Maswali na majibu kwa mawaziri bungeni hayana tija

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,045
5,092
Kipindi cha maswali na majibu kwa mawaziri ambacho huanza hakina tija. Aidha hakifai kupewa airtime katika bunge. Sababu ni:
1) Kuna muda mwingi wa kutunga 'uongo'.
2) Maswali ya nyongeza hukwepwa kwani mawaziri hawajui wizara.
3) Wabunge na wananchi wengi hawana interest na muda huo.
4) Maswali hujibiwa na kuchapwa Dar (si na Waziri) halafu husomwa Dodoma (na Waziri).
5) Mbunge anaweza sema eti 'swali langu namba 5 lijibiwe' na Waziri akasoma!
6) Kuna maswali mengi tu ambayo wabunge huwauliza kwa njia ya simu au ofisini bila kuwekwa kumbukumbu.
USHAURI:
i) Kuwepo na kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa mawaziri, zamu kwa zamu! (kama PM-Pinda on Thursdays)
ii) Mawaziri wajibu wakiwa kwenye nafasi zao! Kuokoa muda wa kutembea 'ili tuone suti zao'
iii) Majibu yapelekwa kwa wenyeviti wa mtaa/kijiji chenye interest na swali husika.

iv) Hii itaepusha kila mbunge kujiona anaweza kuwa Waziri!
Nawasilisha kwa mjadala
 
Back
Top Bottom