Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu; awashauri MwanaHalisi wakakate rufaa!

Ni kweli kwa siasa za mabwepande anayehisi kuonewa ndo anatakiwa kwenda mahakamani na hata kwenye mgomo wa madaktari na walimu serikali ilihisi kuonewa na ilikimbilia mahakamani.

Ndo maana Pinda kawambia MwanaHalisi waende mahakamani ikiwa wanaona wameonewa. Tatizo ni kule mahakamani, kesi ya nyani atapewaje ngedere? Na majaji ndo waleee waliopoteza sifa.
 
Kiongozi wa Kambi ya upinzani mh. Freeman Mbowe amembana pinda kuhusu serikali kulifungia gazeti la mwanahalisi. Mbowe alihoji kwa nini serikali imelifungia gazeti kwa kutumia sheria mbaya inayo lalamikiwa.

swali, Mh. waziri mkuu, kwa kuwa sheria iliyotumika kulifungia gazeti la mwanahalisi ni miongoni mwa sheria zinazolalamikiwa na wadau. Je, wewe huamini kwamba kulifungia gazeti la mwanahalisi ni kinyume cha utawala bora, na ni kuendeleza utawala mbovu.

Majibu, mimi naamini ni sawa kulifungia gazeti la mwanahalisi maadam tumetumia sheria iliyotumiwa na wabunge hili.

My take; Mbowe alishasema sheria inayotumika inalalamikiwa (hajesema siyo sheria iliyotungwa na Bunge)Kwa hiyo, hajajibu swali na anapotosha umma.

Wenje
W mkuu, nimemsikia DC pale mwanza akiwa amevalia sare za ccm na akisema mkutanoni kuwa ameletwa Mwanza ili awaunganishe wana ccm wa Mwanza.
Swali, je ni sahihi kwa Mtumishi wa umma kutumikia cha cha siasa?
Pinda, ni sawa kabisa kwa sababu sote tunatekeleza ilani ya ccm na nia yetu ni kuhakikisha ccm inaendelea kutawala. Hata sisi mawaziri na vivyo hivyo. Kwa hiyo DC alikuwa sahihi.

Mkuu mbona unapotosha makusudi Pinda kamjibu Mbowe kama Mwanahalisi wanaona wameonewa waende mahakamani...kama umeamua kuripoti ondoa ushabiki wa kichama.
 
Pinda anasema mwanahalisi waende mahakamani wakati anajua huko mahakamani wapo wale majaji na mahakimu alio wasema TL kwenye utetezi wake.

Sidhan Kama Huko pinda alikoelekeza Kuna haki tena!! Imebaki Historia!! Hawa majaji wa Voda Faster!!
 
Liwalo na Liwe
As usual!..

Fikra sahihi huja kwa lugha sahihi!
Pinder hafikiri kwa lugha sahihi.
 
Swali kama hilo lilipaswa liulizwe na Muhonga au Lucy Owenya and the like sio kwa KUB
Mkuu,
Mosi, tupe vigezo vya kutenganisha suali la KUB na hao wabunge wengine. Binafsi mimi sijui.

Pili, kati ya wanajf wanaosema suali hilo ni high na wewe unayesema ni too low,ni nani yuko sahihi au gret thinker? Na je, Tutumie vigezo gani kutofautisha great thinker?

Hopefully wewe unajambo na Mbowe.

Waziri Mkuu Pinda kamjibu Mbowe Gazeti la Mwanahalisi kama wanaona hawajatendewa haki waende mahakamani.

Mkuu soma hapa chini:

JAJI ALOYSIUS MUJULIZI

Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishirini walioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili ya Ishengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam. Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocates vile vile walikuwa mawakili wa Tangold Ltd.

Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishia mabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na 2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya Tangold Ltd. ililipwa dola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyaraka zilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana wa Benki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwamba Tangold Limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Haya yote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates.

‘SIFA MAALUM’ ZENYE SHAKA

JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK

Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba: “Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.”

Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984, “mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba.” Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama.

by Tundu Lisu Mb.
 
Kiongozi wa Kambi ya upinzani mh. Freeman Mbowe amembana pinda kuhusu serikali kulifungia gazeti la mwanahalisi. Mbowe alihoji kwa nini serikali imelifungia gazeti kwa kutumia sheria mbaya inayo lalamikiwa.

swali, Mh. waziri mkuu, kwa kuwa sheria iliyotumika kulifungia gazeti la mwanahalisi ni miongoni mwa sheria zinazolalamikiwa na wadau. Je, wewe huamini kwamba kulifungia gazeti la mwanahalisi ni kinyume cha utawala bora, na ni kuendeleza utawala mbovu.

Majibu, mimi naamini ni sawa kulifungia gazeti la mwanahalisi maadam tumetumia sheria iliyotumiwa na wabunge hili.

My take; Mbowe alishasema sheria inayotumika inalalamikiwa (hajesema siyo sheria iliyotungwa na Bunge)Kwa hiyo, hajajibu swali na anapotosha umma.

Wenje
W mkuu, nimemsikia DC pale mwanza akiwa amevalia sare za ccm na akisema mkutanoni kuwa ameletwa Mwanza ili awaunganishe wana ccm wa Mwanza.
Swali, je ni sahihi kwa Mtumishi wa umma kutumikia cha cha siasa?
Pinda, ni sawa kabisa kwa sababu sote tunatekeleza ilani ya ccm na nia yetu ni kuhakikisha ccm inaendelea kutawala. Hata sisi mawaziri na vivyo hivyo. Kwa hiyo DC alikuwa sahihi.

Tayari CCM Imekaliwa kichwani na CDM. Kama hayo majibu ni kweli w.Mkuu kasema hivyo bungeni.
 
Majibu ya pinda kwa swali la Wenje limezi kututhibitishia kuwa post za wakuu wa mikoa na wilaya hazina manufaa yeyote kwa umma na Chadema wakichukua madaraka zinatakiwa zifutwe mara moja!!!
kwani zipo na zinaendelea kuundwa kwa ajili ya kukizi matakwa ya urafiki na kukilea chama kama alivyojibu Pinda shame to ccm
 
Kumbuka DC na RC ni wajumbe katika kamati za nidhamu za mahakimu wa wilaya na mikoa respectively. Hii kamati ndo inawaadabisha Mahakimu wa Wilaya/Mikoa wakikosea jambo. Kuna haki hapo??

Swali kama hilo lilipaswa liulizwe na Muhonga au Lucy Owenya and the like sio kwa KUB
What is the power of mwanahalisi, to your judgement. Do you love this nation? Go to the newspaper sellers and ask them for the rate of sales and then refine your input. Your comment fits for magazeti ya udaku na lile la freedom ya mafisadi.
 
Wenje
W mkuu, nimemsikia DC pale mwanza akiwa amevalia sare za ccm na akisema mkutanoni kuwa ameletwa Mwanza ili awaunganishe wana ccm wa Mwanza.
Swali, je ni sahihi kwa Mtumishi wa umma kutumikia cha cha siasa?
Pinda, ni sawa kabisa kwa sababu sote tunatekeleza ilani ya ccm na nia yetu ni kuhakikisha ccm inaendelea kutawala. Hata sisi mawaziri na vivyo hivyo. Kwa hiyo DC alikuwa sahihi.

Kwa hiyo basi, huko Zanzibar akina Seifu na mawaziri wa CUF kwenye serikali ya Zanzibar wanaitumikia CCM katika kutekeleza ilani ya CCM na kuhakikisha CCM inaendelea kutawala huko Zanzibar.
 
wakati serikali inatagaza uamuzi wa kulifungia gazeti la mwanahalisi,ilitoa onyo pia kwa magazeti mengine yanayoandika taarifa za uchochezi na kupandikiza chuki kwa jamii.
 
kwa majibu ya pm kuhusu wakuu wa mikoa kuna unalazima wakuu wa mikoa na wilaya wawe wanachaguliwa rasmi na wananchi.
 
kwa hiyo basi, huko zanzibar akina seifu na mawaziri wa cuf kwenye serikali ya zanzibar wanaitumikia ccm katika kutekeleza ilani ya ccm na kuhakikisha ccm inaendelea kutawala huko zanzibar.
magamba ni kama mkusanyiko wa mbuzi hawajielewi kabisa.
 
Back
Top Bottom