Massage Parlours/madanguro

Aaah kwani ukienda pale unabakwa.... si baada ya kukandakandwa ukilegezewa macho na kutambulishwa hiyo bidhaa nyingine ndio unashawishika kununua? Ukiwa mgumu, biashara ya spa ikisha unarudi home na nguvu mpya.
 
Mh, mbona mambo na tunatarajia ukimwi uishe; ndio kwanza unaota mizizi.
Kweli kuishi kwingi kuona mengi.
 
Ninaloliona katika michango hii mbalimbali ni kwamba jamii imekwisha kabisa kimaadili.Karibu kila mtu anaonekana kushabikia uovu huu.Mungu atusaidie sana.Hakuna tofauti kiroho kati ya ukahaba na ufisadi.Kama unashabikia ukahaba wewe ni mnafiki unaposema ufisadi ni mbaya.Nionalo mimi,kama msimamo juu ya ukahaba ndio huo,hatuna 'credibility' kabisa ya kuwachukia mafisadi.
 
Biblia inasema 'Kumcha Mola ni chanzo cha maarifat', na pia M/Mungu anasema 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifat'..

Kama maoni mengi yanaonekana kusupport mambo ya ukahaba, nadhani ni ndoto kwa jamii yetu kujikwamua na umasikini na madhila mengine yanayoizunguka jamii yetu. Kwa maoni yangu sisi watanzania tusipojifunza kumcha M/Mungu tutaendelea kujiangamiza na kuandamwa na madhila ya kujitakia achilia yale ya laana kutoka kwa M/Mungu.
 
Mlalahoi kuna biashara inaitwa ukahaba kila mtu amebariki hilo hata viongozi wa dini serikali wanajua wao ndio wateja wakubwa wa hawa makahaba kila sehemu wapo tumezoea kuwaona wengine wako na ndoa zao ila ndoa zinatunzwa na kazi hii ya ukahaba kwanini tusiuhalalishe basi watalipa kodi na mambo mengine watatambulika watakuwa na saccoss zao na vyama vingine vingi

This is a very strong assertion...

kama kuna watu wengi wenye mtizamo kama huu kweli tumekwisha..fikiria mtu mwenye mawazo kama haya apewe dhamana ya kutunga sera au sheria.... jamii yote itapotoka maana itaburutwa kama gari bovu kushabikia na kufuata itikadi zenye mashaka zisizo na mwelekeo.

Inabidi tuwe macho na tuwakwepe kama ukoma na tusiwape dhamana watu kama hawa..watatupelekea kuchomwa kiberiti kama sodoma na gomora!

Turudi tuangalie sheria zetu za Tanzania... kwanza ukahaba kama " biashara " hautambuliki kisheria... rejea sheria ya makosa ya jinai sura 16 ya sheria za Tanzania.Japokuwa ukahaba kama ukahaba haujaraharamishwa.. ni sawa na "uongo" na dhambi nyingine... maadam binadam ana kasoro ha hulka mbovu nyingi, ni vigumu sheria kumfuata kila mtu mvunguni kumchokonoa anafanya nini gizani au behind closed doors! Hivyo hivyo kahaba anapofanya shughuli zake kibinafsi sheria haimfuatilii... ila pale atakapoji organise na kufanya shughuli kwa mtindo wa " kujirasmisha"..hapo dola itamshukia.....

Tusipotoshane hapa JF kwa kudai ati ukahaba ni biashara inayotambulika/kubalika!!..wewe unayeikubali na kuibariki ni uamuzi na matakwa yako binafsi.

Tafuta facts na ushahidi kwanza kabla ya kutangaza mambo usiokuwa na uhakika nayo!
 
Hiyo biashara imetoka mbali sana. Hapa nilipo kuna rafiki yangu siku moja alinipa "free pass" yake anayotumia kuhudhuria katika parlour moja inaitwa "Ambassador". Utaratibu wao ni kwamba ukiingia unalipa pound 10 mlangoni halafu huko ndani unachagua unayetaka akufanyie massage kisha mnawekeana appointment ya saa ambazo utakuja. Gharama za huduma zitategemea huduma utakayochagua, maana msichana yeyote utakayechagua anayo orodha ndefu tu ya huduma wanazotoa, atakupa brochure ambayo zote hizo zimeandikwa na bei zake, lakini ngono haijaandikwa, haiko kwenye orodha. Ukiwa na free pass unaingia bure, hulipi hizo pound 10 (utalipia tu huduma utakayokubaliana na unayemchagua).

Sasa mimi nikawa curious, nikataka tu niende "niwasanifu" hao wasichana (si nina free pass bana?) halafu niondoke bila kununua huduma yoyote. Nikafika mlangoni nikabonyeza kengele, akaja mhudumu nikamwonesha pass yangu akaniruhusu kuingia. Nikaambiwa nikae kwenye kochi penye reception ambako pia kuna mashine zinauza kahawa, soda, juice na bites. Nikanunua espresso yangu, wakati nakunywa wanapita mmoja mmoja wasichana hao, wako minimally dressed kila mmoja kwa mtindo wake, wanakuja kwangu wanajitambulisha kwa majina na kutokomea. Baada ya kama 10 min, akaja yule aliyenifungulia akaniuliza umemchagua yupi? Nikamwambia kwa kweli sijachagua yeyote. Akaniambia kuna mmoja hujamwona, tulikuwa tume-reserve kwa ajili yako tulijua utakuja, hata kama hutaki huduma atakusadia tu hata kuongea na wewe, inawezekana ni upweke umekusibu ukashindwa kujua unahitaji nini, na hii huduma ya kuongea na mteja kumwondolea upweke ni ofa kwa wateja wetu, hutalipa chochote. Akaja huyo binti, na sielewi ilikuwaje hata nikajikuta nimezungumza naye zaidi ya nusu saa, ana akili kwa kweli anazungumza kila kitu kuanzia rugby hadi politics za number 10 Downing street kwa ufasaha ajabu, ana elements fulani za psychology anaongea pia, alinishangaza kwa kweli. Mwisho akanipa namba yake ya simu tukaagana. Nilishindwa kujizuia kumpigia simu.
 
panaitwa 'Magic Hands',namanga. haya nenda lol!



ACHA UONGO, MIMI nimefika hapo kwa massage karibu mara tatu hata siku moja sikuwa kuambiwa extra. Wewe utakuwa uliomba hiyo extra baada ya kunogewa labda na massage(ulikaribia kupasua nguo yako ya ndani) binti nae kwa shida zake alizonazo akukujibu sawa. Bora uwe kweli kuliko kupaka matope biashara ya mtu kwamba hali niyo.
 
Aaah kwani ukienda pale unabakwa.... si baada ya kukandakandwa ukilegezewa macho na kutambulishwa hiyo bidhaa nyingine ndio unashawishika kununua? Ukiwa mgumu, biashara ya spa ikisha unarudi home na nguvu mpya.

Kweli kabisa, ni vema kuacha generalization ya mambo, wakati the whole issue is on few individuals weakness-wanaofanya na wanaofanyiwa massage
 
ACHA UONGO, MIMI nimefika hapo kwa massage karibu mara tatu hata siku moja sikuwa kuambiwa extra. Wewe utakuwa uliomba hiyo extra baada ya kunogewa labda na massage(ulikaribia kupasua nguo yako ya ndani) binti nae kwa shida zake alizonazo akukujibu sawa. Bora uwe kweli kuliko kupaka matope biashara ya mtu kwamba hali niyo.


boma you are right ..katika parlour zote nilizopita magic wako proffession....sijawahi kupewa hiyo ofa ya extra...wanakufanyia ukimaliza unaaga....hayo mambo ya extra ni lazima mteja ndio utakuwa umeanzisha ....na binti ana hiyari ya kukupa contacts zake au vinginevyo......that is adult consent....

kuna parlour za uswahilini ambazo mabinti hawajui ku massage......hao ndio kila mteja anayefika hujaribu ku m divert kwenye ngono...kwa lugha nyepesi ..kwao ngono ni kazi rahisi kuliko kum massage mteja...tukumbuke masseur ni kazi inayosomewa na ni sanaa watu wana hadi diploma......kwa asiyeijua hatakuwa na namna ya kumfurahisha mteja zaidi ya kumpa ngono....

..kwa kawaida nikienda mahali wanapo innitiate ngono huwa sirudi tena ....hayo ni mazingira hatarishi!!!!
 
Gazeti pendwa la Ijumaa linakuwa la kwanza kufichua siri kwamba wanawake waliokamatwa ndani ya kituo hicho kama wahudumu wa massage na ngono kwa mlango wa nyuma, ni wake za watu.

Funua funua ya wadaku wetu imebainisha kuwa wanawake hao wamekuwa wakijishughulisha na biashara hiyo bila waume zao kujua.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko katika toleo lake la juzi (Jumatano) lilikuwa la kwanza kuandika habari ya kituo hicho chini ya kichwa: “Aibu ya mwaka” ambacho kilisindikizwa na maneno, “Kituo cha vigogo kujivinjari kwa ngono chafumuliwa”.

Katika habari hiyo, ilielezwa kuwa kulikuwa na biashara haramu ya ngono ndani ya Kituo cha Massage, kilichopo Kijitonyama, Dar es Salaam ambapo vigogo wa serikali, watumishi kwenye taasisi zinazolipa mishahara mikubwa na wafanyabiashara ‘wenyenazo’ walifika mara kwa mara kupata huduma.

Liliandika kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi wake, askari polisi wa Kituo cha Oysterbay kwa kushirikiana na waandishi wa habari, walikivamia kituo hicho na kuwafumania wahudumu wawili wakiwa uchi kama walivyozaliwa pamoja na wateja wawili, hivyo kutoa picha kuwa walikuwa kwenye harakati za kutenda ngono.

Baada ya kutoka kwa habari hiyo juzi, Ijumaa lilivujishiwa nyeti kuwa wanawake wawili waliokamatwa kituoni hapo ni wake za watu ambao wamekuwa wakijishughulisha kwa siri na kazi hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, wanawake hao (pichani), mmoja alikutwa uchi, mwingine akiwa amevaa, wote ni wake za watu ambapo wamekuwa wakijishughulisha na kazi hiyo pasipo waume zao kujua.

Katika ‘unyetishaji’ huo, gazeti hili liliwekwa kweupe kwamba mwanamke mwingine aliyenaswa akiwa uchi na mteja chumbani, ni mchumba wa mtu na kwamba alimweleza mpenzi wake kuwa anafanyakazi saluni ya kike.

Ijumaa lilielezwa kuwa mwanamke anayeonekana kulia ukurasa wa kwanza anaitwa Lulu George na kwamba yupo kwenye ndoa na anaishi na mumewe Mbezi Tangibovu, Dar es Salaam kwa mwaka wa pili sasa.

Lilielezwa kuwa mwanamke anayeonekana kushoto ukurasa wa kwanza, yeye alikutwa uchi na kwamba jina lake ni Aisha, anaishi Tandika Mwembe Yanga, asili yake ni Mkoa wa Tanga na ana mchumba wake (jina tunaliminya).
Inaelezwa kuwa Aisha alijieleza kuwa anafanyakazi saluni ya kike wakati Lulu yeye alikuwa akimweleza mumewe kwamba ameajiriwa hotelini kama msimamizi wa wahudumu.

Mwanamke mwingine aliyenaswa kituoni hapo, anaonekana katika picha ndogo iliyozungushiwa duara ukurasa wa kwanza, naye imebainika kwamba ni mke wa mtu, ingawa hakukutwa uchi.

Gazeti hili lilimtuma paparazi Oysterbay Polisi kufuatilia maendeleo ya waliokamatwa katika ambushi hiyo ambapo alielezwa kwamba watuhumiwa wamepelekwa Mahakama ya Jiji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Habari zaidi kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa, waume wa akina dada hao walipopata taarifa za uchafu huo waliangua vilio kama watoto wadogo na kushindwa kufika polisi.

Ijumaa linalaani vikali biashara hiyo haramu na linaahidi kufuatilia sakata hilo katika Mahakama ya Jiji na kutoa maendeleo yake.

Chanzo: Global Publishers

My take: Hivi inawezekanaje ukaishi na mke wako na usifaham anapofanyiakazi, au akawa anakueleza nafanyakazi mahali flani na haujawahi fika?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom