Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu; awashauri MwanaHalisi wakakate rufaa!

Waziri Mkuu Pinda kamjibu Mbowe Gazeti la Mwanahalisi kama wanaona hawajatendewa haki waende mahakamani.

unamaanisha hizi mahakama ambazo zinatawaliwa na kuendeshwa na serikali...tangu lini ukamshtaki mbuzi kwa fisi...
 
sasa kama mbowe anajua hivyo kwa nini kauliza swali hilo.
kauliza hilo swali kwa sababu aliyelifungia mwanahalisi sio mahakama ni serikali na ndio maana akamuuliza kiongozi wa serikali dhaifu swali sahihi kwa kwa wakati muafaka.halafu pinda anajua kabisa hakuna sehemu yeyote tz hii wanakoweza kulifungua mwanahalisi.kweli magamba wamechoka wanaogopa hata vigazeti shame on them.
 
Waziri Mkuu Pinda kamjibu Mbowe Gazeti la Mwanahalisi kama wanaona hawajatendewa haki waende mahakamani.

Mahakama gani ???????????? za Ghachacha au za Khadhi maana ndio zimebaki hapa Bongo
 
mkuu soma hapa chini:

jaji aloysius mujulizi

jaji aloysius mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishirini walioteuliwa majaji wa mahakama kuu mwezi februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake, jaji mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili ya ishengoma, masha, magai & mujulizi advocates (immma) ya dar es salaam. Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuni iitwayo deep green finance co. Ltd. Mnamo tarehe 18 machi 2004. Immma advocates vile vile walikuwa mawakili wa tangold ltd.

Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishia mabilioni ya fedha zilizoibiwa benki kuu ya tanzania kati ya mwaka 2005 na 2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya agosti 1 na desemba 10, 2005 kampuni ya deep green finance ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (epa) iliyokuwa benki kuu ya tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya tangold ltd. Ililipwa dola za marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya epa. Nyaraka zilizowasilishwa brela na mawakili wa immma advocates na kusainiwa na gavana wa benki kuu wa wakati huo daudi ballali tarehe 20 mei 2005 zinaonyesha kwamba tangold limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka jamhuri ya mauritius. Haya yote yalitokea wakati jaji mujulizi akiwa wakili mwenza wa immma advocates.

‘sifa maalum' zenye shaka

jaji wa rufaa mbarouk salim mbarouk

mbarouk salim mbarouk aliteuliwa kuwa jaji wa rufaa wa mahakama ya rufani ya tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo jaji mbarouk alikuwa jaji wa mahakama kuu ya zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa jaji wa rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya katiba: "majaji ... Wa rufani watateuliwa na rais, kwa kushauriana na jaji mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu ... Zilizoainishwa katika ibara ya 109 ya katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu ya zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano."

kwa mujibu wa ibara ya 94(3) ya katiba ya zanzibar, 1984, "mtu hatoweza kuteuliwa kuwa jaji au kaimu jaji wa mahkama kuu mpaka awe na shahada ya sheria ya chuo kikuu kinachotambuliwa au chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa jaji wa mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika tanzania au sehemu yoyote ya jumuiya ya madola au mahkama ya rufaa kutoka mahkama hizo; au awe mwanasheria wa zanzibar au tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba." jaji mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya katiba ya zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya tanzania kama.

By tundu lisu mb.
ukiwa ccmagamba ukakubali kupiga magoti na kunyenyekea kisha ukakubali kutekeleza kila utakaloambiwa basi kwako cheo nje nje.
 
ilikuwa ni lazima kulifungia lile gazeti kutokana na taarifa ya kijinga linaloandika
 
Waziri Mkuu Pinda kamjibu Mbowe Gazeti la Mwanahalisi kama wanaona hawajatendewa haki waende mahakamani.

Ukitaka gazeti lako lidumu,sifia kilakitu,hata mbunge asemaye ukweli hupigwa pini kwa kuzulia tuhuma kama vile mwizi ,mbakaji,nk
 
Hivi kweli huyu Pinda amesoma SHERIA? Gazeti la mwanaHalisi limefungia kwa sheria ya magazeti halikupelekwa mahakamani. Sasa litakwenda je kukata rufaa mahakamni kama halikupelekwa mahakamani in the first place?

Sio kwamba kila sheria inayopitishwa na bunge ni sheria nzuri, vinginevyo leo ile sheria ya SSRA ya kuzuia mafao ya kujitoa isingerudishwa bungenu kufanyiwa marekebisho. Get real dhaifu Pinda.
Mambo ya sheria bwana mmh..
 
Kumbuka DC na RC ni wajumbe katika kamati za nidhamu za mahakimu wa wilaya na mikoa respectively. Hii kamati ndo inawaadabisha Mahakimu wa Wilaya/Mikoa wakikosea jambo. Kuna haki hapo?

Kwa ujumla Aweda, umekuwa great thinker, sasa una sifa ya kwenda mjengoni kuungana na wenzako.

Naona kila siku unapiga stepu kwenda mbele. Hongera sana. Lakini pia akina mbowe wanapochemsha usiwatetee sana. Naona umekomaa unamsafisha mbowe. Kwani wao hawakosei?
 
kazi bado ipo kwa watanzania aisee,mijitu inavichwa vigumu kweli yani
 
Back
Top Bottom