuletea na shule kutupa maarifa, bali walihimiza kuwatumiikia kama watumwa na kutuuza kama bidhaa na kudhalilisha utu wa mababu zetu? Lakini pamoja na missioneries kufungua shule kulikuwa na waislamu wengi tu kama akina Kawawa and the rest waliosoa St. mary's school ambayo baada ya kutaifishwa ilitwa Tabora school, au waliosoma Minaki na shule zingine za mission

hali kadhalika nimeshangazwa na ndugu zangu waislamu kukosa fadhila kwa kumtuhumu Mwl Nyerere kuwa aliendelea kuwabagua waislamu, tunasahau kuwa baada ya uhuru shule zote za mission zilitaifishwa na serikari chini ya Mwl Nyerere ili kuwezesha watanganyika wote waweze kupata elimu, na waislamu waliokuwa na mwamko wa elimu walipata fursa kubwa ya kusoma bure, kwenye shule hizo hizo zilizokuwa za mission na hakuna wakristo waliowahi kulalamika. Je swali kama shule hizo zingekuwa chini ya taasisi ya kislamu na zikataifishwa na serikari waislamu wangemezea? sasa huu uzushi wa kuwa Nyerere aliwabagua waislamu unatoka wapi? Kuna uthibitisho gani tunaweza toa kuwa nyerere alikuwa na nia njema ya kutoa elimu kwa watanganyika wote zaidi ya kurejesha shule zote za mission mikononi mwa serikari? na kutoa elimu bure, kwa nini waislamu hawakuchangamkia fursa hiyo.

Hivi leo tunaona taasisi nyingi za kikristo zimeendelea kufungua shule na vyuo vikuu vingi na vyuo vingine ambavyo sio vya mchepuo wa dini wanaruhusiwa mpaka waislamu kusoma, mfamo St. Augustino na Tumaini University, Je huo ubaguzi unaonwa na miwani zenye umande za mashehe wetu tu?

Swala la Mwisho nalopenda kujadili ni tuhuma zilizoinishwa kuhusu Augustino Mrema na serikari kuwasaidia BAKWATA, lakini tukumbuke wakati huo RAISI wetu alikuwa Maalim Ali Hassan Mwinyi, sasa sina uhakika kama mzee mwinyi ambae ndo mkuu wa nchi na tena mwislamu safi ambaye alikuwa part time Immamu, anaweza kuacha uislamu utiwe najinsi na waziri wake, Kama waislamu hawaihitaji bakwata basi lilikuwa kosa la mkuu wa nchi mzee mwinyi ambae alikuwa mwislamu na mashehe wa kislamu waliokubali kuanzisha BAKWATA. Hivyo adui wa uislamu ni waislamu wenyewe, tusitafute mchawi. Swala la msingi waislamu kwa waislamu tumeshindwa kushikamana na kuunda chombo kimoja kinachoweza kutuunganisha na kutatua matatizo yetu kama wakristo walivyo na TTC, TEC etc,

Jamani, mbona Lowasa aliondolewa madarakani na kamati ya Mwakyembe na watanzania wote tukaridhika kuwa alistahili kuwajibishwa au mafisadi Dr Slaa alio wataja Mwembe Yanga ni waislamu pekee? wezi wa EPA ni waislamu pekee? Kwa nini waislamu wanawakingia kifua mafisadi au hizo pesa zinazochotwa na mafisadi ni mradi wa kuinua hali za maisha ya waislamu, au ni mradi wa kuwapa fursa za elimu kwa waislamu? au ni mradi wa kupunguza ukali wa maisha kwa waislamu?

Kwa mwendo huu hawa viongozi wa dini ya kislamu wanakosa moral respensibility kama wanaweza kukubalii kudhalilishwa na kudhalilisha uislamu kwa dhana iliyopotoka na isiyokuwa na mantiki hata chembe, kulaumu vitu kama wabunge 75% ni wakristo sio kweli na ni upotoshaji wa makusudi na hata kama ingekuwa ni kweli, waslamu kwa nini hawajitokezi kugombea ndani ya CCM ili wananchi wawachague, kwani according to CIA WORLD FACTS BOOK waislamu ndo majority hapa Tanzania, sasa waislamu wasipojitokeza kugombea ubunge ni kosa la wakristo, hoja kama hizi ni mwislamu kipofu ndo anaweza kuziunga mkono. Tushikamane jamani tuibane serikari yetu bila ku play udini card.
 
Tulipowashinda wakoloni sio sie tuliemkabidhi Julius nchi? adui wa uslamu ni mwislamu wala msiwasingizie wakristo ukipata fursa soma kitabu cha Mohammed Said kitabu kinaitwa Abdulwahid Sykes.\

Book Details Summary: The title of this book is Maisha Na Nyakati Za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika and it was written by Mohamed Said, Ali Salum Mkangwa. This edition of Maisha Na Nyakati Za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika is in a Paperback format. This books publish date is January 2002. There are 416 pages in the book and it was published by Phoneix Publishers. The 10 digit ISBN is 9966471693 and the 13 digit ISBN is 9789966471697. For the most current lowest price, Click Here.

Ukipata muda soma hii upate kujua waislamu wanacholalamikia.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ayajua-haya-ya-tanganyika-kabla-ya-uhuru.html

Afadhali wewe umesema. Kikulacho ki nguoni mwako. Siamini na wala sitakaa kuja kuamini kuwa adui yangu yuko nje kule anaplan kuniharibia bila mimi kwanza kumruhusu afanye hivyo. By the way, uislamu sio adui wa ukristu. Ukiniambia freemasons, na hawa jamaa wenye secret societies I would agree. Agenda zao secret organizations ni za hatari zaidi kwa ukristu kwasababu kwa ndani wanaweza kabisa kuwa haamini uwepo wa Mungu. Ila wanafanya mambo as if wanayaamini yale wanayoyafanya, ingawa taratibu wanapenyeza agenda zao za kiruhani. Ukristu ni adui wa uislamu toka lini au ni kujihisi tu bila sababu?
 
Wacha wakejeli tu hili tamko. Nilichofanya ni kuli save kwenye hard disk yangu kisha kuli-email kwa watu wengi niwezavyo, maana najua hii mada haita dumu itafungwa tu. From there tutapita nyumba kwa nyumba tukieleza dhambi hizi wanazofanyiwa waislamu ndani ya nchi yao.

Hili litafanyika contonously kama lilivyoasisiwa na jumuia ya Warsha ya Waandihi wa kiislamu miaka ileeeee ya mwanzoni mwa 80's. Lengo ni vizazi vijavyo vijue dhulma hii na viamue juu ya mustaqbali wa maisha yao katika nchi hii inayodaiwa ni huru.

Si vibaya ukifanya hivyo ili mradi muda unao. Ila hautafanikiwa chochote maana mambo mengi hapo sio kweli ni ya kupika na yamejengwa katika hoja za kujinyong'onyeza ili watu wawaonee huruma.
 
Haziendi msikitini wala hazitapokelewa msikitini

MoU ya kanisa na Serikali kuchota hela za umma kuendesha miradi ya kanisa bila shaka ni ufisadi mbaya pia? au siyo
JK si afute tu hiyo MoU tuone nani atazidiwa na shida baada ya kufuta? Hivi tumewahi kwenda huko vijijini kuona hali ya mambo ilivyo au tunasema tu bila kufikiria athari zake? Mmmh, hii hapa sio dini inayopiganiwa. Dini gani inataka kuona watu wanakufa na maradhi ati kwasababu mbele yake kuna hospitali ya kikristu! Na madaktari wa kiislamu kwenye hospitali hizo inakuwaje.
Kweli ni afadhali kukosa mali kuliko kukosa akili, Period!
 
Upupu mtupu. Hiki ni kithibitisho cha uwezo mdogo wa waswahilina. Mawazo yao yapo confined kwenye uislam tu. Poleni sana ndg zangu. Tatizo lenu ni kuipa kisogo elimu dunia ambayo ingewapa uwezo wa ku-argue na kujenga hoja.
 
Soma kwenye hizo bold nyekundu na nikipata nafasi nitakujibu kipengele kimoja baada ya kingine.

Nimesoma mara mbili hili tamko la ndugu zangu wa damu lakini nimegundua kuwa hili tamko linajipinga lenyewe na limekosa dhana na mantiki au maudhui yenye uhalisia, na tamko lenyewe limejengwa kwa dhana dhaifu zenye kufikirika kinadhadharia (fiction).

Kwa mfano, wanapo ongelea kuwa historia ya kuja wakoloni na kuleta dini ya kikristo Tanganyika wanasahau kuelezea upande wa pili kuwa dini ya uislamu ililetwa na wakoloni wa kiarabu ambao waliwatumikisha mababu zetu na kuwauza kama bidhaa na kuwachapa mijeredi na viboko bila kuwapaa maarifa yoyote, hivyo dini zote mbili zililetwa na wakoloni wa kikiristo na wakoloni waki arabu, kabla ya hapo watanganyika na wazanzibari walikuwa wapagani. huo ndo ukweli sio tamko lao linalo onesha kuwa watanganyika walikuwa waislamu kabla ya upagani,

Anaelezeya Sheikh Abdillahi kwenye kanda iitwayo "Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki," kuwa Himaya ya Kenya ilikuwa ni nchi kabla ya Koloni la Kenya kuwa ni nchi kwa miaka isiyopunguwa 1,300, na namna chuki za uzalendo wa Kiafrika zilivyowaathiri Waislam na khasa chuki za kikabila na propaganda ya utumwa na Uarabu.5
Sehemu hizo mbili za Kenya, Koloni la Kenya na Himaya ya Kenya au Mwambao, zikawa ni nchi moja ya Kenya kwa makubaliyano ya mabadilishano ya barua baina ya Waziri Mkuu wa Kenya, Mzee Jomo Kenyata na Waziri Mkuu wa Zanzibar Bwana Mohammed Shamte walizoandikiyana London tarehe 5 Oktoba 1963. Barua zote mbili zilikubaliyana juu ya mambo matano yafuatayo:
1) Uhuru wa kuabudu wa watu wa dini zote katika sehemu hiyo utalindwa kwa mujibu wa dini zao; na khasa wale raia wa Sultani na vizazi vyao, ambao ni wa dini ya Kiislamu, watahakikishiwa uhuru wao wa kuabudu katika nyakati zote na hifadhi za nyumba na sehemu zote za dini yao.
2) Uwezo wa Kadhi Mkuu na Makadhi wengine wote kuhukumu kwa sharia ya Kiislamu utahifadhiwa kufuatana na sharia ya Kiislamu katika kesi zote za ndoa, talaka na mirathi.
3) Katika zile sehemu ambazo wakaazi wake wengi ni Waislamu, watawekwa, kila inapowezekana, Maafisa Utawala (Mabwana Shauri) Waislamu.
4) Watoto wa Kiislamu, kwa kadri inavyowezekana watasomeshwa lugha ya Kiarabu katika kudumisha dini yao ya Kiislamu kwa vile lugha hii ndiyo lugha ya dini yao. Ule msaada wa fedha unaotolewa kuzisaidia skuli za msingi za Kiislamu katika hilo jimbo la Mkoa wa Pwani utaendelea. Hautakatwa.
5) Umilikaji wa ardhi kutokana na mikataba iliyokwisha kusajiliwa utatambulikana na kukubalika wakati wote. Mwenendo huohuo utaendelea na kuhifadhiwa katika kusajili mikataba mipya ya kumiliki ardhi isipokuwa tu pale itakapokuwa ni lazima kuchukua ardhi kwa masilahi na faida ya umma; lakini papo hapo wale wenye ardhi zao watabidi kulipwa fedha
.
hivyo basi wakoloni wa kikristo walikuja na strategy tofauti ya kuweza kuwafanya watanganyika waweze kuwatumikia kwa uadilifu na kwa maarifa ndo maana walianzisha mission school ili kuweza kuwavutia watanganyika kwenye dini yao, je hilo ni kosa kwa wakoloni wa kikristo kutoa elimu na maarifa kwenye mission school na baadae kuwapatia ajira watu wenye maarifa? ndugu zangu waislamu swali la msingi la kujiuliza wakoloni wa kiarabu kwanini walipotuletea uislamu hawakutuletea na shule kutupa maarifa, bali walihimiza kuwatumiikia kama watumwa na kutuuza kama bidhaa na kudhalilisha utu wa mababu zetu? Lakini pamoja na missioneries kufungua shule kulikuwa na waislamu wengi tu kama akina Kawawa and the rest waliosoa St. mary's school ambayo baada ya kutaifishwa ilitwa Tabora school, au waliosoma Minaki na shule zingine za mission.

Mkuu ukumbuke kulikuwa kuna kitu kinaitwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na aim ya hii Walfare ilikuwa kuendeleza waislamu kielimu na ni nyerere akieivunja na kuikatalia kujenga chuo kikuu cha kislaam mwaka 1964 eneo la kibasila Dar es Salaam
Kilele cha mapinduzi ya Tanganyika ni kudhoofishwa nguvu za umma wa Kiislamu pale ilipovunjwa East African Welfare Muslim Society (EAMWS) na zilipozimwa juhudi za kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislam mwaka 1964.2
hali kadhalika nimeshangazwa na ndugu zangu waislamu kukosa fadhila kwa kumtuhumu Mwl Nyerere kuwa aliendelea kuwabagua waislamu, tunasahau kuwa baada ya uhuru shule zote za mission zilitaifishwa na serikari chini ya Mwl Nyerere ili kuwezesha watanganyika wote waweze kupata elimu, na waislamu waliokuwa na mwamko wa elimu walipata fursa kubwa ya kusoma bure, kwenye shule hizo hizo zilizokuwa za mission na hakuna wakristo waliowahi kulalamika. Je swali kama shule hizo zingekuwa chini ya taasisi ya kislamu na zikataifishwa na serikari waislamu wangemezea? sasa huu uzushi wa kuwa Nyerere aliwabagua waislamu unatoka wapi? Kuna uthibitisho gani tunaweza toa kuwa nyerere alikuwa na nia njema ya kutoa elimu kwa watanganyika wote zaidi ya kurejesha shule zote za mission mikononi mwa serikari? na kutoa elimu bure, kwa nini waislamu hawakuchangamkia fursa hiyo.

Sisi Wazanaki tuna sifa mbili kwa majirani zetu…Kwanza, ni wajanja, na sifa ya pili ambayo inaifuata sifa ya kwanza, ni kuwa si waaminifu. Watu husema ‘Rafiki wa Kizanaki atakuuwa' ambayo si kweli. Sijui vipi tumeipata sifa hiyo… -Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
- Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru

Hivi leo tunaona taasisi nyingi za kikristo zimeendelea kufungua shule na vyuo vikuu vingi na vyuo vingine ambavyo sio vya mchepuo wa dini wanaruhusiwa mpaka waislamu kusoma, mfamo St. Augustino na Tumaini University, Je huo ubaguzi unaonwa na miwani zenye umande za mashehe wetu tu?

Hapo chini kuna sehemu umeainisha CIA records zinasema waislam ni wengi sana Tanzania ni kweli hata ukingalia shule za msingi mnapoanza darasa la kwanza waislamu ni wengi sana kuliko wakristo, mkifika form one waislam wanapotea, form five wanabaki wa kuhesabu sasa hao wakuhesabu ndio unataka waonekane huko tumaini university? hivi kweli watoto wa kiislam hawana ufahamu? si ndio hawa hawa wanaohifadhi juzuu 30 za Quraan? Ali Muhsin Albaruwani ni mmoja wa wanafunzi walio soma dini akahifadhi juzuu 30 kisha akaenda shule ya kizungu na kufika mpaka makerere Ali Muhsin al-Barwani - Wikipedia, the free encyclopedia Je huyu anatofauti gani na hawa wa sasa wasiosonga mbele? mnataka waislamu waamini kuwa wao ndio tatizo? anyway unajitahidi kujenga hoja ila kwa mwerevu na mwenye kujua ukweli uongo kwake hujitenga.
Swala la Mwisho nalopenda kujadili ni tuhuma zilizoinishwa kuhusu Augustino Mrema na serikari kuwasaidia BAKWATA, lakini tukumbuke wakati huo RAISI wetu alikuwa Maalim Ali Hassan Mwinyi, sasa sina uhakika kama mzee mwinyi ambae ndo mkuu wa nchi na tena mwislamu safi ambaye alikuwa part time Immamu, anaweza kuacha uislamu utiwe najinsi na waziri wake, Kama waislamu hawaihitaji bakwata basi lilikuwa kosa la mkuu wa nchi mzee mwinyi ambae alikuwa mwislamu na mashehe wa kislamu waliokubali kuanzisha BAKWATA. Hivyo adui wa uislamu ni waislamu wenyewe, tusitafute mchawi. Swala la msingi waislamu kwa waislamu tumeshindwa kushikamana na kuunda chombo kimoja kinachoweza kutuunganisha na kutatua matatizo yetu kama wakristo walivyo na TTC, TEC etc,

Jamani, mbona Lowasa aliondolewa madarakani na kamati ya Mwakyembe na watanzania wote tukaridhika kuwa alistahili kuwajibishwa au mafisadi Dr Slaa alio wataja Mwembe Yanga ni waislamu pekee? wezi wa EPA ni waislamu pekee? Kwa nini waislamu wanawakingia kifua mafisadi au hizo pesa zinazochotwa na mafisadi ni mradi wa kuinua hali za maisha ya waislamu, au ni mradi wa kuwapa fursa za elimu kwa waislamu? au ni mradi wa kupunguza ukali wa maisha kwa waislamu?

Kwa mwendo huu hawa viongozi wa dini ya kislamu wanakosa moral respensibility kama wanaweza kukubalii kudhalilishwa na kudhalilisha uislamu kwa dhana iliyopotoka na isiyokuwa na mantiki hata chembe, kulaumu vitu kama wabunge 75% ni wakristo sio kweli na ni upotoshaji wa makusudi na hata kama ingekuwa ni kweli, waslamu kwa nini hawajitokezi kugombea ndani ya CCM ili wananchi wawachague, kwani according to CIA WORLD FACTS BOOK waislamu ndo majority hapa Tanzania, sasa waislamu wasipojitokeza kugombea ubunge ni kosa la wakristo, hoja kama hizi ni mwislamu kipofu ndo anaweza kuziunga mkono. Tushikamane jamani tuibane serikari yetu bila ku play udini card.

Nadhani nitakuwa nimekujibu kiasi nikipata wasaa nitakuzijibu hoja zako zaidi.
 
DuH! hilo tamko la aina yake! I never thought there are some races horribly treated like that!!! hata hivo nakumbuka Nyerere aliamua kutaifisha shule binafsi na muhanga mkubwa walikuwa wakatoliki wakifuatiwa na wakristu wengine. Sasa nashindwa kuelewa ni jinsi gani waislam wamlaum nyerere ambaye alitakiwa alaumiwe na wakristu pamoja na Wahindi!! kuongelea miaka mia moja ya manyanyaso na mingine hamsini haikingii akilini! Kwam mfano; Zanzibar ilikuwa chini ya usultani kwa miaka takribani mia nne. Usultani ulikuwa ukiongozwa na uislam. Je, Sultani aliacha secondary ngapi Zanzibar? ukiangalia mzani huo utaona utamaduni wa waarabu ambao ndio chimbuko la kuingia uislam Tanzania halikuwa ujenzi wa elimu Dunia bali Elimu ya Dini tena ya kiislam. kwa hivo kizazi cha waislam wa sasa kulaumu historia ya wakristu kujielemisha she uungwana hata kidogo!! Napendekeza waislam Watoe tamko la kuwalaumu waarabu badala ya wakristo!.
BINAFSI HISIA ZANGU NI KWAMBA SISI WENYE DINI ZETU ZA ASILI TUMEDHULUMIWA SANA NA WATU WANAOFUATA DINI ZA KIISLAM NA KIKRISTO!! KATIBA MPYA LAZIMA ISITAMBUE DINI ZOTE ZILIZOINGIZWA NA WAKOLONI AU WAFANYABIASHARA WA NJE YA TANZANIA!
 
amin wana jf, dini kwa huku kwetu africa ina historia yake, kwa elimu yangu ndogo dini zimeletwa kwetu especially ukristo na uislam na yoote walikuwa wakitafuta kututawala na kuchukua mali asili na kila mmoja akitafuta teritoty, sasa after alnost 50 years bado tuna endelea kuwasikiliza, kuwaabudu. china walikuwa hawana kanisa wala mskiti nafikiri mpaka labda 60s or seventies. lakini leo hii mtu anasema yeye ameokoka au ni muislamu safi.ukimuuliza baba yake babu yake alikuwa anaswali mti gani au anaabudi mlima hupi hajui. naaliishi kwa amani na furaha please tusiwe stupid kiasi hiki. hakuna uislamu wala ukristo africa
 
kikaoikulu.jpg

Mojawapo ya kikao cha kamati kuu ya chama cha mapinduzi, ambacho kazi yake ni kuishauri serikali, na jukumu la serikali ni kutekeleza ushauri wa kamati kuu ya chama.

Angalia wajumbe walioketi karibu na mwenyekiti wa chama ni wa dini gani na ni maoni gani wametoa hadi yanayomfanya Mkristo pekee ashike tama kwa mshangao.
 
Nimekupata kaka ila tatizo letu sisi waislam hatuwezi ku walk on our words, hao walioandika huo waraka wakipigwa mpunga na pesa kidogo wanauza maslahi yetu kwa kitu. Wachache sana wenye kuweza kusimama kidete mfano Sheikh Ali Basaleh lakini hana msaada wowote.

Mfano kwenye ilani ya chama chetu tawala ya mwaka 2005 iliyoandaliwana idara ya itikadi na uenezi ya chama na kupitishwa kwenye CC ya chama kulikuwa na kipengele cha mahakama ya kadhi. Tuache unafiki wote waliisifia ile ilani mapadre, makasisi na mashekhe wakamuita JK chaguo la Mungu. Ilipokuja mjadala wa mahaka ya kadhi kilichotokea sote tunakijua.

Silaha ya waislam ilikuwa kwenye sanduku la kura lakini kwa mgawanyo wetu na unafiki wetu yaliyojiri mnayajua sina mengi ya kusema ila ukweli utabaki pale pale. Itatuchukua miongo mingi sana kujipanga kupata solution ya matatizo ya kiislam na uislam.

My Take,

Waislam hawawezi kubadilika na hawatabadilika.

Kwanini usikasirike ukaamua kutoka kwenye huo uislamu, maana inaelekea unakuboa kweli kwa jinsi ulivyokaa hovyo hovyo na watu wake walivyokaa hovyo hovyo.:A S 39:
 
Kwanini usikasirike ukaamua kutoka kwenye huo uislamu, maana inaelekea unakuboa kweli kwa jinsi ulivyokaa hovyo hovyo na watu wake walivyokaa hovyo hovyo.:A S 39:

Kisha niende dini gani? upagani? acha kudharau imani ya mtu kaka hapa tunafahamishana kwa lugha nyepesi kuwa wapo waislam wa kweli ila waliowekwa mfano "bakwatwa" wapo kimaslahi zaidi sijaamanisha kuwa uislam unaniboa hutaniboa na nitakufa nikiwa Muislamu Insha'Allah.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom