Maskini Salmin Amour! MUNGU AKUPE NGUVU

Nasikia hata Mataka wa PPF enzi hizo alishataka kula mzigo baada ya kugundua kuwa komando ni mcameroon
 
Lyatonga, aliwahi kusema siku moja kuwa nchi hii inaongozwa na mashemeji zake, akamtaja komando, sumae, ben na kama sikosei marehemu dk. omary kwa wakati huo. Na aliongeza kwa kusema hawamtii hofu vinginevyo atawaamru dada zake warudi uchagani. Leo shemeji yake anaumwa, nini kauli yake bwashemeji...
 
dah kabla hujafa hujaumbika yule mke wake wa zamani atakuwa anahusika
Yule mmachame siku nyingi kwisa ondoka baada ya mzee kustaafu akaona U 1st lady umekwisha ngoja ajiondokee zake ,radio mbao zinasema alikuwa na hekalu Mikocheni ndiko anakoishi hata yule kaka yake brazameni wa pale Bungoni Ilala nae kapotea baada ya ushemeji kuota mbawa
 
UNAMMAANISHA SALMA?? HUYU MAMA NAYE KWAO WANAKUFA NDUGU ZAKE KARIBU WOTE WAMEKUFA SIJUI NI NINI? HAPA KWAO PAMEBAK HOUSEGIRL TU , PAMECHAKAA HUWEZI AMINI KM NI NYUMBANI KWA MKE WA RAIS, ngoja niache umbea
Kuna kaka yake mmoja brazameni wa ukweli alikuwa anaitwa Muddy alikuwa anaishi mitaa ya Bungoni Ilala naye haonekani siku hizi,enzi zile shemeji yupo madarakani jamaa alitikisa sana pande ya jiji la maraha D'salaama siku hizi kimyaaa sijui kunani
 
Salma Salmini alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu anaehusishwa na Muamar Gadaffi, kama si yeye mwenyewe ni mwanawe, na alianzia tangu wakiwa madarakani manake Kamandoo alikuwa rafiki wa Gadaffi au japo alikuwa anajipendekeza sana kwake.
Labda dhambi ya kuua bandari ya Zanzibar nayo inamwaadhibu, mnakumbuka enzi zile watu wanafurika toka Tanganyika kuja kukomba vitu bei chee Zanzibar? hiyo iliisha mwanzoni mwa miaka 2000 Salmini alipotaka Bandari Huru ya Zanzibar (out ya bandari za Tanzania) kwa hiyo bandari ya zanzibar peke ya haina uwezo wa kujiendesha au kuleta meli kubwa peke yake moja kwa moja.
Mimi nafikiri wakati ule raisi alikuwa Mohamed Raza,pamoja na kuwa mshauri wa michezo yeye ndie alikuwa kila kitu,kulipa mishahara ,aliwahi muhamisha askari mmoja pale bandarini baada ya kuambiwa yakhe panga foleni wakati yeye ni'raisi'
 
katili kwa nani?

1.Alifukuza kazi Watumishi wengi wa Serikali bila sababu ya msingi.

2. Alivunja nyumba za watu maskini ambao hawakumchagua katika uchaguzi wa mwaka 1995. Baadhi walikufa kwa presha.

3.Aliwaweka ndani wanachama wa Cuf akiwatuhumu kuwa ni mahaini. Alipoenda kuombwa awaachie huru akasema kuwa wale ni watu na si mapapai kama yataoza.

4. Enzi za utawala wake ilikuwa kupigwa virungu na askari ni jambo la kawaida.
 
Huyu Mzee wana hana hali... kinachoskikitisha zaidi ni kuwa serikali haitaki kumsamehe na kumsaidia. Ameanza kuugua miaka mingi sana na yuko pale kigamboni kama mwana mpweke, yaani familia yake imeachwa imhudumie yenyewe kana kwamba hakuwa kiongozi wa kitaifa. na hali ya afya yake ni mbaya sana
Nje ya mada ya Salmin. Huyu mzee Jumbe alikuwa rais wa Zanzibar, hata umakamu wa rais wa muungano ulitokana na urais wake wa Zanzibar. Serikali inayowajibika kumhudumia ni ipi kati ya SMZ na serikali ya Muungano? Kwa nini hataki kurudi kwao visiwani?
 
Mkutano Mkuu wa CCM wa kuteua mgombea urais Zanzibar Mwakajana alifika Dodoma akiongozana na huyu Waziri wa mambo ya Ndani Vuai, mwonekanao na tembea yake akitegemezwa na watu kadhaa kumzunguka ilikuwa inaonyesha kila dalili ya kupungukiwa na nguvu katika moja ya milango mitano ya fahamu ingawa wakati huo alikuwa ametoka matibabuni nchi za nje yaliyoratibiwa na Shamsha Vuai akiwa kama Waziri Kiongozi wa Zenj.
Ana dalili zote za kuathiriwa na kiharusi.
 
Inamaana nae anapigwa bomba kama marehemu mzee kawawa au?


Jamani tuwe na heshima na staha kwa viongozi wetu......uhuru wa kuongea chochote usiwe uhuru wa kuropoka kila unachowaza kichwani kwako. Tupime ya kuandika hapa jamani. Dah
 
Tumpe pole maana aliyoyafanya kama binadamu tumsamehe ila ukweli utabaki kuwa jamaa alikuwa katili
 
malipo duniani akhera huenda hesabu tu,huyu salmin komandoo feki alitesa sana watu na alidhalilisha sana watu wote waliokua na muelekeo wakutaka mabadiliko ya kidemokrasia,mpaka leo huko zenj watu wanamlaani nakumuombea mabaya zaidi,wakati wautawala wake watu waliuliwa,walibakwa,na walifanyiwa ukatili wa kila aina,alivunja majumba ya watu eneo la mtoni unguja kwa chuki za kisiasa tu,kwahakika mungu hulipa duniani,kama huamini kama huyu salmin alikuwa katili muulize juma duni haji waziri wa sasa wa afya zenj ambae ni mjobawake na salmin aliteswa nakuwekwa ndani miaka3 kwa sababu za kipuuzi za kisiasa.

Nadhani msofe amekuelewa
 
Salmini alidanganywa na madaraka kiasi cha kuwa rais wa pili kuua watu wasio na hatia baada ya Abeid Karume ukiachia mbali kuona mpalestina toka Machame asijue moto mtupu. Ingawa Salimuni Amri ni wa kuonea huruma, twapaswa kujifunza kuwa wanyenyekevu. Maana avumaye bahari papa na isitoshe binadamu ni nini hadi ajione wa maana wakati ni mavumbi matupu? Mie ni mwanafalsafa tu.

Mwanafalsafa hapayuki
 
Jamani wapendwa
nimemwona mh wetu rais wa zamani wa zanzibar mh salmini amour
akiwa anaongozwa na kifimbo hakika nikahuzunika sana sana
nilipouliza jamani kuna nini ndipo nikajuzwa maskini haoni amekuwa hivyo muda kidogo
mwisho namtakia heri hata akishindwa kuona vingine basi vya kitandani aone
kila lal kheri baba
Hii ni mojawapo ya njia za kuwajua wakwale!
 
Komando alitaka kubadili katiba ili awe Rais wa maisha Zanzibara,sa sipati picha kama angefanikiwa,ina maana leo Zanzibar Rais angelikuwa kipofu,Duuh masikini komando,kweli hujafa hujaumbika,pole japo huoni sms yangu.....!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom