Masuala ya ulinzi Tanzania na afrika kwa ujumla

Mzee2000

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
527
221
Nilikuwa nachunguza majeshi ya nchi mbalimbai afrika na nimegundua kwamba afrika nzima, ni nchi moja tu, South afrika ambayo inayoweza kujilinda kwa kiasi fulani na maadui wa nje.

Nimeangalia nchi kama libya ambayo ilitumia mabilioni ya dola kununua silaha lakini jeshi lake liliiharibiwa kirahisi na majeshi ya Nato. Kitu ambacho nimegundua ni kwamba viongozi wa afrika hawana upeo wa mbali.

Viongozi hawa wanatumia mabilioni ya pesa kununua silaha kutoka nje wakati pesa hizo tena asilimia ndogo tu zingetumiwa ku research silaha na kutengeneza silaha zao wenyewe wangepata uwezo mkubwa zaidi wa kujilinda na vievile kuongeza upeo wa sayansi na teknolojia. Kama pale UDSM tukianzisha Aerospace engineering na kozi nyingine za kisayansi hii inaweza kutusaidia sana kutengeneza silaha zetu wenyewe in the long run badala ya kununua kutoka Ukraine.

Je kama Ukraine hawa wakitushambulia silaha tutatoa wapi? Off course wanatuuzia 2 rate silaha ambazo tutazitumia kuuana wenyewe kwa wenyewe lakini sio kutulinda against real threats.

Muda si mrefu ujao Africa itakuwa battle ground. Ona kila nchi sasa inataka kuiinvest Afrika. China wameishiwa na raw materials mafuta,chuma n.k marekani wanataka malighafi yetu kwa hiyo miaka ya mbele Afrika itakuwa battle ground. Kama tusipoanzisha defence system zetu wenyewe, tukitegemea tu kununua silaha kutoka nje tutaweza kujilinda wenyewe? Ukweli, kama libya ,ni kwamba hatutaweza!!

Inabidi tuanze high tech weapons reserch sasa hivi, kama India, china, Brazil na hata south afrika wanavyofanya, tuanzishe course kama aerospace engineering n.k katika vyuo vikuu vyetu tujitegemee wenyewe katika ulinzi wa nchi zetu,sio kila siku tunanunua goboli hizi kutoka China, katika mazingira ya sasa hivi silaha hizi haziwezi kushinda vita, we need to go hightech!!!
 
Akina nani hao watafanya hizo high tech weapons research? UDSM? UDOM? au?.....acha utani wewe!
 
Back
Top Bottom