Maswali yaliyomfanya Nape azomewe Kakola-Bulyanhulu

Hizo zitakuwa ni fujo.............Mimi siungi mkono maandamano, kuchoma makanisa, kubomoa misikiti na kufanya fujo. Na ninapokataa kuunga mkono vyama vya upinzani si kwamba sivipendi la hasha... Navijua kwa undani sana. Ipo siku nitatoa ushahidi ni kwa nini siikubali chadema ama nccr au cuf ama TLP au UDP. Nina siri nzito!
............ebu tupishe huko!!! siri nzito utakuwa nayo wewe? Unajifanya unavijua vyama vya upinzani kuliko hao wakuu wako walioshika dola, sidhani kama kuna mtu anayeweza kusubiria hiyo siku asikilize hizo pumba zako kuhusu vyama vya upinzani...........ikiwa hao viongozi wenu akina Nape wanaongea uozo kama huo, sioni cha maana unachoweza kuzungumza juu ya vyama vya upinzani.
 
Baada ya kumaliza kuhutubia watu wasiozidi 70, Nape alisikika akisema tofauti yangu na Mzee Slaa ambaye hajawahi kuwa hata katibu kata na hawezi kuwaruhusu kuuliza maswali,kwa sababu hawezi kuyatatua,ni kwamba mimi ndio msemaji wa chama tawala na akija mwingne ni feki,mimi ni kama baba naomba niwape nafasi muulize maswali. Watu wakajitokeza.

Swali la kwanza: Mh Nape, CCM ndio chama tawala,na hakuna chama kingne tena chenye serikali, tunafahamu kwamba nchi yetu inaendeshwa na sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria,lakn cha kushangaza sisi wafanyakazi wa mgodini hapa Kakola -Bulyanhulu tumekuwa tukifukuzwa bila taratibu za kisheria kufuatwa,mfano mimi niliwahi kuuliza swali katika kikao chetu tulichofanya hapa mgodini na waziri wa madini alipokuja mgodini, swali lilihusu maslahi yetu na hivyo nilijua nitafukuzwa na mapema kabisa nilimwambia waziri kuwa baada ya swali hli najua sitakuwa na kazi,na yeye mbele ya wamiliki wa mgodi ule na wafanya kazi wenzangu alinìhakikishia kuwa sitafukuzwa,lakini leo ninapoongea hapa tayari nimekwisha fukuzwa,na nimemtumia ujumbe waziri huyo wa CCM lakn hadi leo hajanitetea,je mhe Nape huoni kuwa serikali ya CCM imewekwa mfukoni na kampuni hii ya Barrick?

MAJIBU YA NAPE: Nataka nikuoneshe kuwa nafahamu tatzo hilo, kuna watu sita mmefukuzwa na nimewagiza wabunge wenu akiwemo Maige ambaye yuko hapa wawape ushrikiano ktk kudai haki zenu. Watu wakaguna.!

SWALI LA PILI, Mh Nape kumekuwa na tabia ya watu wakawaida kufungwa kila wanapokamatwa wameiba, lakn jambo hli limekuwa halitokei kwa mawaziri wanapokamatwa kwa wizi,na matokeo yake wamekuwa wakijiuzulu na kuendelea kukaa majukwaani kama ambavyo leo uko na Maige hapo jukwaani, je huoni kuwa huu ni uonevu zidi ya wanyonge?

JIBU LA NAPE. Serikali ya kikwete tangu iingie madarakani imepangua baraza mara 3,hii ni kithibitisho kuwa hatuvumilii ufisadi, na ukweli ni kwamba kuna mawaziri wameshtakiwa, wananchi wakasikika wakisema tunataka wafungwe si kushtakiwa tu.

Halafu wakazomea, wakati m/kiti wa mkoa ccm shinyanga bwana Mgeja alipofunga mkutano ule watu wale wasiozidi 70 wakaanza kuimba peoples power.,peoples power,na kuonesha vidole viwili! Na Nape akapanda Gx lake akitanguliwa na Maige akifuatiwa na Mgeja wote wakiwa ktk magari tofauti wakati wa kuondoka.

Source mimi mwenyewe nilikuwepo.. Sema sikuwa na Camera. Nape anajua nimeandka ukweli mtupu,naweza kuapa kwa jina lolote kuwa hvyo ndvyo ilivyokuwa

Tatizo la nape hana akili.anapenda kujiweka na watu wenye ufahamu na uelewa mkubwa kama Mh.slaa.
 
hivi Kikwete hakuwahi kuanzisha kipindi cha kuulizwa maswali tukapewa na email ilituwe tunatuma..
 
Nape Nnauye ni katibu mwenyezi wa CCM, Dr Slaa ni Katibu wa CHADEMA kama Mukama alivyo kwa CCM. Sieweli ni kwa misingi ipi Nape anaona yeye na Dr Slaa wako level moja. Pia, lugha aliyotumia Nape wakati anamtaja Dr Slaa inaonekana kuna tatizo kubwa sana la kimaadili ndani ya CCM. Nape anaongea kama kibaka! Kuna tatizo gani huko Lumumba?

Pili, Katibu mwenezi wa chama cha siasa anapata wapi mamlaka ya kuagiza watendaji wa serikali na wabunge? Hii tabia inaonekana kuota mizizi lakini inadhalilisha.
hayo yanawezekana ndani ya ccm na sirikali yake
 
Tatizo la Nape ni kufikiri anajua sana kuliko wengine hata wazee waliopo Ccm. mtu mwenye uelewa ni yule anayengalia zaidi shutuma na lawama anazopewa ili aweze kujirekegisha kuliko kutazama dheo na baadhi ya sifa apewazo. anapaswa kujua kuwa hata kupitia wapinzani anaweza pata maarifa na uelewa zaidi

Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni,ukitaka kujua hawajiwezi katika kujibu hoja lazima hoja zao zianzie na Dr. Slaa na kuishia na Dr. Slaa.Lakini wanashindwa kujua kuwa wao ndiyo ngazi kubwa ya umaarufu wa mzee yule makini asiye kurupuka.
 
Baada ya kumaliza kuhutubia watu wasiozidi 70, Nape alisikika akisema tofauti yangu na Mzee Slaa ambaye hajawahi kuwa hata katibu kata na hawezi kuwaruhusu kuuliza maswali,kwa sababu hawezi kuyatatua,ni kwamba mimi ndio msemaji wa chama tawala na akija mwingne ni feki,mimi ni kama baba naomba niwape nafasi muulize maswali. Watu wakajitokeza.

Swali la kwanza: Mh Nape, CCM ndio chama tawala,na hakuna chama kingne tena chenye serikali, tunafahamu kwamba nchi yetu inaendeshwa na sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria,lakn cha kushangaza sisi wafanyakazi wa mgodini hapa Kakola -Bulyanhulu tumekuwa tukifukuzwa bila taratibu za kisheria kufuatwa,mfano mimi niliwahi kuuliza swali katika kikao chetu tulichofanya hapa mgodini na waziri wa madini alipokuja mgodini, swali lilihusu maslahi yetu na hivyo nilijua nitafukuzwa na mapema kabisa nilimwambia waziri kuwa baada ya swali hli najua sitakuwa na kazi,na yeye mbele ya wamiliki wa mgodi ule na wafanya kazi wenzangu alinìhakikishia kuwa sitafukuzwa,lakini leo ninapoongea hapa tayari nimekwisha fukuzwa,na nimemtumia ujumbe waziri huyo wa CCM lakn hadi leo hajanitetea,je mhe Nape huoni kuwa serikali ya CCM imewekwa mfukoni na kampuni hii ya Barrick?

MAJIBU YA NAPE: Nataka nikuoneshe kuwa nafahamu tatzo hilo, kuna watu sita mmefukuzwa na nimewagiza wabunge wenu akiwemo Maige ambaye yuko hapa wawape ushrikiano ktk kudai haki zenu. Watu wakaguna.!

SWALI LA PILI, Mh Nape kumekuwa na tabia ya watu wakawaida kufungwa kila wanapokamatwa wameiba, lakn jambo hli limekuwa halitokei kwa mawaziri wanapokamatwa kwa wizi,na matokeo yake wamekuwa wakijiuzulu na kuendelea kukaa majukwaani kama ambavyo leo uko na Maige hapo jukwaani, je huoni kuwa huu ni uonevu zidi ya wanyonge?

JIBU LA NAPE. Serikali ya kikwete tangu iingie madarakani imepangua baraza mara 3,hii ni kithibitisho kuwa hatuvumilii ufisadi, na ukweli ni kwamba kuna mawaziri wameshtakiwa, wananchi wakasikika wakisema tunataka wafungwe si kushtakiwa tu.

Halafu wakazomea, wakati m/kiti wa mkoa ccm shinyanga bwana Mgeja alipofunga mkutano ule watu wale wasiozidi 70 wakaanza kuimba peoples power.,peoples power,na kuonesha vidole viwili! Na Nape akapanda Gx lake akitanguliwa na Maige akifuatiwa na Mgeja wote wakiwa ktk magari tofauti wakati wa kuondoka.

Source mimi mwenyewe nilikuwepo.. Sema sikuwa na Camera. Nape anajua nimeandka ukweli mtupu,naweza kuapa kwa jina lolote kuwa hvyo ndvyo ilivyokuwa

Swali la kwanza. Kwanini asifukuzwe wakati yeye ni mzandiki. Jee, umemuuliza kwanini alifukuzwa?

Swali la Pili. Waziri afukuzwe tu kama raia wa kawaida? faida gani ya kuwa waziri?

Swali la tatu.? mbona hujaliandika?
 
Nape hana mashiko, hajui hata mipaka ya majukumu yake. Yeye ni msemaji tu wa chama, mtu wa propagamba, mtetea chama, yeye husema yale yaliyokwishafanyiwa uamuzi. Hawezi kutoa suruhisho la serikali maana yeye ni wa CCM. yeye hana dhamana yeyote kwa wananchi kama walivyo wabunge. kwahiyo hapaswi kabisa eti kumwagiza mbunge. kwa mamlaka gani?, labda akiwa ndani ya vikao vya CCM, sio kwa wananchi. kwanza mimi ningekuwa mkazi wa eneo hilo ningentaka akae chini maana hastahili kusema na mimi mwananchi kwa kuwa hana mamlaka ya kiserikali.Mamlaka yake yanaishia ngazi ya chama.
 
yaani kwa kifupi ccm ina kazi 2015 maana wananchi wanaelewa nini pumba na mchele ni upi hawandanganyiki tena
 
ninawachukia sana watu wanaokuja humu na kutuambia tutashuhudia mengi ifikapo mwaka huo, yaani wanachofanya ni kutukatisha tamaa wenzao, hivi kama wewe ni mtu hai, mtanzania halisi, unasota kama sisi, unaweza kweli kuwa kwenye msafara wetu kama shuhuda? toka humu ndani upesi hatutaki kujazana na watu waliokata tamaa wanaotaka kutukatisha tamaa na sisi, hopeless kabisa na bado wanajiona wanaishi?
 
jaman tunapoelekea kubaya. kama katibu mwenezi anatoa majibu rahis hivyo na ya kimzaha ipo siku atashushwa na m
awe
 
quote_icon.png
By Malyenge

[/QUOTE]Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala!Usiku mwema.[/QUOTE]

Free Speech, kila mtu yupo huru kutoa shauku yake. Mimi sijatoa oni hapa ila ni mshangao kwa yanayojilia na kuhisi tu kushuhudia mengi hadi 2015. Ningetoa kuali yangu kihoja nadhani maoni yako yangukuwa sahihi, lakini kwa maoni yako uliyoweka umejibu mshangao wangu ambao haukuonyesha kuegemea upande wo wote.

Mkuu, viongozi huchaguliwa kwa sifa zilizokubaliwa na kuwekwa na taasisi husika hususan TZ, na si kwa maeneo, kabila, rangi au jinsi yao.
Katika historia ya TZ, kituko cha kuchagua kiongozi kwa kutumia ubaguzi wa jinsi kimewahi kutokea mara moja tu, na labda kitajirudia tena kwa kuwa kila kitu kinawezekana TZ. Nacho ni kuchaguliwa kwa Mhe. Anne Makinda kuwa Spika wa Bunge kwa kigezo kwamba mara hii tunataka spika mwanamke!!!???
 
Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala! Usiku mwema.

Malyenge (Maryenge) ni mtu mwenye macho yaliyokaa ndivyo sivyo (makengeza).
 
quote_icon.png
By Malyenge
Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala!Usiku mwema.[/QUOTE]

Mkuu, viongozi huchaguliwa kwa sifa zilizokubaliwa na kuwekwa na taasisi husika hususan TZ, na si kwa maeneo, kabila, rangi au jinsi yao.
Katika historia ya TZ, kituko cha kuchagua kiongozi kwa kutumia ubaguzi wa jinsi kimewahi kutokea mara moja tu, na labda kitajirudia tena kwa kuwa kila kitu kinawezekana TZ. Nacho ni kuchaguliwa kwa Mhe. Anne Makinda kuwa Spika wa Bunge kwa kigezo kwamba mara hii tunataka spika mwanamke!!!???[/QUOTE]

Ila hiyo CHADEMA mnayoipigia kelele mtakuja kuijutia sana!!!! Mimi nawajua sana watu wa Kaskazini.... Ni wabaguzi sana na pia wana roho mbaya sana. Uroho wa madaraka ndo usiseme.... Mungu tuepushe na hili balaa la kutawaliwa na CHAMA kutoka nchi za jirani..... Amin.
 
ninawachukia sana watu wanaokuja humu na kutuambia tutashuhudia mengi ifikapo mwaka huo, yaani wanachofanya ni kutukatisha tamaa wenzao, hivi kama wewe ni mtu hai, mtanzania halisi, unasota kama sisi, unaweza kweli kuwa kwenye msafara wetu kama shuhuda? toka humu ndani upesi hatutaki kujazana na watu waliokata tamaa wanaotaka kutukatisha tamaa na sisi, hopeless kabisa na bado wanajiona wanaishi?

Mtu anayesota hawezi kuwa na uwezo wa kuingia kwenye mtandao akarusha mada. Gharama za kutumia kwenye mtandao ni kubwa.... Na gharama za maisha kwa mtanzania ni chini ya dola moja.
 
............ebu tupishe huko!!! siri nzito utakuwa nayo wewe? Unajifanya unavijua vyama vya upinzani kuliko hao wakuu wako walioshika dola, sidhani kama kuna mtu anayeweza kusubiria hiyo siku asikilize hizo pumba zako kuhusu vyama vya upinzani...........ikiwa hao viongozi wenu akina Nape wanaongea uozo kama huo, sioni cha maana unachoweza kuzungumza juu ya vyama vya upinzani.

Kwa taarifa yenu CHADEMA ama chama chochote cha upinzani siku ukiona kimeshika madaraka basi ujue ni CHAMA CHA MAPINDUZI ndo kimeamua iwe hivyo....... Na si kweli kwamba chama hicho cha upinzani kinasera nzuri kuliko CCM. Uliza chama cha UNIP, KANU utaambiwa......
 
Back
Top Bottom