Maskini Prof Mbwete wa OUT

Inasikitisha sana kwa sie tukie mpenda ila bwana amempenda zaidi
naamini atamfungulia njia nyingine;prof tunakupa hongera kwa uliyofanya hii ni kazi kila mtu anapita

open with sadness

Mkuu unatutisha bwanaaaaaaaaa!
Mie nilifikiri kafariki?
Hayo mbona mambo ya kawaida sana katika utumishi wa umma? Huenda tenure yake imekwisha na hajataka kuongeza nyingine, ama serikali haijataka kumuongezea nyingine, so anatafuta ustaarabu mwingine.
Heading inatisha mkuu, ila asante kwa info.
 
"NITOKE VIPI" NYINGINE BANA MHHH!!!
UTAFANYA WATU WAZIMIE ILHALI NI KITU CHA KAWAIDA!
Next time ndugu, kuwa mstaarabu hata kama unataka kutega watu wakusome siyo kwa mtindo huu!

Lakini avatar yako imenimaliza zaidi.
 
Jamani hizi style za uandishi kazi kwelii kweli

Nachokijua ni kwamba serekali ilibadilisha sheria, nakuweka kikomo cha uongozi kwa wakuu wa hivi vyuo vikuu vya umma.Nafasi i ya u vice chancellor (VC) inakuwa ni mihula miwili ya miaka mitano mitano,, Ukimaliza miaka yako mitano nafasi inatangazwa public kila mtu mwenye sifa anaweza kuomba, na aliyemaliza mhula moja na yeye anaruhusiwa huomba, wanafanyiwa interview anayeshinda ndo anapewa mamlaka ya kuendesha chuo.

navyojua kwa Prof Mbettwe ametawala OUT huu ni mwaka wa tano,na wametangaza hiyo nafasi na yeye naamini ataomba kwani sheria inamruhusu iakishinda interview ataendelea kuwa mkuu wa chuo, lakini kipindi chake cha pili kikisha hataruhusiwa tena kuomba, labda kwa chuo kingine kama UDOM au UDSM,
 
Hii heading siyo kabisa sasa hapo maskini umeweka ya nini? bora ungesema Prof.Mbwette amwaga manyanga out?Mi nlijua katutoka yani!
 
Inasikitisha sana kwa sie tukie mpenda ila bwana amempenda zaidi...... open with sadness

Hopeful hutarudia kuandika bandiko lingine kwa mtindo huu...was disgusting, to be polite!
Au mkuu ulitaka tukueleweje?
 
My professor!

Mkuu tafadhali edit thread yako, ulinifanya nisipumue kwa muda!
 
Mara nyingine nashawishika - beyond reason- kufikiri kwamba labda vichwa vingine badala ya kuwa na mbongo vimejaza utumbo.
 
Wewe Mhalisia unapotosha watu kwa heading yako bana .Chunga unaweza kukatisha roho za watu pasina sababu.BE CAREFUL ON WORDING!!!!!!

Yaani umesema lililokuwa kichwani kwangu Kimatire. Nilipanic nilidhani ameumia sana au hatunaye. Mnajua kuna ndugu za watu hapa muwe makini katika kuandika.
 
Labda hajui maana ya "sie tulimpenda lakini bwana kampenda zaidi." Au ana chuki kiasi kuwa kuacha kazi kwa prof, kakufananisha na kifo. I think the prof has a life, na mtu mwenye CV kama ya Mbwete atapaa kazi nyingine na nzuri wakati wowote atakao.
 
Jamani hizi style za uandishi kazi kwelii kweli

Nachokijua ni kwamba serekali ilibadilisha sheria, nakuweka kikomo cha uongozi kwa wakuu wa hivi vyuo vikuu vya umma.Nafasi i ya u vice chancellor (VC) inakuwa ni mihula miwili ya miaka mitano mitano,, Ukimaliza miaka yako mitano nafasi inatangazwa public kila mtu mwenye sifa anaweza kuomba, na aliyemaliza mhula moja na yeye anaruhusiwa huomba, wanafanyiwa interview anayeshinda ndo anapewa mamlaka ya kuendesha chuo.

navyojua kwa Prof Mbettwe ametawala OUT huu ni mwaka wa tano,na wametangaza hiyo nafasi na yeye naamini ataomba kwani sheria inamruhusu iakishinda interview ataendelea kuwa mkuu wa chuo, lakini kipindi chake cha pili kikisha hataruhusiwa tena kuomba, labda kwa chuo kingine kama UDOM au UDSM,

Mimi nafikiri kuna mawili hapa either jamaa ni mwandishi wa magazeti au vijarida vya udaku au anategemea kuapply au kama hategemei mi ningemshauri aende huko manake anafaa, si mnajua magazeti yetu ya udaku? Anakuandikia heading ya kukuvuta ujue nini kilichopo ndani lakini ukinunua ni tofauti kabisa. Kazi kweli kweli mzee unaua watu wangali hai hili ni kosa
 
Back
Top Bottom