Maswali yaliyomfanya Nape azomewe Kakola-Bulyanhulu

Aluyetoa taarifa anawaza kwa kuludi nyuma, kufunga kiongoz siyo suala la uchaguzi wa udiwan na nchii hstufungani kwa wingi wa tuhuma au kwa kufuata siasa za mkumbo.
 
hahahahaha nimeipenda hiyo na hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania wanavyoamka usingizini sasa na ikitokea viongozi wanaulizwa maswali ya namna hiyo na wanachi wa kawaida mara kwa mara lazima wajiulize mara mbilimbili kulikoni haya yote yanatokea wao binafsi bado wanaamini ya kuwa sisi bado tupo enzi zile na wanaweza kufanya lolote juu yetu kitu ambacho leo hii hakikubaliki Hilo swali la pili mimi ningependa liulizwe namna hii Je ni viongozi wangapi kipindi cha jk wamefungwa jela kutokana na wizi wa fedha ya umma kama ilivyokawaida kwa raia wa kawaida ambao hufungwa pindi wapatikanapo na hatia? swala la nnape kusema kuwa kesi zipo mahakamani ni nani anayethibitisha hili kuwa kesi zipo mahakamani lakini pia kesi mahakamani ni jambo moja na kuufungwa pia ni jambo jingine Pia swali jingine ningependa liulizwe hivi nnape kuna kipindi ulikuwa unazunguka nchi nzima ukitangazia umma kuwa lowasa na chenge ni magamba ndani ya ccm lakini hadi leo tunaona wameendelea kula bata halmashauri kuu ya chama cha ccm(NEC) kulikoni hizo mbio zako ziliishia wapi na kitu gani kilichokufanya unyamaze? je upo tayari sasa kuwashilikisha watanzania kama ulivyowashilisha katika kuwatangaza kuwa ni magamba ndani ya chama Mimi binafsi nimefarijika sana kusikia watanzania wenzangu kuuliza maswali ya namna hiyo tukiendelea hivyo hawa viongozi watashika adabu kwani kabla ya kugombea uongozi lazima wajiulize ya kuwa watanzania wa sasa wana ufahamu juu ya mambo yao ya msingi hivyio basi hapa lazima tujipange sawasawan na hata suala la uwajibikaji litakuwa juu
 
Ila hiyo CHADEMA mnayoipigia kelele mtakuja kuijutia sana!!!! Mimi nawajua sana watu wa Kaskazini.... Ni wabaguzi sana na pia wana roho mbaya sana. Uroho wa madaraka ndo usiseme.... Mungu tuepushe na hili balaa la kutawaliwa na CHAMA kutoka nchi za jirani..... Amin.[/QUOTE]

Mkuu, mroho wa madaraka ni yule anayekuwa tayari kutoa mamilioni ili kununua wapiga kura.
 
Mtu aliyeishiwa hoja humalizia hoja zake uvundo kwa kutukana. Hana sera!!!!!

Hivi inatakiwa uwe na degree ngapi ili uweze kuelewa kuwa mtu aliyethibika kuwa mwizi wa mali ya uma anastahili kufungwa? Kama una maslahi yeyote kutokana na wizi wa rasilimali za nchi hii nadhani utafute kisingizio kingine na sio upeo wa watu kuelewa. Sheria za nchi yetu sasa zimekuwa ni kwa ajili ya watu masikini tu. viongozi wetu wote wanaonekana wapo juu ya sheria.
 
tangia lini Nnape akaweza kujibu maswali ama kaanza jana ....si mnakumbuka 2010 alivyoshindwa kujibu hoja mpaka akapigwa chini kwenye kura za maoni,huyu bwana hana uwezo wa kujibu maswali ya papo kwa papo
 
Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala! Usiku mwema.
We kweli DOMOKAYA,kwa kuwa watu wanaupeo mdogo basi wasipigania haki yao yoyote hata ile wanayoijua pamoja na kuwa wameijua?,we kweli MUA-MSHWA,Umeamshwa lini mwenzetu? bora urudi kulala.Maana kuamka kwako unaelekea U-PUMBAVUNI.
 
Ila hiyo CHADEMA mnayoipigia kelele mtakuja kuijutia sana!!!! Mimi nawajua sana watu wa Kaskazini.... Ni wabaguzi sana na pia wana roho mbaya sana. Uroho wa madaraka ndo usiseme.... Mungu tuepushe na hili balaa la kutawaliwa na CHAMA kutoka nchi za jirani..... Amin.

*Mkuu, mroho wa madaraka ni yule anayekuwa tayari kutoa mamilioni ili kununua wapiga kura.[/QUOTE] We kweli KIMEO,wapigania maendeleo tupo kila kanda ya nchi sa hv we kaa kimeo chako CHAMA CHA MABWE-PANDE kinacho hangaika kumsafisha EL,WAPUMBAVU kweli.bosi wenu kiwete anasumbuliwa na RUSHWA za MTANDAO wa EL,Na nyie mmekuja mwaga PUMBA mnadhani kuna mlaji hapa?.
 
Kwa taarifa yenu CHADEMA ama chama chochote cha upinzani siku ukiona kimeshika madaraka basi ujue ni CHAMA CHA MAPINDUZI ndo kimeamua iwe hivyo....... Na si kweli kwamba chama hicho cha upinzani kinasera nzuri kuliko CCM. Uliza chama cha UNIP, KANU utaambiwa......
..........mkuu, hayo ni mawazo ya watu waliozoea kupewa kofia, khanga, ubwabwa, skafu na vitumbua kwaajili ya kuuza utu na haki zao za msingikila baada ya miaka mitano. Tuombe uhai ili tushuhudie yale ambayo Mungu katupangia tuyaone.
 
Mmhhhhh MBONA THREAD ILE YA WINGI WA WATU KWENYE MIKUTANO YA NAPE MMEITOA?IRUDISHENI.......MSEME NA KWAMBA CCM IMESHINDA KWENYE HIZO KATA



Baada ya kumaliza kuhutubia watu wasiozidi 70, Nape alisikika akisema tofauti yangu na Mzee Slaa ambaye hajawahi kuwa hata katibu kata na hawezi kuwaruhusu kuuliza maswali,kwa sababu hawezi kuyatatua,ni kwamba mimi ndio msemaji wa chama tawala na akija mwingne ni feki,mimi ni kama baba naomba niwape nafasi muulize maswali. Watu wakajitokeza.

Swali la kwanza: Mh Nape, CCM ndio chama tawala,na hakuna chama kingne tena chenye serikali, tunafahamu kwamba nchi yetu inaendeshwa na sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria,lakn cha kushangaza sisi wafanyakazi wa mgodini hapa Kakola -Bulyanhulu tumekuwa tukifukuzwa bila taratibu za kisheria kufuatwa,mfano mimi niliwahi kuuliza swali katika kikao chetu tulichofanya hapa mgodini na waziri wa madini alipokuja mgodini, swali lilihusu maslahi yetu na hivyo nilijua nitafukuzwa na mapema kabisa nilimwambia waziri kuwa baada ya swali hli najua sitakuwa na kazi,na yeye mbele ya wamiliki wa mgodi ule na wafanya kazi wenzangu alinìhakikishia kuwa sitafukuzwa,lakini leo ninapoongea hapa tayari nimekwisha fukuzwa,na nimemtumia ujumbe waziri huyo wa CCM lakn hadi leo hajanitetea,je mhe Nape huoni kuwa serikali ya CCM imewekwa mfukoni na kampuni hii ya Barrick?

MAJIBU YA NAPE: Nataka nikuoneshe kuwa nafahamu tatzo hilo, kuna watu sita mmefukuzwa na nimewagiza wabunge wenu akiwemo Maige ambaye yuko hapa wawape ushrikiano ktk kudai haki zenu. Watu wakaguna.!

SWALI LA PILI, Mh Nape kumekuwa na tabia ya watu wakawaida kufungwa kila wanapokamatwa wameiba, lakn jambo hli limekuwa halitokei kwa mawaziri wanapokamatwa kwa wizi,na matokeo yake wamekuwa wakijiuzulu na kuendelea kukaa majukwaani kama ambavyo leo uko na Maige hapo jukwaani, je huoni kuwa huu ni uonevu zidi ya wanyonge?

JIBU LA NAPE. Serikali ya kikwete tangu iingie madarakani imepangua baraza mara 3,hii ni kithibitisho kuwa hatuvumilii ufisadi, na ukweli ni kwamba kuna mawaziri wameshtakiwa, wananchi wakasikika wakisema tunataka wafungwe si kushtakiwa tu.

Halafu wakazomea, wakati m/kiti wa mkoa ccm shinyanga bwana Mgeja alipofunga mkutano ule watu wale wasiozidi 70 wakaanza kuimba peoples power.,peoples power,na kuonesha vidole viwili! Na Nape akapanda Gx lake akitanguliwa na Maige akifuatiwa na Mgeja wote wakiwa ktk magari tofauti wakati wa kuondoka.

Source mimi mwenyewe nilikuwepo.. Sema sikuwa na Camera. Nape anajua nimeandka ukweli mtupu,naweza kuapa kwa jina lolote kuwa hvyo ndvyo ilivyokuwa
 
kua waziri raha unaiba weeee ukikamatwa unafukuzwa kazi unapewa na mafao yako huyooo unaenda zako kupumzika...ndo mana kila mtu anataka uwaziri
si hivyo mkuu bali mtu akiona anatingwa na kazi ngumu na hana majibu aanaamua kuiba pesa nyingi ili zifidie yote ambayo ataikosa atakaposimamishwa uwaziri
 
Back
Top Bottom