Maswali 10 yanayonisumbua; sihitaji majibu!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nilikuwa nawaza tu:(yote ni original)

1. Mwanasiasa akianguka wakati wa uchaguzi ni vizuri kumuinua?

2: Je fisadi ambaye ameamua kuokoka anaitwa Fisadi Mlokole?

3: Kwanini unafikiri inaitwa Meremeta? kwa sababu iko gizani.

4: Unajua ni kwanini ni vigumu kwa serikali kusimamia dhahabu yetu? Ni nzito!

5: Unajua kwanini CCM imelea ufisadi nchini? kwa sababu ina walezi wake!

6: Kwanini Naibu Spika akizungumza bungeni anaitwa naibu Spika? Kwa sababu hazungumzi sana!

7: Wawekezaji wanaochukua faida yote kupelekwa kwao bado ni wawekezaji?

8: Je Tanesco inaweza kukosa umeme?

9: Mtu akiichafua serikali je inaweza kumsafisha?

10:Wafanyabiashara weusi wanaitwa wafanyibiashara wazalendo, mafisadi weusi wanaitwaje?
 
Last edited:
Namba 6 haijakaa sawa, imemlenga mtu binafsi, na haina maslahi kwa mjadala na taifa unless uprove jina la mtu lina uhusiano na viashiria mbalimbali vya nchi
 
Namba 6 haijakaa sawa, imemlenga mtu binafsi, na haina maslahi kwa mjadala na taifa unless uprove jina la mtu lina uhusiano na viashiria mbalimbali vya nchi

ok let me think abt fixing that one.. thanks
 
Umejitahidi kuuuliza maswali machache mno naamini una mengi sana, labda tuanze kufikiri jinsi ambavyo ungeuliza!

11. Kwani mtu akikusaidia kukupigia kampeni ya urais lazima umpe zawadi ya cheo? hata kama hafai?

12. Kwani ni lazima kuukabali uwaziri au vyeo vingine mnavyopewa na rais ili hali ukijua huna vigezo na uwezo?
 
13. kwani nguvu ya kalam pekee inatosha kuleta mageuzi?
14. kwa nini watu wanapigana 'vita' wakiwa exile?
 
MKJJ,
those qns could lead to another report if answered...namimi naongeza tu..
1. kwani ni lazima ukiwa raisi mawaziri wawe washkaji zako??
2. kwani Pinda alikuwa ni chaguo binafsi la JK? unajua chakuo lake??
3. kwanini pesa za EPA zilipelekwa wizara ya kilimo?? unamjua waziri wake ni nani na mahusiano yake na JK..? unazani angefaa kuwa...???
4. kwanini maraisi wetu huwaga mabubu?? hawezi kutoa kauli yoyote public,? hata wafanyakazi wakigoma...mbona wenzetu ambao hata ugomvi wa housegirl ukifika vyombo vya habari raisi atacomment...unakumbuka mlipuko wa mbagala..??
5. kwanini viongozi ni wasaliti na wananchi wanaukubali uozo siku zote???
6. kwanini kama tunahasiri hatuonyeshi hazarani?
7. kwanini watanzania wameanza kuwa wadini, ni dalili gani?? chanzo ni nini??
.....
.....

mi kwangu ni hayo tu...japo yapo mengi..?
8. kwanini waendelee kuongoza japo wana kashfa za ufisadi??? nani anawalinda??
9. kwanini viongozi hawapendi kujiuzuru wanapokuwa na makosa?? je ni system inayowalinda au anayetakiwa kuwawajibisha ni muungwana zaidi?
10. je niini hatima ya Buzwagi? iptl?richmond? kagoda?radar?..........F****@#%^&**)(ck...
11, je hii nchi ni yetu sote au kuna watu wameilisi kutoka kwa wazee wetu, wameachiwa waile peke yao???

f^%*&K the qns keep coming....ngoja niache tu....i wish JK dies b4 2010...
 
Mimi hunisumbua maswala ya imani zao:
1. Viongozi wetu wanatoa wapi ujasiri kungia msikitini au kanisani kusali?
2. Hivi sala zao inawezekana zinafanana kama matendo yao?
3.Kwaninini pamoja na wadhfa na uwezo bado wengine wanaabudu uchawi?
4. Hivi siinaweza kuwa hata kuuwawa Albino ni kwa sababu zao?
5.Wanaficha vipi aibu zao vizuri namna hiyo?
6. Inawezekana kweli kuwa Mwalimu aliwaasa msikubali, piga ua garagaza msikubali kutoka Ukulu ng'o?
7. Itakapotokea wameondolewa wataenda kujificha wapi?
8. Hivi hawaoni hata huzuni kulaza taifa zima gizani?
9. Hizi ishara mbaya zinazowaandama pindi waingiapo Uongozi hawazielewi? Ziwa Victoria, Mabomu mbagala, ajali za ndege zinauwa waziri, ajali tata za magari zinauwa viongozi, helikopta zinakata vichwa vya wasaidizi nk nk?
10. Pamoja na ubabe wote huo na ufisadi hawaoni aibu kuendelea kuomba omba?
 
Back
Top Bottom