Maswali kwa PM Julai 14, 2011

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Kama kawaida ya leo Alhamis ni maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu

Bibi Kiroboto kitini

GR leo ndani ya Mjengo
 
Swali la kwanza kiongozi wa Upinzani Mh. Mbowe

Anaitaka serikali kuunda kamati kutoa maelezo na mbinu mbadala kuhusu Umeme, wananchi wamechoka na kauli zile zile

PM: Suala si Tume, hapa ni dhamira na serikali imejipanga kushughulikia tatizo hili na litakwisha
 
Swali: Milioni 12 kwa mwezi zinalipwa kwa Nyumba ya Mh. Sitta huko Masaki akiwa Spika na hivi majuzi kasafiri kwenda India na Familia yake kwa hadhi ya Spika.

Lini ataondoka katika nyumba ya Spika na kutopewa hadhi ya daraja la kwanza ili kuipunguzia serikali mzingo

Spika anaingilia kati: Huyu ni Spika mstaafu kama alivyo Msekwa na wengine wowote, hili si swali

Kapotozewa

Mh. Regia
 
Anauliza

Kuhusu kuwawajibisha wabunge wasiotimiza majukumu yao vema huku wanapewa fedha na serikali

wabunge wanatokana na vyma fulani fulani CUF, CDM na kadhalika, utaratibu uliowekwa na serikali kutekeleza wajibu wako kwa hiyo serikali inafanya jukumu ka kuwawezesha kutimiza wajibu wao na watawajibishwa na wananchi

Mh. Regia anasisitiza serikali lazima iwamonite kwa kuwa fedha hizo zinakaguliwa na CAG

PM: anasisitiza kila chama kina jukumu kwa wabunge wake na si busara kuingiza serikali katika jukumu jingine na gharama za kuunda chombo kipya kuwasimamia wabunge
 
Mwanamrisho Abdallah
Anaulizia Suala kuhusu kero za Muungano kutotatuliwa na athari zake kama zilivyotabiriwa na Mzee Karume sasa ni kama unaelekea kukwama?

PM: Muungano umetujengea heshima na umetuunganisha kama pande mbili na kutufanya kuishi kwa raha, tuchelee kuubeza na tuendeleze yale mazuri
 
Nyongeza: Huoni kama umefika wakati pande mbili kupiga kura za maoni kuhusu Muungano kwa sasa

PM: Fikra zako kama ndio za wengi ni vema zikaelekezwa katika kuandika katiba mpya. Zanzibar wapo kama milioni moja na Tanzania zaidi ya milioni 40. Ni vema kuendelea kusaka namna ya kumaliza kero zilizopo kuliko kufikiria kutengana.
 
Kuna mbunge mama wa Kizanzibar kamnukuu Marehem Abed Amani karume kuwa MUUNGANO NI KAMA KOTI,UKIVAA UKAONA LIMEKUBANA UNAVUA.Kwa hiyo anamuuliza waziri Mkuu aoni kuwa ni wakati mwafaka matatizo ya muungano yanaipa nafasi kauri ya Mzee Karume kuchukua nafsi yake kuwa MUUNGANO UVUNJWE

Nawasilisha
 
Sitta aondoke kwenye nyumba ya U-spika. Sasa hivi ni waziri wa kawaida and he should like waziri wa kawaida. huu ni wizi wa hela za umma. mnafiki original huyu mzee.
 
Sitta aondoke kwenye nyumba ya U-spika. Sasa hivi ni waziri wa kawaida and he should like waziri wa kawaida. huu ni wizi wa hela za umma. mnafiki original huyu mzee.

Alikuwa anajifuta jasho tu wakati swali linaulizwa hata hivyo bibi kiroboto kambeba. Kuwa ni stahiki yake kwa kuwa bado ana hadhi ya Spika Mstaafu na kuwa haki hizo huwa haziondoshwi kisheria
 
Anamwita Mh. Lema

Na anamtania kidogo kuwa Mh.Lema nimukumiss

Lema nae anamwambia nimekumis

Swali:
Kuhusu utitiri wa waajiriwa kutoak nje kwa nafasi ambazo hata watanzania wanaziweza

PM:
Tatizo la watanzania ni visingizio na uzembe, leo mtoto wa mjomba anaumwa mwingine anaharisha na visingizio kibao hakuna mwajiri atakayevumilia haya

Tubadilike sasa
 
Swali Kuhusu bei ya Mafuta: Soma thread ya GR ya jana Serikali itaoka Likizo Lini?


PM: Serikali ilipotamka bei ya mafuta tulitambua kuwa haitabadilika mara moja kwa kuwa kuna shehena kubwa na huchukua siku kati ya 35 hadi 40 kuimaliza ila tumeishawaagiza EWURA kuchunguza shehena hizi na tujue zinakwisha lini kutokana na hila za wafanyabishara.

Baada ya muda huo na taarifa ya EWURA tutatoa Tamko.

Kamaliza na G.R bado nipo nipo kidogo kufuatilia mjadala wa wali kabla ya kuchomoka
 
Ishu ya mafuta naona sanaa tu! Hajajibu kitu! Anasema bei itashuka baada ya muda mpaka stock iishe wakati huo huo mafuta ya taa yalipanda tu baada ya tamko?
 
Alikuwa anajifuta jasho tu wakati swali linaulizwa hata hivyo bibi kiroboto kambeba. Kuwa ni stahiki yake kwa kuwa bado ana hadhi ya Spika Mstaafu na kuwa haki hizo huwa haziondoshwi kisheria
Ni Tanzania tu. Mtu anakuwa mstaafu na huku ni waziri pia! Anaitumia hadhi anayoona inamfaa kulingana na mazingira na wakati aliomo.
 
Ni Tanzania tu. Mtu anakuwa mstaafu na huku ni waziri pia! Anaitumia hadhi anayoona inamfaa kulingana na mazingira na wakati aliomo.

Yaaani unajua mkuu nimeshangazwa sana na hayo maelezo kuhusu spika Sitta. Hivi kweli TZ tupo serious????????????
 
Back
Top Bottom