Mastaa wa bongo: JK amwita Diamond ikulu

Status
Not open for further replies.
Kwakuwa ni huyuhuyu Jk wala asioni ajabu, angekuwa mwingine walau ningestuka kidogo.

Uzoefu wetu watz wamiaka 6 sasa unatupa fursa yakumtambua kiundani huyu ndugu yetu aliyeshindwa wazi kabisa kuliongoza taifa lawatu wasiozidi milioni 60, tena wengi wao ni wakulima na wasomi wa chini kabisa yaani wakata.

Kama alihongwa suti ili watu wabebe twiga na dhahabu anashindwaje chini ya ushawishi wa kimada?
 
Ahaaa haa wewe mwandishi wa article hii kama kweli ni mbunge basi utakuwa ni wabunge la vichaa! Umekosa cha kusema JK na Loveness wapi kwa wapi; hizi dhana zenu wakati mwingine zifungieni kwenye chupi; basi kila kukicha hamkosi utumbo wa kusema?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nini kisichofaa iwapo msanii ataalikwa ikulu?
Marijani Rajabu au Saadan Kandoro akienda Ikulu kula chakula na Rais ina ubaya gani?

Hakuna ubaya Rais kualika raia wa nchi yake pale ikulu. Hapa nasema raia ni kimaanisha hata wanamuziki wa nchi hiyo ni raia.

Na kwa suala lililopo huyo 'Diamond' naye ni raia, hivyo ana haki ya kuonana na rais hapo ikulu.

Tatizo linakuja pale suala linalompeleka ikulu 'Diamond' kutiliwa shaka kwa namna lilivyoendeshwa.
 
Aaah! Tanzania Tanzania, nakuchukia kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania, jina lako ni chungu sana, nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri jana wee, Tanzania Tanzania, nakuchukia kwa moyo wote. Hizo ndiyo priorities za mkuu wa nchi kwa ajili ya nchi na wananchi wake! Huyu jamaaa hajui cha kufanya, sasa ataachaje kuwa promoter? Anasubiria misiba itangazwe atie timu, Zenawi anazikwa lini by the way? Ngulume je yule mama mwenye kinywa kichafu? Tunataka tukamsindikize mwenzetu!
 
Kumbuka Obama kafanya hivi wakati wa kampeni, sote tunajua Obama na Rony wakati wa kampeni wote ni sawa, yaani Obama anakuwa kama ka'freeze' cheo cha URAIS.

Lakini hili la 'mtawala' wa nyumbani ni tofauti kabisa.

Mkuu hawa wapo kwenye kampeni mbona kikwete alivyokuwa akizunguka na bongo flava wakati kampeni tulikuwa hatusemi kitu kwasababu ilikuwa ni wakati muafaka . Hata angesafiri diamond pasingekuwa na tatizo. Tatizo lililopo ni kitendo cha kumuita ikulu Kama promota wale wanao beep na kumpa deal la kwenda kupiga mziki marekani

Kitendo cha Bon Jovi kupanda air force one na President ni deal kubwa kuliko alilopewa Diamond. Ukionekana hadharani unaongea personal issues na President wa Marekani tayari unapata attention ya hali ya juu. Obama and the White House know that ndio maana Obama alivyoumizwa kwenye basket ball katika viwanja vya White House, walisema hawatataja jina la aliyemuumiza ili kumpunguzia usumbufu wa media attetion.

Ona hapa jinsi kuwa karibu na President kunavyoweza kuongeza biashara ya mtu.
Obama Gives

Hata hivyo watu mnaopingana na Rais kwa kila analofanya siwashangai kwa sababu hata katika hicho unachoona ni sawa kwa Obama kumpandisha ndege ya Rais Bon Jovi, wapinzani wake wamemshambulia. Kwahiyo, endeleeni kumshambulia Kikwete, lakini mnatakiwa kufahamu kuwa mnafanya hivyo just because you choose to not because there is a reason to.
 
Ahaaa haa wewe mwandishi wa article hii kama kweli ni mbunge basi utakuwa ni wabunge la vichaa! Umekosa cha kusema JK na Loveness wapi kwa wapi; hizi dhana zenu wakati mwingine zifungieni kwenye chupi; basi kila kukicha hamkosi utumbo wa kusema?

Chama
Gongo la mboto DSM
Kwani diamond hakwenda USA ? Hilo deal hakulipata kwa promota wetu wa ikulu kupitia shinikizo la Loveness?
 
Je, inawezekana wana DMV wanaoipenda nchi yao kumsusia huyu jamaa na show yake?? au kuipiga zengwe??

Maana tumezidi kulalama tu, lakini tunashindwa kuintervene hata basic issues kama hii
 
Kikwete na CCM wanaliaibisha Taifa. Anatumia ikulu vibaya. Iweje Rais atumwe na Mwanamke, ambaye siye mkewe kumuita msanii kwenda Marekani? Mwezi wa sita mwaka huu, Mwanamke mmoja anayeitwa Loveness Mamuya, alikuja pale Bungeni Dodoma. Tukiwa wana CCM kadhaa, alituelezea jinsi Rais Kikwete alivyomteua kuwa mwenyekiti wa CCM-DMV huko Marekani. Vigezo, anajua yeye mwanamke na Kikwete. Mwanamke huyu aliendelea kuelezea ombi lake kwa Rais la kumlepeleka msanii Diamond marekani katika ufunguzi wa Tawi la CCM.

Mnakumbuka wiki jana, magazeti tofauti pamoja na ya UDAKU, yaliandika Rais alivyomwalika msanii huyo(Diamond) Ikulu na kumpa kazi maalum nje ya nchi. Je ni vibaya kuhoji ni kwa nini Rais asifanye kazi za Kitaifa hadi kuingilia mambo mengine ya upromota? Mbona asingemwachia msaidizi wake? Kwani Waziri wa Michezo, Nape Nnauye wasifanye hizo kazi za U-promoter? Kwenda kufungua tawi la watu hamsini, wakati hata Matawi vijijini yenye watu 1000 na zaidi rais hausiki?

Ikulu ni taasisi takatifu katika nchi. Ni taasisi inayostahili heshima zote. Ikulu letu imegeuka kuwa pango la walanguzi, wanyang’anyi, wauaji wa Mabwepande, mapromoter, na wapokea suti. Ikulu imegeuka kuwa sehemu ya kuuzia rasilimali zetu na kugawa vyeo kwa ma hawara. Mbona taasisi ya Rais imeshuka hadhi kiasi hiki?

Hon: Member of Parliament (CCM)

UKICHAGUA garasha usitegemeebkushinda katika mchezo wa karata!
 
Kitendo cha Bon Jovi kupanda air force one na President ni deal kubwa kuliko alilopewa Diamond. Ukionekana hadharani unaongea personal issues na President wa Marekani tayari unapata attention ya hali ya juu. Obama and the White House know that ndio maana Obama alivyoumizwa kwenye basket ball katika viwanja vya White House, walisema hawatataja jina la aliyemuumiza ili kumpunguzia usumbufu wa media attetion.

Ona hapa jinsi kuwa karibu na President kunavyoweza kuongeza biashara ya mtu.
Obama Gives

Hata hivyo watu mnaopingana na Rais kwa kila analofanya siwashangai kwa sababu hata katika hicho unachoona ni sawa kwa Obama kumpandisha ndege ya Rais Bon Jovi, wapinzani wake wamemshambulia. Kwahiyo, endeleeni kumshambulia Kikwete, lakini mnatakiwa kufahamu kuwa mnafanya hivyo just because you choose to not because there is a reason to.
Mkuu mbona unashindwa kutofautisha kitu kidogo Rais alimuita diamond akamwambia nina deal wakakubaliana bei mkuu akapiga mahesabu yake akaona itamlipa wakasaini mkataba. Tofauti Obama kampa bon jov ya safari kwenye Air force one. Halafu USA kuna mgomo wa madaktari au uchumi mbovu? Tusijilinganishe nao
 
Kwani diamond hakwenda USA ? Hilo deal hakulipata kwa promota wetu wa ikulu kupitia shinikizo la Loveness?

Diamond yupo hapa lakini si kweli kaletwa na CCM wala JK muulizeni huyo aliyeandika uzushi na uongo ambao hauna kichwa wala miguu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu mbona unashindwa kutofautisha kitu kidogo Rais alimuita diamond akamwambia nina deal wakakubaliana bei mkuu akapiga mahesabu yake akaona itamlipa wakasaini mkataba. Tofauti Obama kampa bov offer ya safari kwenye Air force one

Hahahahahahahahahahaha hizi hadithi nyingine kama kuna mtu anaamini basi nchi imeoza. Ndio maana ilikuwa rahisi sana kwa babu wa Loliondo kuwaingiza watu chaka. Kuna mtu anaamini kwamba Rais kasaini mkataba na Diomond ili akaimbe Marekani wagawane pesa. Hahahahahahahahahhahahahaa mimi nilidhani tunajadili jambo la msingi kumbe tuko kwenye jokes. Anyway, it was funny enough...
 
nilishawahi kusema na ninana sema tena kikwete hafai kuwa hata afisa michezo wa huko Gamboshi..huyu alitakiwa kuwa sehemu ya waigizaji wa vichekesho wa futuhi yaani awe anaigiza kama raisi ninauhakika watanzania msingekuwa mnakosa kipindi hicho na kuvunja mbavu..tujilaumu sisi wenyewe kawa kushindwa kulinda kura na hili nifundisho kuanzia chaguzi za 2014 tutakuwa makini...
 
This president is a joke.Sikuwahi kumfuatilia kabisa hata alipochaguliwa.Baada ya utumbo mwingi ie ufisadi kuanza kwa kasi.Nikaona humu watu wanavyoponda.Nikasema huyu ngoja nimfwatilie kidogo labda wanamwonea.
Matokeo yake yalinisikitisha sana.Nikajiuliza ilikuwaje akachaguliwa kuwa rais?Nikaja nikapata lil
e jibu la wanamtandao,na alivyomwua muislam mwenzake Salim eti mwarabu wa Hizbu!Hakuingia kwa merits za uchapaji kazi ama atawafanyia nini watanzania zaidi ya slogan ya kitapeli ya "maisha bora kwakila mtanzania"

This president ni janga kubwa la Taifa na madhara ya utawala wake yatabaki for decades if not generations.
Mkuu jmushi1 pole sana. Wengine toka jina lake linapendekezwa mwaka 2005, tuliwatahadharisha Watanzania juu ya hatari ya kufungua milango ya jehanum...mimi kwa mfano nilikosana na ndugu na marafiki kwa msimamo wangu huo. Namshukuru Mungu kwa kuwawezesha wengi kufunguka macho na kumwona huyu msanii katika rangi yake halisi na idadi yao yaongezeka siku hadi siku. Kupitia wizi, kwa mfano EPA, aliingia madarakani na tangu hapo mkono wake upo katika kila tendo la kihalifu nchini linalolindwa na serikali kuanzia wizi wa rasilimali za taifa hadi sasa wizi wa roho za Watanzania wasio na hatia. Of course wapo akina ZeMarcopolo! Watakosaje? Wanafiki, wajinga na walafi ndio mtaji wa CCM, ndio mtaji wa Kikwete na ndio mtaji wa Mafisadi.
 
nilishawahi kusema na ninana sema tena kikwete hafai kuwa hata afisa michezo wa huko Gamboshi..huyu alitakiwa kuwa sehemu ya waigizaji wa vichekesho wa futuhi yaani awe anaigiza kama raisi ninauhakika watanzania msingekuwa mnakosa kipindi hicho na kuvunja mbavu..tujilaumu sisi wenyewe kawa kushindwa kulinda kura na hili nifundisho kuanzia chaguzi za 2014 tutakuwa makini...

You sound like a jealousy loser...
 
Diamond yupo hapa lakini si kweli kaletwa na CCM wala JK muulizeni huyo aliyeandika uzushi na uongo ambao hauna kichwa wala miguu.

Chama
Gongo la mboto DSM
Yalitoka mdomoni mwa diamond tena kwa furaha sana baada ya kupata promota mpya Wa uhakika ambaye habeep
 
Hahahahahahahahahahaha hizi hadithi nyingine kama kuna mtu anaamini basi nchi imeoza. Ndio maana ilikuwa rahisi sana kwa babu wa Loliondo kuwaingiza watu chaka. Kuna mtu anaamini kwamba Rais kasaini mkataba na Diomond ili akaimbe Marekani wagawane pesa. Hahahahahahahahahhahahahaa mimi nilidhani tunajadili jambo la msingi kumbe tuko kwenye jokes. Anyway, it was funny enough...
Afadhali umeelewa Rais wetu alivyo kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Teh! Teh!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom