Maswali manne (4) kuhusu imam maalik bin anas

Ngosasa

Member
Jul 25, 2016
8
6
NONDO NNE ZA MASWALI.


Swali la kwanza:

Ikiwa muanzilishi wa Madh-habu ya Hanafy ambaye ni Imam Abuu Haniifa,na jina lake kamili hasa akiwa anaitwa Annuuman bin Thaabit ( mmoja wa wanafikih katika nchi ya Iraq), alizaliwa mwaka 80 H.katika nchi ya Iran na kufariki mwaka 150 H. Na pia ambaye wengi walikuwa wakimuita Imam Adhwim . Kabla ya mwaka wa 80 H.ambao ndio mwaka aliozaliwa Imam huyu, watu walikuwa wakifuata madh-habu gani ? !! Na je hii yake na hiyo iliopita ni ipi ya kweli ?!

Swali la pili:


Ikiwa muanzilishi wa Madh-habu ya Maaliky ambaye ni Imam Maalik bin Anas aliezaliwa mwaka 93 H. na kufariki mwaka 179 H. ambaye pia ndiye mtunzi wa kitabu ‘ Al-muwatwa,a’ , na Madh-habu yake kusambaa sana katika Magharibi mwa nchi ya Spain. Swali,kabla ya mwaka wa 93 H.ambao ndio mwaka aliozaliwa Imam Maalik, watu walikuwa katika Madh-habu gani ? !! Na je hii yake na hiyo iliopita ni ipi ya kweli ?!

Swali la tatu:


Ikiwa muanzilishi wa Madh-habu ya Shaafy ambaye ni Imam Shaafi mwenye jina lake kamili Muhammad bin Idirisa bin Abbas bin Oth’maan bin Shaafi,aliezaliwa Gaza mwaka 150 H na kufariki mwaka 204 H huko nchini Misri, ambaye pia Imam huyu alikuwa ni mtu mwenye fani ya mashairi sana mbali na elimu ya dini aliokuwanayo.Na miongoni mwa mashairi yake yakiwa kama haya:" Ikiwa kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume {saww} ni uraafidh ( ukafiri),basi naomba vizito viwili ( majini na binaadamu au kitabu na Ahlubayt ) vishuhudie kuwa mimi ni raafidh”. Swali la kujiuliza ni hili: Kabla ya mwaka wa 150 H. ambao ndio mwaka aliozaliwa Imam Shaafi, watu walikuwa katika madh-habu gani ? !! Na je hii yake na hiyo iliopita ni ipi ya kweli ?!

Swali la nne na la mwisho ni hili:


Ikiwa muanzilishi wa Madh-habu ya Hanmbaly ambaye ni Imam Ahmadi bin Hambali akiwa miongoni mwa kunia (sifa) zake alizokuwa mashuhuri kwazo ni Abuu Abdillah,ambaye pia ni Muarabu kutoka Shiiban huko nchini Iraq,sehemu ambayo iko karibu na Iran,na alizaliwa katika mkoa wa Bagh-dad nchini Iraq mwaka 164 H. na hatimae kufariki mwaka 241 H. Na zaidi pia yeye ndie mtunzi wa ‘ Musnad Ahmad bin Hanmbal’,kitabu ambacho ni cha hadithi na kinakadiriwa kuwa na hadithi 4000 takriiban. Ni lazima pia ujiulize swali hili : Kabla ya mwaka wa 164 H. ambao ndio mwaka aliozaliwa Imam Ahmadi bin Hambali, watu walikuwa katika madh-habu gani ? !! Na je hii na hiyo iliopita ni ipi ya kweli ?!

-------/////-------///////---------

Ninatumai maswali yangu umeyafahamu vizuri kabisa.

Sasa ninayasubiria majibu yako insha Allah.




BY: Shk : Khamisi.


na lengo la maswali haya ni kuwarejea masheikh na maimam wa miskiti hasa wale ambao ni wafuasi wa madh-habu haya,ili tuweze kupata rai zao na maoni yao.Na ukilipata jawabu basi,tunaomba ututumie kupitia namba yetu hiyo ilioko mwisho kabisa mwa ukurasa wa pili wa karatasi hii.
____________
Tufikiri Kwa KINA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom