Mastaa kibao wa vichekesho wagombea fomu za Ze Comedy!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
mastaa kama Jackson Makwaya ‘Bambo’ , Hamis Changale ‘Mtanga’, Rashid Mwishekhe ‘Kingwendu’, Yusuf Hamis ‘Zimwi’ Sunche na Kapeto wakiwa wamepanga foleni ya kuingia kwenye usaili mara baada ya kujaza fomu.

Chipukizi waliokuwa wakiwania nafasi hiyo, hawakufurahishwa na kitendo cha wasanii kwenda kugombania nao nafasi kwakuwa tayari wana majina makubwa hali iliyosababisha waanze kuwazodoa.

“Hawa wamefuata nini hapa, si wameshaonekana kwenye runinga? Mbona wanakuja kutubania nafasi zetu? Hawaoni hata aibu kujipanga foleni na sisi?” Alisikika aking’aka ‘underground’ mmoja huku akiwaangalia wasanii hao ambao walikuwa kama hawasikii.

“Si ndiyo hapo hata mimi nashangaa! Badala ya kutuachia sisi wasanii wachanga tuuze sura kwenye kioo, wao wanakuja kubanana na sisi. Kwa staa kama Bambo hakuna asiye jua uwezo wake, inakuwaje aje kujidhalilisha hapa?”Alidakia chipukizi mwingine.

Lakini baadaye, Mtanga aliamua kuvunja ukimya kwa kusema: “Haya yote ni maisha tu. Tumekuja hapa kusaka nafasi hii adimu ya kujiachia kwenye runinga tunavyotaka. Hawa wasanii wanaojiita underground walie tu, tutakomaa nao humuhumu.”

Hadi Paparazi wetu ‘anang’oa’ eneo hilo, wasanii hao walikuwa bado hawajaingia kwenye usaili kwani kulikuwa na bonge la foleni, hivyo kutojua kama walifanikiwa kupata nafasi au lah!

1266562961bambo.jpg
 
HIvo hivo maisha ni popote na pia ni kuonyesha kuwa kwa sasa wamefulia wakati wenzao ile ni ajira nzuri kabisa. Ni nani anafanay huo usaili si kutakuwa na upendeleo wa kujulikana?
 
wakipata director mbunifu nadhani kipindi chao kitakuwa bomba kuliko kilichopita
 
Kwa kweli hata mimi nina wasiwasi kama huo usahili utakuwa fair na hasa kama kuna wasanii wenye majina ambao nao wameingia... KWa kweli huyo bambo, kingwendu na Mtanga ni watu wanaofahamika ina maana kama anayeendesha usaili alishawaona runingani kuwaacha inakuwa ngumu vinginevyo wawe na vigezo tofauti lakini kama ni kuchekesha tu mh!
 
Kwa kweli hata mimi nina wasiwasi kama huo usahili utakuwa fair na hasa kama kuna wasanii wenye majina ambao nao wameingia... KWa kweli huyo bambo, kingwendu na Mtanga ni watu wanaofahamika ina maana kama anayeendesha usaili alishawaona runingani kuwaacha inakuwa ngumu vinginevyo wawe na vigezo tofauti lakini kama ni kuchekesha tu mh!
Am still in the dark kwani EATV walitangaza hiyo nafasi kwa underground au kwa mtu yeyote alie na uwezo wa kuchekesha? ishu za usaili kuwa fair or unfair zinatokana na qualification walizojiwekea!!
 
Bambo na kingwendu sio wabunifu.

Wameshindwa kwa sababu walikuwa wanadhani fani ya uchekeshaji ni kuongea ujinga ujinga na kuiga sauti za ajabu na kuvaa nguo mbaya.

Chuo Cha sanaa Bagamoyo kinadhauriwa sana, ukitaka kuwa msanii mzuri pitia chuoni , ufundishwe miiko, maadali na nidhamu ya sanaa.
 
MAISHA NI MAPAMBANO, NA FIT OF THE FITTEST NDIO WATAKAO WIN, After all EATV wako kibiashara zaidi kwa hiyo lazima watafute watu ambao angalau hawatakuwa na shida sana ya kuwashape, hata kama wewe ni mwajili CV yenye udhoefu wa kazi inakuwa na nguvu kuliko somebody junior
 
Hakuna haja ya kulaumu mtu waacheni jamaa wauze CV zao. Lakini kuwabeza wakina bambo bado wanamchango mkubwa na kielelezo tosha kwamba usanii bongo haulipi na jamaa wananyonywa manake wana cinema kibao lakini wanaonekana bado wamechoka kimaisha.
 
Njaaaaaaaaaaaaaa inaniuma sana. hawa jamaa nja sana wameshindwa kutengeza hata DVD moja sasa wanajibananisha na madogo. Mbaya sana
 
Back
Top Bottom