Maswali muhimu kwa Mizengo Pinda

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Kwa kuwa wewe ni Kiongozi wa Juu katika nchi hii, na kwakuwa wewe si Kiongozi wa Juu kabisa ktk nchi, na kwakuwa wewe kwa kutumia madaraka na mamlaka uliyopewa ulishindwa kuuzuia mgomo wa Madaktari wa awamu ya kwanza na ya pili, hadi Kiongozi wa Juu kabisa alipoingilia kati, na kwakuwa unajua maendeleo ya mazungumzo kati ya Kamati ya Madaktari kwa upande mmoja na Serikali upande wa pili:
1. Mara ya mwisho kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Dr S. Ulimboka ilikuwa lini?

2. Mara ya mwisho kuzungumza na Dr Ulimboka kabla ya kutekwa ilikuwa lini na saa ngapi?

3. Unakumbuka ni siku gani katika mazungumzo na simu na Dr Ulimboka umewahi kutumia neno "chonde chonde"? Ulikuwa unamsihi afanye nini?

4. Unafahamu nembo na muhuri katika document ambayo watesaji waliyokuwa wanamwonyesha Dr Ulimboka asaini ni vya nani?

5. Unafikiri ni kwanini ulisema wewe "si muumini wa Mungu bali ni muumini wa dini"? Ufafanuzi wa kina.

Nitarudi kukuulizamaswali mengine kabla sijaenda kwa Abdiel/Abedi/Ayoub.
 
Response yake itakuwa kati ya haya
  1. Kumwaga chozi
  2. kwa kujitutumia atasema "liwalo na liwe"
 
Response yake itakuwa kati ya haya
  1. Kumwaga chozi
  2. kwa kujitutumia atasema "liwalo na liwe"

Futa machozi, kisha nijibu swali hili;
6. Kabla ya kutamka "Liwalo na liwe" Bungeni, usiku uliopita uliwasiliana na nani ambaye ni daktari wa tiba?
 
sasa wewe ndugu kama kweli unania ya kumuuliza Mtoto wa mkulima hayo maswali na kama kweli unania ya kujibiwa na huyu bwana hayo maswali unategemea atakujibu hapa????? kwanza sio member wa JF. Nalazimika kuamini kwamba unania nyingine na sio kuuliza hayo maswali na kujibiwa hayo maswali pole sana kwa kuwa tumeshaijua nia yako mapema na unachodhamiria kukifanya hasa kimeshashindikana kwahio unapoteza muda wako. Ni vyema utafute shughuli ya kufanya na sio hii.
 
Pinda alikuwa TISS na alifanya kazi hiyo kwa mda mrefu sana akiwa IKULU kabla ya kuingia siasa.

LIWALO NA LIWE ni coded words ambayo ina maana kubwa sana kwa TISS.

Na maana yake tumeifahamu sasa kwa kile alichofanyiwa Dr. Ulimboka.

Coded ya LIWALO NA LIWE imekuwa UNCODED, Sasa hawezi kujificha tena.
 
Kadri siku zinavyosonga,tutaendelea kufahamu mengi juu ya wahusika. Maoni yangu ni kwamba Pinda alihusika kutoa amri akiwatumia baadhi ya watu ktk TISS na Polisi. Lakini mpango wao haramu umekwama na umechafua vyombo vya usalama na serikali. Rais asione aibu kuwakamata wahusika na kuwapeleka Mahakamani. Hizi stori za Mkenya ni za kipumbavu na kipuuzi kama ilivyo utekaji wa Ulimboka.
 
Back
Top Bottom