Maskini rais wanguuu...

Status
Not open for further replies.
Pengine huo unaweza ukawa ni ushahidi tosha wa namna mikataba yetu inavyosainiwa na mawaziri.
 
RAIS Jakaya Kikwete akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani 300,000 sawa na zaidi ya Shilingi za Tanzania Milioni 400 kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) kwa nchi ya Tanzania na Uganda Bw, John McIntire Dar es Salaam jana. (Picha na Rajabu Mhamila)
Hawa ni Majira


President Jakaya Kikwete receives cheque for USD 200,000 from the Leader of CEO Roundtable, Ali Mufuruki during the launch of CEO Scholarship fund in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Tryphone Mweji)
Kipande hiki toka Ippmedia

hivi JK alipokea cheki ngapi?
 
Jamani msiniue kwa kicheko, yaani nimecheka leo na machozi yanatoka. Bahati niko peke yangu ofisini maana kuna mtu angeniona angefikiri nimechanganyikiwa.

Yaani mungu wangu matatizo ya kukimbilia kila opportunity ya kupigwa picha.

JK una kazi baba mwaka huu, hao watu wote unaoongozana nao, wanafanya nini?
JF babu kubwa!!!
Wanasubiri kukatiwa chao... mwendo mdundo kama wasemavyo... na ndiyo maana tunaona madudu kama haya katika kila kona ya maisha ya Watanzania!

Na haya yote ni mapungufu ya kutokuwa na 'jicho pembufu'. Utamaduni wa kuuliza maswali umedumaa na umedidimizwa kwa kivuli cha filosofia ya 'amani na utulivu'.

Haraka haraka za kupokea kila kitu upewacho badala ya kujiuliza kwanza na kukipigia 'chabo' ili ujue undani wake. Tumekuwa majalala ya taka za bidhaa hadi mikataba. Photo opportunity zimebakia kuwa 'photo opportunities' zisizo na malengo ya kitaifa bali matakwa binafsi ya kujihusisha katika kila kitu hivyo yale yafanyikayo kama mwangwi wa Taifa hayapo tena, kwani matakwa binafsi yametawala... Ya kuwa mimi nilikuwa hapa, mimi nilifungua hiki, mimi nilipokea hiki; badala ya hiki kilifunguliwa kwa nia hii, mimi nikuwa hapa kwa ajili ya hili, n.k kwa ajili ya taifa langu.


YOU KNOW WHAT, SOMEHOW THE INCIDENT EPITOMISES THE STATE OF OUR NATION.

SteveD.
 
Naona watu wanapata shida isiyo ya lazima:

a. Huo ulikuwa ni ufunguzi wa Mfuko wa ma CEO
b. Ma CEO mbalimbali walikuja na michango yao huyu mzungu na mafuruki ni miongoni mwao.
c. Bila ya shaka benk ambayo imefunguliwa akaunti ya mfuko huo ni Exim
d. Hivyo hizo mnazoziangalia ni cheki mbili tofauti siyo cheki ile ile zikionesha michango ya MaCEO hao.
e. Cheki ya Mafuruki haina tatizo na imeripotiwa sawasawa
f. Cheki ya Mzungu imeripotiwa ikionesha kiasi kilichoandikwa kitarakimu lakini ikiwa na maneno yasiyolingana na kiasi hicho.
g. Hivyo This Day imesema kweli, na the Citizen imesema kweli!!
h. Tatizo Picha imeonesha UONGO!
 
unajua mwanakijiji wengi wanaamini unayosema hapa JF, sasa unaposema picha imeonyesha uongo maana yake nini ? au ndio wikiendi tena !
 
unajua mwanakijiji wengi wanaamini unayosema hapa JF, sasa unaposema picha imeonyesha uongo maana yake nini ? au ndio wikiendi tena !

wikiend inaanza jumanne?kaaazi kweli kweli, ebo au kuna kitu hapa nimekimiss?!!
 
And then He wonders why Tanzania is not developed. He is holding the answer.
 
Kwa maoni yangu Raisi Kikwete hana tatizo.yeye kama raisi alikuja pale kuzipokea hundi hizo na wasaidizi wake lazima wazikague hundi hizo ni sawa na nikitaka kumpelekea raisi zawadi alafu kumbe ndani kuna bomu,wasaidizi wake wanafanya uzembe wa hali ya juu sana kwa kutokagua kazi anazopaswa kufanya raisi kwenye public.

Kwa mfano Muungwana aitwe kwenda kuweka jiwe la msingi la shule.Huwa tunaona kuwa anafungua kile kitambaa anapigwa picha hapo.Sasa je kama wasaidizi hawajakagua ni kweli shule inafunguliwa sio kuwa linafunguliwa dangulo.Nani mwenye makosa hapo?
 
Majira_09_Oct_07.JPG


The message is self explanatory! Nothing more nothing less! Kuna mwenye kujua nini namaanisha? Kazi ipo... Ni kutoka gazeti la Majira la leo Oktoba 9, 2007

Picha kama hizi wazungu ndio wanatumia kueneza propaganda jinsi gani hata maraisi wetu walivyo bogasi.

Inachekesha sana na inatia huruma.Hii picha akitokea mgeni akanionyesha na kutoa majina mabaya kwa raisi wetu kweli sitakuwa na la kumjibu.

Ule msafara wa watu 50 kazi zao huwa ni nini? wenyewe wako wanagombania kababu,keki na chai ya maziwa hawajui kinachoondelea ukumbini
 
That is precisely what you get when you have a nation that is led by seedy characters. They are unable to tell a 3 from a 2. I propose that they cannot tell a 30 from a 3 either! I wouldn't be surprised at all if it were to emerge that they accepted mining contracts that pay 3% royalty thinking that it was 30% !

I was going to compare these guys with Idd Amin, but I thought that would be unfair to Amin. He made mistakes, not blunders.
 
Tena JK analetewa ile hundi kubwa kinyumenyume haioni lakini kabla ya kupewa mikononi nasikia lazima wanausalama waikague ukaguzi huo ni kuangalia material waliyotengenezea au ni ukaguzi gani? Hapa ndipo tunaporudi katika mikataba yetu mambo huwa hivyo hivyo.

Unasaini kitu usichokijua hapo Kikwete amepokea kiasi gani? Akikuta kapewa laki mbili hawezi kurudi kudai iliyobaki au tujumlishe iwe laki tano? Yeye ametia dole kwamba mambo poa tu. Ni aibu sana kwa wasaidizi wake yeye kama rais hawezi kuwa kila kitu yeye mwenyewe, msaidieni. Akikosea msisite kumshauri kwamba Mzee hapa hivi sivyo yeye si malaika kwa kuwa tumekuwa tukilalamikiana juu ya matumizi mabaya hapa ni namba moja hapo mtu aidha kala laki moja ama kaliwa laki moja.

Tunapoingia rasmi katika mikataba lazima kuwe na wataalamu wa uchambuzi wa vipengele vya mikataba, nakumbuka wakati Rais anawateua Mawaziri wake aliwaambia kuwa uwaziri hauna shule akimaanisha kwamba yeyote anaweza kuteuliwa kuwa waziri katika wizara yoyote ile hata kwa wizara ambayo angeibuni siku ile ile. Unapoambiwa unatakiwa kujikosha ujue wenzio wanaona umechafuka kuchafuka kwenyewe ndiko huko unachafuka mchana kweupeeee.

Lakini scandal kama hii ingemkuta Mwl Nyerere huyo aliye saini hapo angewajibishwa na ingekuwa fundisho. Hata hivyo aibu imeshatokea hatuna jinsi ya kurekebisha tuelewane kiutu uzima tu.
 
Wakifanya vizuri wasaidizi wa Rais, sifa anapewa Rais. Wakifanya vibaya, lawama ni za Rais vile vile. Sisi hatuwajui, tunamjua Mtukufu Rais. Kama amechagua wasaidizi waliolala, basi wanachafua jina lake, na sio majina yao, kwani hawana kwanza hayo majina.
 
Inawezekana hawa CEOs walipanga ili kuihakikishia IKULU kwamba hata mikataba wanayoisaini huwa na michezo kama hiyo wakajadili kwamba ili kuwapa somo hawa IKULU tufanye hivi ili watambue kuwa wanavyodhani wanajua CEOs wanajua zaidi.
 
ni aibu kwa JK lakini ni aibu kwa watanzania wote, kuongozwa na mtu wa namna hii!

mnafikiri mtu wa nje akiona hii atamsema JK tu?.....tumevuliwa nguo watanzania wote kwa hili, naona hata haya kuitizama mara mbili hii picha! UOZO KWENDA MBELE :mad:
Ndio,maana 80% iliona huyu ndio bora kuliko wote!
 
Inawezekana hawa CEOs walipanga ili kuihakikishia IKULU kwamba hata mikataba wanayoisaini huwa na michezo kama hiyo wakajadili kwamba ili kuwapa somo hawa IKULU tufanye hivi ili watambue kuwa wanavyodhani wanajua CEOs wanajua zaidi.
Bubu Msemaovyo uko sahihi kabisa.Hata hivyo hiyo picha yako hapo pembeni walao imenipunguzia hasira nilizonazo kwa watawala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom