Masikini Tanzania! Kwa sera hizi itagawanyika vipande vipande

About the Charter


Ukisoma hiyo linki utajua kuwa wenzetu ulaya wanangaika kupreserve lugha zao za asili ambzo nyingi zimekufa au kumezwa na lugha zingine sisi mpaka baadaye sana ndio tuaamka usingizini. Kwa mawazo yaha watanzania wako tayari lugha za Kigeni zienezwe mpaka vijijini ila za asili hazina nafasi tena, kweli psycological colonialism in nguvu kuliko physical presence ya mtu mweupe

Mimi nashindwa kuelewa ni kwa nini watanzania wone lugha zao za asili ni mbaya na zimepitwa na wakati, au ni ukabila.
Mimi nachukia sana kujifanya mzungu wakati wenzetu wanajivunia walichonacho.
Ni wakati wakurudia asili yetu
 
Naunga mkono hoja ya kambi ya upinzani iliyowasilishwa na Mr. 2proud (Mbunge). nachukia maendeleo ya sisi masikini yanayofisha na kuzika kila chenye asili yetu. Tamaduni na lugha zetu za asili ni lazima ziendelee kuhifadhiwa na kuenziwa by Tv's radio nk.

Mawazo ya kuendeleza lugha moja na utaifa kwa kuua lugha zetu za asili yalikuwa ya kijinga ni sawa na yale ya kuendeleza miji yetu kwa kubomoa maeneo ya historia.

Na ndiyo maana hatuendelei kila kitu ni cha ku-copy copy tu. Vya asili yetu vyote tunaviona ni vya kijinga.
 
Amezungumzia mambo mengi yanayohusiana na kuhifadhi utamaduni na sio lugha peke yake...Hata kwenye suala la lugha amesema kuwepo na matangazo kwa lugha za makabila mbali mbali lakini kwa usimamizi wa karibu wa serikali, kwa hili hakuna ubaya hata kidogo.

ubaya upo mkuu.
 
About the Charter


Ukisoma hiyo linki utajua kuwa wenzetu ulaya wanangaika kupreserve lugha zao za asili ambzo nyingi zimekufa au kumezwa na lugha zingine sisi mpaka baadaye sana ndio tuaamka usingizini. Kwa mawazo yaha watanzania wako tayari lugha za Kigeni zienezwe mpaka vijijini ila za asili hazina nafasi tena, kweli psycological colonialism in nguvu kuliko physical presence ya mtu mweupe
Mkuu tuko pamoja katika hili, ni muhimu sana kutunza lugha zetu zinazotutambulisha, I mean culture, social and even life style! Hao wanaoona lugha za kigeni ndo za maana acha waendelee
 
Yaani lugha moja ya watu wa mashariki mwa nchi yaani kiswahili ilichukuliwa na kufanywa lugha ya wote halafu zingine zikaonekana ni ukabila , then huo ndio uzalendo mbona kituko.

Nawapongeza sana UNESCO na hatua hii, lazima tukubali asili yetu kama huna asili basi itafute, sio kuiogopa.[/QUOTE]

Mkulu
Kama kuna kitu kinachotuunganisha sisi kama taifa basi ni KISWAHILI.

Tunamatatizo makubwa sana sisi kama taifa kuliko kuzungumzia suala la lugha za asili,UNESCO(UMOJA WA MATAIFA) wanalifahamu hilo

Wasiwasi wangu isije ikawa wapo hatua kumi mbele kwenye hili wanaloshauri kuliko sisi , tukafikiri mambo yote ni shwari ????!!!!
 
Back
Top Bottom