maswali na majibu ya wanawake wanapotongozwa....

Kuna kaka mmoja ktk ofisi moja kulikuwa na wadada wawili,akamuambia mmoja wa wale wadada, nakupenda nataka nikuoe, yule binti akamjibu pale pale mimi sikupendi, yule kaka akaenda kwa mwingine akamuambia the same "nakupenda nataka nikuoe" yule dada akamjibu pale pale nipo tayari. Wakafanya mchakato wa ndoa na sasa ni mume na mke. Ila yule dada aliyekataa kumbe alikuwa anampenda yule kaka, aksikitika sana kuona hamfuati tena kumumbia anampenda, badala yake akaona mwenzake ndo kaolewa akaanza wivu wa hapa na pale na maneno, visa nk. Sasa hapo sijui mnapazungumziaje?
 
Nina appointment na demu nadhani hapa ntapata point za kuanzia,lazima anase tu
 
Code:
Kuna kaka mmoja ktk ofisi moja kulikuwa na wadada wawili,akamuambia mmoja wa wale wadada, nakupenda nataka nikuoe, yule binti akamjibu pale pale mimi sikupendi, yule kaka akaenda kwa mwingine akamuambia the same "nakupenda nataka nikuoe" yule dada akamjibu pale pale nipo tayari. Wakafanya mchakato wa ndoa na sasa ni mume na mke. Ila yule dada aliyekataa kumbe alikuwa anampenda yule kaka, aksikitika sana kuona hamfuati tena kumumbia anampenda, badala yake akaona mwenzake ndo kaolewa akaanza wivu wa hapa na pale na maneno, visa nk. Sasa hapo sijui mnapazungumziaje?
umeona eeh, kawaida yao hao..
 
mm mapenzi yanarun dunia...................

mie naamini kama mwanaume anampenda binti/dada na kumtokea anapoambiwa sipo tayari kuwa na wewe, au maneno mengine ya kukatisha tamaa awezi kukubaliana ni lazima atafanya hili na lile ili mradi awe nae( amkubali),

na kama mwanaume ulikuwa una test zari ndipo hapo unapotolewa nje nawe unasepa kirahisi
 
Akikwambia ana mtu anakua ana maanisha tayari anapenda na kupendwa kwingine!!!

Kuhusu hiyo ya kutohitaji mtu na kama mtu anapanga kupenda au anapenda tu inahitaji maelezo zaidi.Kwanza inawezekana kabisa kumpenda mtu na usiwe nae kwasababu ya mikakati uliyojiwekea...ukielewa hilo utagundua kwamba hapo tatizo sio kupenda au kutokupenda bali ni kile kitendo cha kua na mtu!Pili wewe unapomfuata msichana kumtongoza kwasababu wewe umempenda haina maana kwamba na yeye atakua amekupenda tayari hata kama atakukubalia maana kuna uwezekano hakufahamu kiundani!!Wat wengi wanapenda kiakili
zaidi.....ajue kwanza wewe sio mume wa mtu...una kagari...umesoma...sio mlevi n.k
ndo aachie moyo wake kua huru juu yako!!

Alafu unaposema kwanini mtu asijibu tu sikutaki au sikupendi kwani hayo maswali ya kwanini hunitaki hua yanatokana na nini.???Si mnaambiwaga hapana then mnaaza kutaka sababu....nazo mkishapewa mnataka kujua sababu ya sababu mpaka mtu anaboreka.Anzeni kuchukua HAIWEZEKANI kama haiwezekani na kusonga mbele muone kama kutakua na maneno mengi.Tatizo hapa ni kwamba wale wa no means yes wataachwa sana solemba!

Lakini kuna wengine pia nataka sitaki ni nyingi sana. Wengine wanaogopa kuonekana maharage ya mbeya maji mara moja so nao wanataka waonekane hawakuwa rahisi kupatikana. Ndo maana hutoa majibu yaliyopinda sana.
 
hahahah wanaume kuna kitu hamjui mwanamke anaposema sitaki anamaanisha nataka. Ila yenye msisitizo ni kama hii. NIKO KWENYE UHUSIANO NA MTU MWINGINE SITAKI, OVER AND OUT.

Ukimkuta wa hivi usiirudishie neno atakuumbua. Ila yule wa sitaki nina mwingine, labda mbeleni hakaikisha amekuridhisha nidyo umwache kwenye mataa kwa sababu hana akili.
 
Lakini kuna wengine pia nataka sitaki ni nyingi sana. Wengine wanaogopa kuonekana maharage ya mbeya maji mara moja so nao wanataka waonekane hawakuwa rahisi kupatikana. Ndo maana hutoa majibu yaliyopinda sana.

Hayo mmeanzisha nyie...kama msingekua mnawachukulia wanaotoa majibu yaliyonyooka right away kama sijui warahisi na mambo gani gani kuzungushana kumepungua!!Besides badala ya kumwambia mtu NO wakati jibu ni YES kwanini asiombe muda wa kufikiri???!Nadhani hii ni nzuri zaidi maana haina usumbufu...akishajihakikishia anachotaka anakwambia yanaisha!
 
mimi nadhani kwa namna ya utongozaji wa mtoa mada kupata majibu ya aina hiyo pia wala c ajabu. ila kwa vile kutongoza hakuna straight format sio kila mtongozwa atatoa hayo majibu. nakwaza na generalisation iliyowekwa hapo kwa vile pia sikubalini na generalisation ya utongozaji iliyopo mezani
 
Hayo mmeanzisha nyie...kama msingekua mnawachukulia wanaotoa majibu yaliyonyooka right away kama sijui warahisi na mambo gani gani kuzungushana kumepungua!!Besides badala ya kumwambia mtu NO wakati jibu ni YES kwanini asiombe muda wa kufikiri???!Nadhani hii ni nzuri zaidi maana haina usumbufu...akishajihakikishia anachotaka anakwambia yanaisha!

Issue kubwa ni kutojiamini, wasiwasi na kuogopa risk ya kukisimamia kile unachokiamini kuwa ni ukweli wa mambo.
 
Back
Top Bottom