Maswali mawili yanayokera wanaume!!

Uko wapi? Nipo bar
hapo anakuwa ameshapata na jibu la swali la pili (unafanya nini?)
 
Hayo maswali ni ya kawaida tu but hutegemea na mood ya muulizaji ikiwa kama police wallah inaboa lkn ikiwa kwenye mood nzr ni raha sana kuulizwa maswal km hayo coz unaelewa jinc mwenzio anavyokujali
 
hapa nimejifunza kitu,
kimsingi inategemea anayekuuliza ni nani wako, mpo kwenye terms gani, muda gani, na namna ya uulizaji.
 
inaonekana we ndo unaechukia coz co mwaminifu,wengne hupenda coz hujua nd mapnz y kwl y kumjal mwenz wako,sasa km we unachukiaga ucjumuishe n wanaume wote.
Hakuna mwanaume rijari anayefurahiaga hayo maswali..labda uwe na tabia za kike....
I hate those questions plus kupigiwapigiwa simu na msg kila dk...
 
Mke akikutext unakereka hawara utamtext umekula umekunywa maji n.k

Kwa kawaida mke anajua what to do...kuna time unakuwa umebanwa sana then anakutumia msg unajibu...anatuma nyingine...ukimwambia uko busy ugomvi...
Give me tym to miss u
 
kutokana na kukua kwa teknolojia kuwasiliana siku hizi imekuwa rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Teknolojia pia imeleta vitu vingine ambavyo vimepata ushabiki hapa bongo kama vile ligi kuu ya Uingereza. Kwa kutumia simu wapenzi au wanandoa imekuwa ni rahisi sana kuwasiliana.

Lakini kwa kuwasiliana huko kuna maswali ambayo wanawake huwauliza wenza wao ambayo kwa kweli huwakera wanaume wengi sana. Utakuta mwanamke anapiga simu mwenzie akipokea tu kabla ya kusema anachotaka kusema anaanza kwa swali "uko wapi?" mara nyingi kwa sauti ya kipolisi. Jamaa akijibu alipo linafuata swali la pili "unafanya nini?"

Ki ukweli kabisa haya maswali na jinsi yanavyoulizwa mara nyingi huwakoroga wanaume. Kama wewe ni mwanamke umeshawahi kumuuliza mpenzi wako maswali haya. Na kama wewe ni mwanaume umeshawahi kuulizwa maswali haya na huwa unajisikiaje?

...unaenda wapi.
...kufanya nini?
...na nani?
?.na mimi nije?

Hapo mwanadada anajitafutia mazingira ya kudanganywa tu...
 
tehe.......tehe... binafsi nimependa coment zenu zote nijimlisha na baadhi ya maelekezo ya tajiri yaku napata raha kidogo nauhakika swali hili nimeanza zaidi jana jioni leo na kesho wakati mwingine kutwa mara tatu kinachowezekana ni kwamba kila wakati litaulizwa kwa tune tofauti na vionjo tofauti lakin the same question uko wapi dear,uko wapi,
 
do u love me? Hili linakera sana,mtu nimekutambulisha mpaka kwetu,nimekuambia nakukuonesha countlessy kwamba nakupenda halafu unaniuliza uliza ovyo
 
sidhani kama hilo swali linaboa as long as uko sehem sahihi. ni swali la kawaida kwani kuna ubaya gani mpenzi wako kujua ulipo? mie naona nikmpata asiponiuliza naona kama kuna kanamana
 
Hayo maswali kiukweli ni mazuri pale muulizaji anapokua anauliza kimahaba zaidi...... Sidhani kama kuna ubaya na inaonesha jinc gani anavyokujali
 
msisingizie maendeleo na simu bure.
unajua ukiingia kwenye relationship kuna vitu ambavyo inabisi ukubali kuwa ni sehemu ya maisha ya kuwa wawili nalo hili la kumjulisha mwenzio upo wapi na utakuwa unafanya nini huko unapokwenda ni moja wapo.
wewe kama utampa taharifa mwenzio na kweli ukawa unasema ukweli itafika sehemu mwenzi wako hatakuwa na shaka la kukupigia simu akuulize ulize upo wapi na unafanya nini......ukishaingia kwenye relation basi ni lazima umjulishe mwenzi mipango yako ya nini kumuweka mwenzio roho juu juu?

Wewe ni genius
 
Back
Top Bottom