Maslahi ya Waisrael yawachanganya MENGI na SAKINA DATOO

Status
Not open for further replies.
Omar,
RA anafadhiliwa na nani?

Walituzuga kuwa ni WAIRAN lakini kumbe kanchi kamoja kanaitwa BOT/HAZINA....

Naamini inatosha....

By the way nilikuwa mtu wa kwanza KUTHUBUTU kumsema kuwa ROSTAM AZIZ ndiye mwenye unyang'au wa KAGODA katika kipindi cha live JENERALI ON MONDAY.....

Omarilyas
 
Bwana mdogo Omar,
embu kua kidogo, unajidharirisha wewe mwenyewe, famili yako na hata marafiki zako. Madai yako dhidi ya Mengi yanaonyesha shule haijakusaidia kabisa, kwani kimpangilio wa hoja unaonyesha kabisa uwezo wa hao role model wako kuwa walishindwa kazi ya kukufundisha shule. Dogo uko shallow sio kwa hoja tu, bali hata mpangilio wa habari yenyewe, "inasemekana" au "inahisiwa". Kijana umeenda shule, mbona unaandika kama profesa "maji marefu"?

Ninaposema hivyo ni kuwa ndiyo hivyo....kama unajua uandishi zaidi ya huu wa hapa JF basi nina uhakika unajua ni kwa nini nimetumia staili hii....

omarilyas
 
Katika hiyo habari maneno muhimu kwangu mimi ni Inasemekana, baadhi wachambuzi wa siasa na wadau wa karibu wa IPP. Kwahiyo ni habari iliyokaa kitheory theory tu........................
 
Hapa sasa tunaelekea kule; inafuata kuwa: Rostam anafadhiliwa na Iran na UAE nchi ambazo zinaunga mkono wa Palestina; Mengi anafadhaliwa na Israel na Marekani nchi ambazo zinaunga mkono uwepo wa Taifa la Israeli. Kimsingi huo kumshambulia Rostam ni kujaribu kwenda kinyume na nguvu zilizoko nyuma yake na kumshambulia Mengi nayo inakuwa hivyo hivyo...

well.. tukiendelea kufuatilia hili linatupeleka hadi wapi katika misingi hiyo ya siasa za Mashariki ya Kati?
 
Kaka naomba usome vizuri habari yangu na utaielewa maana siamini kuwa nawe umo katika mkumbo wa kuchagua watu kama walivyo wengi humu.

Tangia enzi za Balozi Mehdawi, Mengi alikuwa na mahusiano mazuri tu na Ubalozi wa Palestina. Hata alipokuwa huyu wa karibuni Yousuph mambo hayakuharibika sana na magazeti ya MENGI yaliyokuwa yakitoa makala zisizoendana na maslahi ya waisrael kuhusu Palestine. Ukweli hata mimi niliposikia habari hizi nilikataa kukubali kwanza hadi nilipoulizia huku na kule na kujumlisha na kutoa nikapata uthubutu wa kuandika suala hili.

Hata hivyo mambo yamebadilika siku hizi kwani Waisrael hivi sasa wamekuwa muhimu zaidi kwetu na wameongeza sana mashambulizi ya kidiplomasia na propaganda hapa nchini.

Kilichotokea hapa ni Mengi kama Mengi. Kachagua maslahi yake zaidi ya misingi na fikira za kizalendo kama ambavyo hupenda kuonekana.

Lakini pia kuna suala la tabia HULKA binafsi ya Mengi ya kutaka kuburuza kila mtu na kupenda kusujudiwa na kila mtu. Yote haya ukichanganya na hali yake kisiasa na mahusiano yalioshaanza kuvurugika na SAKINA kama nilivyoeleza yamepelekea MENGI kufanya makosa haya mengine yatakayomgharimu kifedha na hata kimuonekano.

Katika hali iliyopo Mengi kukubali kutupa investment yote aliyoweka kwa SAKINA na haya magazeti kwa kushindwa kucontrol his EGO na kusimamia misingi kutamuumiza sana haswa sasa wakati huu ambapo wenye CCM tayari wametangaza vita ya wazi dhidi yake.

Hili la Waislamu ni collatoral demage ya makosa yake....anione nimshauri jinsi ya kuepusha kuanguka upande huo maana gharama zake ni kubwa zaidi......sio kwake pekee bali hata kwa mustakabali wa nchi yetu pia...

Iwapo nitakuwa na mtu mzima yeyote anayehitaji ushauri wa jinsi ya kuongea na watoto na tena wenye matatizo ya mtindio wa ubongo, wasioweza kuchambua pumba na hoja nitamshauri akuone. Hiyo yaweza kuwa ndiyo niche market yako kushauri not Mengi or JF Members!
 
Hii nayo ilikuwa na umuhimu gani? come on guys kwani hatuwezi kujadili hoja hadi muanze kutukanana na kudharauliana, kupishana fikra ruksa lakini tubaki na utu wetu haina haja ya kuanzisha matusi kwenye kila thread. Its friday people show love.
 
Kuna watu wanahitaji kuwa treated namna hii, na huyu bwana mdogo ni mmoja wao.
 
Hili la Waislamu ni collatoral demage ya makosa yake....anione nimshauri jinsi ya kuepusha kuanguka upande huo maana gharama zake ni kubwa zaidi......sio kwake pekee bali hata kwa mustakabali wa nchi yetu pia...

omarilyas

Omar Ilyas,
Huna lolote zaidi ya kutafuta shortcurt za kisiasa, siasa haiendi na udini. Kama kuna vilaza wanaoweza kuleta maafa kwa vijana basi wewe ni mmojawao. Naona umeshaanza kudivert issue za ufisadi kwa kutaka kumuhusisha Mengi na Waisrael, ili iweje? nani anakulipa kwa uhalifu huu? ONYO: Omar utajiharibia ndugu yangu kwa kuanza kujiingiza kwenye vita isiyokuhusu, na kuanza kuwapandikizia ubaya watu bila sababu, kwani kuanza kuonyesha Mengi yupo against waislamu, ni uhalifu mbaya, kwani ufisadi unawahathiri zaidi Watanzania bila kujali uislamu au ukristo. Stop that stupidity dogo.
 
Katika hiyo habari maneno muhimu kwangu mimi ni Inasemekana, baadhi wachambuzi wa siasa na wadau wa karibu wa IPP. Kwahiyo ni habari iliyokaa kitheory theory tu........................

Mnataka asemeje sasa? Najua hili nasema hivi inakuwa hivi?
Watu bana kumbe mpo wengi kwenye pay roll
 
Duuuh, tunaomjua Omar ni wengi basi. Mi sikutaka kumgusa Omar kama Omar, najua anamezeshwa na kina Zitto na mpambe wake Hussein Bashe mwana wa Rostam ambaye ndo mchonga deal za hela za kumsafisha JK.
bashe mpinzani wa seleli??????

naona dot nyingii sasa......
 
Nimefuatilia suala la SAKINA na ukweli ni huu: Huyo msichana sio competent kama Mengi alivyodhani wakati anamchukua kutoka Mwananchi Communications. Ana uwezo wa kupiga domo lakini sio utendaji wa kazi za kiuandishi. Halafu yeye hakuwa Mhariri Mtendaji, bali aliundiwa cheo akiitwa 'Group Editorial Director', ingawa aliishia kufanya kazi za kiutawala tu hapo The Guardian, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha safari za waandishi wa habari, na kufikia hata kupunguza posho za safari za waandishi.

Alianza kulalamikiwa na wahariri wa IPP wakihoji uwezo wake lakini Mengi aliwapuuza licha ya kuandikiwa barua akielezwa kuwa hana uwezo wowote zaidi ya porojo na majungu. Alileta mgawanyiko mkubwa pale The Guardian kutokana na majungu na kujikweza kwake, huku akiwagawa waandishi. Alijaribu bila mafanikio kumuenguaa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Kiondo ili yeye awe kama CEO wa The Guardian.

Matatizo hayo na mengine mengi (ambayo nitayaeleza baadaye) ndiyo yaliyosababisha kuenguliwa kwake, na cheo cha 'Group Editorial Director' kufutwa. Sasa anatakiwa kuripoti This Day na Kulikoni ambako atapangiwa kazi nyingine kwenye gazeti ambalo halipo, litakaloitwa 'This Day on Sunday.' Ila kwa haraka haraka sidhani kama ataiva na kundi la wanahabari waliopo pale This Day kwani ni watu wanaoipenda kazi yao na hawana majungu wala hawajipendekezi kwa mtu yeyote. Ni kundi la marafiki wa muda mrefu waliofanya kazi pamoja kwenye vyombo mbalimbali na wenye mshikamano wa hali ya juu. Na hii ndiyo sababu kubwa ya mafanikio ya magazeti hayo kuweza kuandika habari nzito za ufisadi kwa muda mrefu sasa bila kuyumba. Naamini Mengi mwenyewe anawaheshimu sana wanahabari hawa, hatapenda kuona wakisambaratika.
 
Taarifa nyingine ni kwamba wafanyakazi wa The Guardian walishangilia na kunywa bia baadaa ya kusikia Sakina ameondolewa. Nasikia hata kule Mwananchi Communications walifurahi sana alipoondoka na kusema ni 'good riddance'.
 
Kuna watu wanahitaji kuwa treated namna hii, na huyu bwana mdogo ni mmoja wao.

you can simply do that by writing a private mesage if you have anything personal with him, and please lets not debate on this coz its out of discussion.
 
This Day kwani ni watu wanaoipenda kazi yao na hawana majungu wala hawajipendekezi kwa mtu yeyote. Ni kundi la marafiki wa muda mrefu waliofanya kazi pamoja kwenye vyombo mbalimbali na wenye mshikamano wa hali ya juu. Na hii ndiyo sababu kubwa ya mafanikio ya magazeti hayo kuweza kuandika habari nzito za ufisadi kwa muda mrefu sasa bila kuyumba. Naamini Mengi mwenyewe anawaheshimu sana wanahabari hawa, hatapenda kuona wakisambaratika.

Sauti ya simba inaonekana taarifa zako ni za uhakika zaidi, na maelezo hayo niliyoyanukuu ni kama u mmoja wao, sasa tuambie ni kweli huyu dada kakataa hiyo kazi ya this day on sunday kama inavyoelezwa na omar?
 
Hongera wana JF woote mliyoshtukia na kumshugulikia vilivyo bwana Omarilyas kwa ulaghai wake, watu kama hao wako wengi tu humu nalengo lao ni hilo hilo kuingiza maslahi ya udini kwenye kila jambo! Hatuwezi kupiga hatua kwa staili hiyo.
 
Bwana mdogo Omar,
embu kua kidogo, unajidharirisha wewe mwenyewe, famili yako na hata marafiki zako. Madai yako dhidi ya Mengi yanaonyesha shule haijakusaidia kabisa, kwani kimpangilio wa hoja unaonyesha kabisa uwezo wa hao role model wako kuwa walishindwa kazi ya kukufundisha shule. Dogo uko shallow sio kwa hoja tu, bali hata mpangilio wa habari yenyewe, "inasemekana" au "inahisiwa". Kijana umeenda shule, mbona unaandika kama profesa "maji marefu"?
.....
Mbona Omar anaeleweka! Vizuri tu ktk post yake! nadhani kweli hii post imewashika pabaya wape vidonge wakimeza wakitema shauri yao?
 
Katika hiyo habari maneno muhimu kwangu mimi ni Inasemekana, baadhi wachambuzi wa siasa na wadau wa karibu wa IPP. Kwahiyo ni habari iliyokaa kitheory theory tu........................
....
Labda kwa kuwa inamhusu FISADI NYANGUMI ndiyo maana inaiyona iko kitheory theory, ingemhusu RA ndiyo ungeiona ika kipractical zaidi enhee.,!?
 
Kuna watu wanahitaji kuwa treated namna hii, na huyu bwana mdogo ni mmoja wao.
....
Hapana! Kila mtu yuko huru kutoa maoni kwa mujibu wa anacho kiamini
Huna sababu ya kutoa matusi matusi ni dalili ya kushindwa na hoja iliyopo uwanjani.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom