Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,364
ya kaisali mpe kaisali na ya mungu mpe mungu
Unamaanisha tuendelee kumlea jk bila kumwajubusha? ama una maana gani?
ya kaisali mpe kaisali na ya mungu mpe mungu
huenda wakati huo ikawa too late, ni bora akaachia sasa hivi, unakumbuka THB au RTC? ilikuwa hivyo hivyo mpaka maduka yote yakafa.
Ah! Hiyo ilitokea kwa awamu ya RAIS yupi, if I may ASK?
Kwa jina la Raisi Kikwete ni Mbovu kama Benki ya THBhuenda wakati huo ikawa too late, ni bora akaachia sasa hivi, unakumbuka THB au RTC? ilikuwa hivyo hivyo mpaka maduka yote yakafa.
Aliulizwa kwa nini nchi ya Tanzania masikini akajibu hata yeye hajui!!!!!!!!!!!!! Mkuu wa kaya huyo!!!!!!
Wakati wa mzee wa Ruksa, mjanja hujifunza kwa makosa ya wengine na siyo makosa yake mwenyewe, tukisubiri mpaka muda wake uishe huenda hata hivi tulivyonavyo ambavyo vimechoka vitakufa kabisa. Aachie sasa kwa maslahi ya Taifa na watanzania kwa ujumla.
Brilliant indeed!!! Swali? Mzee Ruksa kaongoza kwa kipindi cha miaka kumi -right? Kaja BEN naye kaogoza kwa miaka kumi-eh? - Oh just a second, tusisahau awamu ya Kambarage ambayo kwa kipindi cha takribani miaka kumi na tano kabla ya kung'atuka kwake, tukiwa wakweli atuwezi kusema kwamba kipindi cha mwisho cha Kambarage TANZANIA was a bed of ROSES, tulikuwa na wakati mgumu sana kiuchumi.
Hebu tujaribu ku-analyse awamu zote tatu bila kuwa biased/jazba, kwa hesabu za chapu chapu inaonekana TAIFA letu limekua kwenye Economic TURMOIL na Mismanagement kwa kipindi cha miaka 35 (thelathini na TANO) repeat 35 kabla ya Jakaya hajashika usukani, hilo watu awalioni/kumbuka. Hivi tunamtendea haki kutegemea kwamba Jakaya anaweza kweli kusafisha madudu walio hacha wenzake within a record TIME ya miaka SITA!!!! hata Marshal plan haikuwahi ku-achieve such a feat at such a megaspeed.
Come on folks, tuwe wakweli bila ya kusutwa na dhamila ZETU - haya mambo ya kumlaumu wholesale na kumuita majina ya kila sampuli hayawezi kulisaidia TAIFA letu, raia wenye nia njema na TAIFA lao wangekuwa wanampa ushauri however crude bila kumuogopa au kuwa na hila za aina fulani kwa kumlahumu karibu kila kitu as if yeye alihusika moja kwa moja na matatizo ya TAIFA letu - wakati mambo yenyewe yalikuwa yamekwisha ota mizizi kwa kipindi cha muda mrefu TU (miaka 35) - WHY PICK ON HIM, if I may ask? Nauliza hili swali kwa kwa nia nzuri TU.
Mkuu, Rais wetu sio DHAIFU ila sisi watendaji wake ndio DHAIFU kama tukifanya kazi kwa bidii nchi hii itabadilika. Tukiona mtu hafanyi anachotakiwa kufany ni bora tumkanye. Hata ufisadi utaisha tukikemea maovu.
Ndugu mbona unazunguka sana? Nimesema mjanja ujifunza kwa makosa ya watu wangine na si kwa makosa yake, Jk alitakiwa kurekebisha makosa ya awamu zilizomtangulia, hata Raisi atakae kuja baada yake kama atashindwa kurekebisha makosa ya awamu zilizomtangulia naye tutamshambulia na kumpa majina kama tunavyofanya kwa Jk bila kujali atakuwa nani au anatoka chama gani.
nimekaa na kufikiri nikaona kama jk ameingia ulingoni kupambana ngumi (kuiongoza tz) ktk ulingo usiokuwa na muamuzi (raia ambao ni walalamikaji tu) na kocha wake (bunge). Halina mbinu mbadala. Jk kaelemewa sana na mpinzani wake (matatizo yaliyopo nchini) uso wake (wananchi) hautamaniki jinsi ulivyovimba na kutapakaa damu, kocha wake wala hana mpango wa kutupia taulo ulingoni na ni round ya 9, maskini jk, sijui mwisho wake itakuwaje! Hapa namaanisha raisi wetu nchi imekwishamshinda na hakuna chombo chochote cha serikali kitakacho mnyang'anya raisi madaraka mpaka atakapo maliza muda wake (huu ni udhaifu wa muundo wa kuiongoza serikali) wala wananchi hatuna ubavu wa kuingia street kumtoa raisi, wabunge nao wanaona poa tu raisi hajiwezi (dhaifu) lakini hawachukui hatua yoyote kuliokoa taifa. Nafikiri katiba mpya ni lazima kuwe na kipengele kinachosema kama itaonekana raisi hajiwezi kuiongoza nchi (dhaifu) basi aondolewe kikatiba kulinusuru taifa.