Dickson Ng'hily
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 451
- 485
Magufuli matatani
- JK naye amshambulia waziwazi
na Betty Kangonga
SIKU chache baada ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kudaiwa kwamba alikusudia kujiuzulu kwa madai ya kuingiliwa katika utendaji wake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana Rais Jakaya Kikwete naye aliigeukia wizara hiyo akiitaka iache ubabe katika kutekeleza zoezi la bomoabomoa huku akitoa kauli ya kumshambulia moja kwa moja waziri huyo.
Hali hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa Magufuli bado anakabiliwa na shinikizo la kuingiliwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kiuwaziri.
Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia zoezi hilo la bomoabomoa ambalo mara kadhaa alinukuliwa akisisitiza azma yake ya kuhakikisha nyumba na majengo yaliyoingilia hifadhi za barabara yanabomolewa ili kupisha miradi kadhaa ya ujenzi ukiwemo ule wa miundo mbinu kwa ajili ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.
Mbali na Magufuli, Profesa Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pia ni mmoja wa mawaziri ambao wamekuwa wakitekeleza zoezi la bomoabomoa, lakini katika hali ya kutiliwa shaka, Rais Kikwete amejikuta akimruhusu waziri huyo kutekeleza operesheni za wizara yake bila kumhofia mtu yeyote wala cheche zozote.
Kikwete alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Wizara ya Ujenzi na baadaye kutembelea Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wa idara zilizo chini ya wizara hizo na mashirika yake.
Lazima uangalie historia ya barabara imetoka wapi.siyo kuja na kubomoa maana hakuna mtu anayeweza kubomoa nyumba yake kwa saa 48, alisema Rais Kikwete akionekana dhahiri kumlenga Magufuli aliyekuwepo hapo.
Alisema ni kweli zipo sheria zinazowataka wananchi waliojenga katika hifadhi ya barabara wahame lakini kuna ubabe unaofanywa na wizara hiyo ya Magufuli katika zoezi la bomoa bomoa.
Alisema wapo baadhi ya wananchi wamekaa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo na kuweka vitu mbalimbali hivyo unapowabomolea leo ni kutaka kuwafanya waichukie serikali.
Akitolea mfano barabara ya Chalinze mpaka Segera katika eneo la Msata ambapo kuna barabara kuu inayoelekea Bagamoyo, alisema katika eneo hilo la barabara ya asili kuna nyumba za zamani za wakoloni ambazo zimewekwa alama ya X inayoashiria kuwa zitabomolewa na kuielezea hatua hiyo kuwa ni uonevu.
Alisema huo ni uonevu kwa kuwa barabara inayotaka kujengwa ndiyo iliyofuata wananchi hivyo wathaminiwe na walipwe fidia kitendo cha kupiga X ni uonevu hivyo aliitaka wizara hiyo iache ubabe.
Aliitaka wizara hiyo kuhakikisha inaweka utaratibu maalumu na kuzifanyia upembuzi barabara zote muhimu na siyo kusubiri mpaka fedha zipatikane au bajeti.
Alitaka fedha za barabara zinazotengwa kuhakikisha zinatumika kikamilifu hasa kwa zile za halmashauri na kuunda kitu kitakachoitwa Bodi ya Wakaguzi ambayo itapitia hifadhi zote za barabara na kuepusha suala la bomoa bomoa.
Unakuta watendaji wanapita katika barabara hiyo wanaona watu wanavyojenga bila kuchukua hatuamtu akimaliza nyumba yake mnafika na kumbomolea huku wengine wakipoteza maisha kutokana na shinikizo la damu hapana hili lazima tulisimamishe, alisema.
Alisema kuwa serikali imechota fedha kutoka katika bajeti za wizara mbalimbali jumla ya sh bilioni 250 kwa ajili ya kuipa Wizara ya Ujenzi ili kuweza kuongezea katika kulipa madeni mbalimbali yanayowakabili.
Alisisitiza wazo la kuanzishwa kwa usafiri wa reli akitolea mfano treni inayoweza kuanzishwa kwa kuanzia stesheni mpaka Kimara Temboni ambayo inaweza kupunguza msongamano wa foleni barabarani.
Msitegemee sana usafiri wa mabasi yaendayo kasi, yanaweza kusaidia katika kipindi hiki lakini kumbukeni kuwa idadi ya watu inaongezeka kila kukicha hivyo kwa miaka 10 ijayo tatizo linaweza kuwa kubwa jaribuni kuangalia na njia nyingine, alisema.
Kwa upande wake, Magufuli alisema wizara yake inakabiliwa na changamoto balimbali ikiwa ni pamoja na kiasi cha fedha wanachotengewa kutotolewa kwa wakati.
Alisema hatua hiyo imesababisha makandarasi 35 kutoa notisi kutokana na ucheleweshaji wa malipo ambayo ni sh bilioni 454 zinazodaiwa. Kwa upande wake Profesa Tibaijuka alimuahidi Rais Kikwete kusimamia na kutekeleza yote anayoagiza ikiwa ni pamoja na kurudisha maeneo ya wazi lakini alimuomba pindi maneno yanapokuwa makali dhidi yake amlinde. Alisema wizara yake imepungukiwa wataalamu kwa asilimia 74 katika halmashauri na waliopo hawana sifa stahili.