Maswali ya watoto bwana.

The great R

Senior Member
Jun 7, 2011
142
37
Hivi unamjibu vipi mtoto wako au yeyote wa umri wa miaka kuanzia 3 hadi may be 10, anapokuuliza mtoto mchanga anatoka wapi.
 
Watoto wa siku hiz wanajua kila kitu tofauti na zamani. Hujawahi kuona mtoto wa kike wa kazazi hiki akicheza kuwa anajifungua?Kids are funny.

Enzi zetu unaambiwa mtoto kanunuliwa na unaamini lol.
 
Kwa kweli watoto wa umri huo wana maswali sana hasa kuanzia miaka 3-5. Akikuuliza swali kama hilo unamwambia anatoka kwa Mungu na hata wewe umetoka kwa Mungu
 
Muhimu ni kuepuka kumdanganya. Wakati mwingine mtoto anataka kulinganisha jibu lako na lingine alilopata mahali pengine, ukimdanganya baadaye akijua kwamba ulimdanganya atakosa imani nawe. Vile vile hakuna sababu ya kumfafanulia kwa kirefu. Waweza tu kujibu kwamba wanazaliwa, sio lazima ufafanue wanazaliwaje. Akiuliza wanazaliwaje, mwambie akikua ataelewa. Ila kwa mtoto wa umri kuanzia miaka 8, anajua kila kitu, anafaa kuanza kupata elimu ya uzazi. Utafiti umeonesha hivyo.
 
Back
Top Bottom