Bornvilla
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 924
- 271
Haya ni masikitiko makubwa kwa upande wangu pamoja na wale wanaothamini historia yao. Bob Marley alipata kusema"if you don't know your history,then you don't know where you are coming from".

Jijini Mwanza kuna alama ya mti ambao ulitumika kuwanyongea Waafrika wapinzani wa Ukoloni na serikali yake.Mti huo uko citycentre,umekatwa na kupakwa rangi. Kwa wageni Mwanza,eneo ni round about ya Nyerere road,Kenyatta road,Makongoro road na regional drive pale kwenye jengo la Benki kuu.

Kilicho nisikitisha zaidi ni uamuzi wa serikali kuweka kibao (display) kilichoandikwa "MTI HUU ULITUMIWA NA WAKOLONI KUWANYONGA WAHALIFU" Shabaash! Wahalifu? Yaani bado tunaakili za kikoloni? Hawa ni MASHUJAA na tunapaswa kuwaenzi. Kuwaita wahalifu ni ukosefu wa nidhamu na haya ni matusi ya wazi kwa wapigania uhuru.

Watu hawa walimwaga damu na si maji hivyo Bendera ya Tanzania iwe na ufito au mchirizi mwekundu ili kuonesha thamani ya damu ya mashujaa hawa.Kwani vita ilipiganwa kuleta uhuru vita ya majimaji na nyinginezo. Wito wangu kwa afisa utamaduni wa Mwanza abadili maneno ya kibao na Serikali iweke rangi nyekundu kwenye bendera yetu. Ukweli inasikitisha sana.