Maswali Makubwa Mawili Kuhusu Maadhimisho Ya Leo 9/12/2015

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Ndugu watanzania wenzangu,

Asubuhi nimefuatilia Vyombo vya habari na kuona shughuli mbalimbali za ufanywaji wa usafi Dar es salaam na mikoani zikiendelea huku viongozi mbalimbali wa nchi waendelea na kuungana na wananchi katika shughuli hizo.

Maswali yangu kuhusiana na sherehe hizi za uzalendo hasa kwa jiji la Dar es Salaam...

1. Kutokana na jiji hili kuwa chafu kila kona kutokana na usimamizi mbovu wa viongozi wa chini mpaka juu, tumeshuhudia mirundikano ya kila aina ya uchafu mitaani lakini leo tumejitokeza kufanya usafi. Je, huo uchafu tunaoufanya utaenda kumwagwa wapi? Nauliza hivi ni baada ya kuona watu wakifanya usafi na kurundika kwenye madampo yasiyo rasmi.

Je, baada ya kufanya usafi leo, serikali imeweka sheria gani kuwa kwa yeyote atakayechafua baada ya usafi kufanyika leo kuchukuliwa hatua zozote.


TUACHENI SIASA NA MAIGIZO WATANZANIA WENZANGU

Watu wanapiga mapicha na kutumia kwenye mitandao eti nao waonekane wamefanya usafi looooh!! UPUMBAVU MTUPU.
 
Kwa kweli challenge ipo kwenye uzoaji wa hizo taka. Wananchi wamejitahidi kufanya usafi lakini je manispaa watazoa hizo taka????
 
Nikajua umekuja na wazo la kujenga na kuendeleza kilichofanyika leo..kumbe umekuja na kaugonjwa kale kale kakulalamika.. :-[
 
Sidhani kama yupo mtz anaefanya usafi wa leo kwa moyo wa dhati..wengi ni unafiki tu.
 
Keshokutwa utazikuta barabarani....kama kawaida. Ingawa wazo ni zuri Hakukuwa na mpango endelevu tunajua kupiga picha tu
 
Yani kama kufanya usafi ni upumbavu kwako basi si shaka utakua na shida kidogo ndugu! haya ni mambo ya kawaida ktk kutilia mkazo wa watu wajifunze kuwajibika,hapa napo eti mnataka kuponda tu,kwa nini Watanzania tumezoea kulalamika lalamika tu?
 
G'taxi Yani kama kufanya usafi ni upumbavu kwako basi si shaka utakua na shida kidogo ndugu! haya ni mambo ya kawaida ktk kutilia mkazo wa watu wajifunze kuwajibika,hapa napo eti mnataka kuponda tu,kwa nini Watanzania tumezoea kulalamika lalamika tu?[/QUOTE]

G'tax ninachojaribu kuelezea hapa ni kuwa hakukuwa na mipango endelevu ya namna ya kendeleza usafi huu...pia makusanyo ya takataka yanatolewaje pale yalipokusanywa...kubwa zaidi ni kuwa kuna sheria yoyote iliyowekwa kwa yule atakayechafua tena.
 
Last edited by a moderator:
Tunataka mipango thabiti ya uzoaji taka,,hichi ni kama kichekesho au kioja,,,hakuna huduma za uzoaji taka kabisa,,nimehamia dar mwaka wa tatu sijaona gari la kuzoa taka mtaani tena mtaa wa wanaojiweza sijui kwingine,,,nawapa hongera wakazi wa dar maana ungekuta kila mahali ni taka ,,,hakuna vibox vya taka nyepesi kuanzia kibaha mpaka posta mmeti ukikutwa unatupa taka fainu,,nchi ya alfa holela holea
 
Katika majiji 3 ya DSM kuna dampo moja la lPugu Kinyamwezi. Hili liko Ilala na limezidiwA , Majiji ya Kinondoni na Temeke hayajafanya jitihada yoyote kupata Dampo. Ukweli ni ardhi haipo.. Masika Mwezi Machi. Apr na Mei ni shida hakuna uchafu unapenya Kinyamwezi nawakuu watataharuki tena. itakuwa aibu kubwa. Majiji yatafute ardhi kule Mkuranga, Kisarawe na Bagamoyo kwa madampo.Sitapenda kuona nchi yangu inakopa Benk ya Dunia / WB kwa ajili ya usafi na kununua ardhi / fidia kwa madampo
 
Back
Top Bottom