Masonga, sikumkimbia John Heche huko Njombe

Aug 1, 2012
35
27
KUTOKUWEPO KWA NYERERE NA UWEPO WA WADAI HAKI ISIWE NEMBO YA KUHALALISHA UKANDAMIZAJI.

MWALIMU Nyerere katika uhai wake amehusishwa na ukombozi na mpigania uhuru wa nchi, pia alisaidia kujenga taifa taifa lenye mshikamamno na wananchi walioishi kwa kupendana wao kwa wao,watanzania walipendana pamoja na utofauti wao wa vyama, dini, kabila,na rangi.
Baada ya kifo cha Mwalimu baadhi ya wananchi wamepata wasiwasi, wameingiwa hofu, kwamba amani ya nchi itavunjika kwakuwa tu Mwalimu amekufa, kwa madai kuwa yeye ndiye aliyeleta amani, sasa amekufa na nchi itaparaganyika, alkini hawajaaishia hapo wanatumia kauli za viongoi wa kisisa juu ya kukemea uovu wa serikali kuhalalaisha ukandamizaji wa wananchi, mfano kauli ya Dr Slaa alipokuwa akizungumzia ubadhilifu waserikali aliposema nchi haitatawalika pindi serikali isipotenda haki, lakini pia kauli za viongozi kudai haki zinaitwa uchochezi, pale viongozi wa vyama vya siasa wanaposema ukweli eti ni uchochezi kwa wananchi.
Viongozi wakubwa wa nchi nao wamekuwa wakijenga hofu kwa wananchi juu ya upotevu wa amani na kutahadharisha wananchi na vyama vya siasa kuwa ni chanzo cha kuvuruga amani nchini,swali kubwa la kujiuliza je nchi hii haina sheria ya uchochezi na sheria ya kuhatarisha amani ya nchi mpaka kila siku viongozi wahubiri na kuvituhumu vyama vya siasa pasipo kuchukua hatua za kisheria na endelevu kwa manufaa ya nchi? Na zaidi wananishia kumnukuu mwalimu nyerere na kusema alitengeneza nchi yenye amani na kuheshimiana pamoja na tofauti zilizokuwepo.
Lakini hofu hii inatoka wapi hasa, kitu gani alichokuwa nacho Mwalimu Nyerere kimezuia amani isichafuke wakati wa uhai wake na kwanini amani itoweke wakati huu ambao Mwalimu ametoweka, tunaweza kujiuliza au wanakili uwezo wao mdogo wa kuongoza nchi kama sio kuamini nyerere alikuwa mtu tofauti na wao, lakini utapata shida kidogo kutafuta ukweli wa haya, kwanza ni pale viongozi wanapoelekeza tuhuma za kuivuruga nchi kwa wapinzani, ikumbukwe pamoja na kutokuwepo upinzani Nyerere aliona umuhimu wa upinzani ndipo akaamua kuleta mfumo huu Tanzania kwani aliamaini pia changamoto ndio zilizomjenga akiwa rais wan chi kwa kupata mawazo tofauti kutoaka kwa wasomi walioichambua serikali yake.Lakini tutakubaliana kwa pamoja kuna fukuto kubwa la wananchi kutokubali mwenenndo wa uendeshaji nchi unaoendeshwa na chama cha mapinduzi hivyo kukikataa wakati watawala wakiwa na hamu ya kuendelea kutawala.
Kutokana na hali hiyo wanaamua kutumia mbinu ya kuwagawanya watanzania kwa misingi ya kidini,itikadi,kabila na rangi, Itakumbukwa walianza na Zanzibara kuwafanya wakichukie chama cha CUF wakafanikiwa kuendelea kuiongoza Zanzibar baada ya kuwaua sana wananchi, lakini hawajachoka kuwafanya watanzania wakichukie chama cha demokrasia na maendeleo ili waendelee kutawala na kusema nyerere aliacha nchi yenye amani hivyo watanzania waituinze na kumuenzi Nyerere, lakini watanzania hawaambiwi kumuenzi mwalimu kwa kukemea wizi na taifa lisilojenga usawa kwa wananchi wake.
Kwani nini kinafanya amani iwepo au kipi kinasababisha amani isiwepo mpaka tuingiwe na hofu kubwa kiasi cha kuihusisha amani ya nchi na Mwalimu Nyerere na kuzungumzia swala la wapinzani kuchochea upotevu wa amani kwa kuwajengea chuki wananchi kwa minajili ya kuwweleza ile iliyo kweli kwa juu ya wizi wa rasilimali zao ulioko serikalini.
Tusijinyong’eshe kwa imani za ajabu ajabu tulizojengewa nchini muda mrefu sasa, kila kitu kinakwenda kwa muda maalum na wakati maalum. Mwendeshaji wa mambo yote ni Mungu. Yeye ndiye mwenye uwezo wote.
Viongozi wote wa vyama vya siasa, wa dini na madhehebu mbalimbali wapewe hadhi na fursa sawa na heshima isibague watu katika nafasi zao,Vyombo vya dola vitumie sheria katika kazi zao, viache kutumia jazba na chuki binafsi, wala kutumiwa na vyama vya siasa hususani watawala katika kushughulikia matatizo ya makundi ya watu na wachukuliwe hatua za kisheria wakibainika na makosa.
Haki itawale katika shughuli za kiserikali za kila siku ndio amani itadumu, wasinyimwe watu haki yao kwa wingi wao ama kwa uchache wao ilimradi haki yao wapewe na atakayezuia achukuliwe hatua ili kuepusha vurugu.
Serikali isitumie propaganda za kuwepo kwa vyama vya siasa na kufa kwa Mwalimu Nyerere kama kinga ya kuwaogopesha wanaodai haki zao wasidai kwa kuwahusisha na machafuko ya nchi, Serikali isihofishe watu na kuwakandamiza kwa kuwa tu Mwalimu ametoweka na kuwatangaza vibaya kwa wengine kuwa wanataka kuvuruga amani ili ipate kuwakandamiza kwa manufaa yao wenyewe.
WATANZANIA TUHESHIMU VYAMA VYA SIASA SERIKALI IHESHIMU VYAMA VYA SIASA, WATENDAJI WAACHE KUFANYA SIASA, WATAWALA TUSILAZIMISHE KUTAWALA PALE TUSIPO KUBALIKA NA KUKUBALI KUSHINDWA, TUHESHIMU UTU NA UHAI WA MTU, HATUHITAJI KUUA ILI TUSHINDE UCHAGUZI, WATANZANIA TUSIKATE TAMAA KUDAI HAKI ZETU HATA WATAWALA WAKITUTISHA KUTETEA MASLAHI YAO BADO TUWAAMBIE UKWELI JUU YA MIENENDO YAO MIBOVU.
 
Ndugu zangu naomba tuendelee na vita tuliyoianza kulinda rasilimali za nchi yetu ili tulete mapinduzi ya kweli katika taifa letu kwa ujumla.

Kuna taarifa zilizoenea katika mtandao huu wa jamii forum kwamba nilimkimbia John Heche kwenye mkutano uliofanyika Njombe mjini na umoja wa vijana wa CHADEMA ukiongozwa na JOHN HECHE. Huu si ukweli ila ni uongo ambao unasambazwa kwamba niliamua kikimbia kuogopa vitisho vya watu ambao si waadilifu. Ref: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...mbe-na-kutoonekana-mkutano-wa-john-heche.html

NAOMBA IELEWEKE KUWA SIPO NJOMBE KWA MUDA NIKITIMIZA MAJUKUMU MAALUMU YA CHAMA NA NITAREJEA PUNDE NA JUHUDI ZA UKOMBOZI ZITAENDELEA KAMA ILIVYO ADA.

SIKUKIMBIA MKUTANO NA JUHUDI ZA UKOMBOZI ZITAENDELEA VIJANA TUPO PAMOJA.
Wengine tuna hofu. Hayo majukumu maalum isijekuwa ni ya kutigita na wale Kigoma stars.
 
EMMANUEL MASONGA
Karibu JF Kamanda umefanya vyema kufafanua humu humu yalikoanzia ....waliolianzisha karibuni ili sisi wasomaji tujue pumba ni ipi na mchele ni upi....Ningefurahi akina ZZK wakaiga mfano wako.
 
Kamanda mbona mimi siamini kama hukukimbia,lakini sasa masonga wewew mbona hatukusikii na ile kasi yako hapa mjini kama mwanzo?

Na huonekani kwenye matukio nini kimejili?

Sasa wewe unaonekana nguvu zako za mafuta ya taa vile kaka twambie uko wapi na unafanya nini ukaamua kuacha tuuu chama huku kipo na sagasaga na lutonndwe peke yao
 
Back
Top Bottom