Masikini Edward Lowassa

mkuu ninapicha za msafara wa lowasa ukizomewa na wakazi wa kikatiti hakika leo ccm imevuna aibu hapa arumeru...nitazirusha nikifika kwenye pc...wameru wasema hawataki mafisadi

Mkuu tunasubili kwa hamu hizo picha, nataka niwe shahidi wa kifo cha ccm!
 
na kweli jf ni kisima cha great thinkers.mzee mzima nimerudi utotoni leo
baba asiye kifani,
akajibu lile swali,
ninakufa maskini,
baba yenu sina mali,
neno moja lishikeni,
nami nawapa kauli,
kama mnataka mali,
mtaipata shambani.

urithi tunatamani mali yetu ya halali sema ipo wapi mali tukaifate shambani
 
Mkuu, Usinikumbushe miye mambo ya Enzi hizo!

Wakazidi kumchimba, Baba mwenye homakali
Baba yetu watufumba, Fumbo hili la akili
Akili yetu nyembamba, haijajua methali.

Watoto wake wakaja, Ili kumtaka hali
Wakataka na kauli, Iwafae maishani


Akatamka mgonjwa, Ninaumwa kwelikweli
Hata kama nikichanjwa, Haitoki homa kali
Roho naona yatoka Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, Mtayapata shambani.

Kwanza shirikianeni, Fanyeni kazi kindugu
Kama mnataka mali, Mtayapata shambani
 
urithi tunatamani mali yetu ya halali sema ipo wapi mali tukaifate shambani

Great. Sina shaka Nyerere atakuwa kasema yake kiaina ila sasa akiona vijana walivyochacharika kuuza mashamba badala ya kutifua waikute hazina inamuuma sana.
 
muda bado Kampeni ni saa 10:00 jioni wacha watu wapange viti kwanza, ingawa si halali kumkampenia mkwe wake lakini kwa CCM watajaa tu
weka picha tuone hizo za saa hizi 1:39

Si watajaa hao wa kuletwa na malory!
 
Duh!! We wasira atakufaa zaidi kama suala ni kuuza sura tu,kwani itakuwa hata kwwenye uwanja wa seremala ukitaka game jamaa yeye anakoroma hapohapo ukimweka kwenye V!!!

Teh teh kweli mkuu huyu cha usingizi anamfaa kweli kweli!
 
Tuambieni ni malory mangapi yameleta magamba ya kijani huko?
 
Watoto wake wakaja, Ili kumtaka hali
Wakataka na kauli, Iwafae maishani


Akatamka mgonjwa, Ninaumwa kwelikweli
Hata kama nikichanjwa, Haitoki homa kali
Roho naona yatoka Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, Mtayapata shambani.

Kwanza shirikianeni, Fanyeni kazi kindugu
Kama mnataka mali, Mtayapata shambani
Wakapata na vikombe, mavazi na baiskeli,
Wakawanunua ng'ombe, majike kwa mafahali
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata Arumeru!

 
Amekuja kumsaidia mkwe wake jamaani. Imekaa vizuri hiyo! naona aibu kumshirikisha baba mkwe wangu kwenye biashara zangu jamani. nitamdaihe?
 
Aibu ya kujitakia utu-Uzimani!
Mwenye nchi mwenyewe Ba-Mwanaasha kagwaya...Kaja jana Arusha kwa kuingia Usiku, na saa 5 LEO kajiondokea zake kimya kimya kurudi Dar!...Watchdogs wake weshampa Live kuwa asithubutu kukanyaga Arumeru, maana washanusa hali halisi!...Yeye anajifanya shababi...Poooof!

Alikuwa Mount Meru Hotel leo asubuhi kufungua session ya international association of ant-corruption.

8E9U9037.JPG
 
maskini EL,ujui na hujui kama ujui,kuna uchafu unaoweza kusafishika lakini si uchafu wa kifisadi,unajipa matumain kwa kua unapesa ulizozipata kiharamu,yote utafanya lakini mungu hapokei rushwa
 
Watoto wake wakaja, Ili kumtaka hali
Wakataka na kauli, Iwafae maishani


Akatamka mgonjwa, Ninaumwa kwelikweli
Hata kama nikichanjwa, Haitoki homa kali
Roho naona yatoka Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, Mtayapata shambani.

Kwanza shirikianeni, Fanyeni kazi kindugu
Kama mnataka mali, Mtayapata shambani
537413_3610067575454_1386669031_3493437_1477920730_n.jpg
sizitaki mbichi hizi​
 
Back
Top Bottom