Masikini Babu Seya, hali yake kiafya yawa mbaya apelekwa Muhimbili

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,263
16,287

Mwanamuziki nguli nchini anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anadaiwa yu taaban ambapo amekimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Mwandishi wetu alimshuhudia Babu Seya akiwa Muhimbili chini ya ulinzi wa askari magereza watatu na wafungwa wengine watano katika Jengo la Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) huku akiwa amedhoofu.

Haikuweza kujulikana mara moja ugonjwa uliosababisha Babu Seya ahamishiwe Muhimbili kwa matibabu kwa sababu Jeshi la Magereza lina hospitali yake na mwandishi alipoomba kwa mmoja wa askari magereza ili aweze kumsalimia mwanamuziki huyo, hakupewa ruhusa.

Baadhi ya wananchi waliomshuhudia mwanamuziki huyo akiwa Muhimbili na kuingizwa katika chumba cha daktari namba 112 walisema, anavyoonekana ni dhahiri ni mgonjwa kwa sababu hakuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake.

“Nguza (Babu Seya) mara nyingi huwa mchangamfu lakini leo amekuwa mnyonge, mwili umepungua na hata ngozi yake siyo ang’avu, bila shaka anaumwa sana,” alisema mwananchi mmoja hospitalini hapo.

Hata hivyo, mara baada ya matibabu, Babu Seya aliingizwa katika gari la magereza na kurudishwa Gereza la Ukonga kuendelea kutumikia kifungo chake.

Dodosadodosa ya mwandishi hospitalini hapo ili kujua kinachomsumbua Babu Seya, haikuambulia chochote kwani daktari mmoja alisema ni mwiko kwao kutaja ugonjwa wa mgonjwa bila ridhaa yake na ni kinyume cha maadili ya kidaktari.

“Umeniuliza anaumwa nini, kwanza mimi siye niliyemtibu lakini hata kama ningejua ugonjwa wa Babu Seya, siwezi kukuambia ni unethical (kinyume cha maadili). Lakini kweli ni mgonjwa na ndiyo maana ameletwa hapa kutibiwa,” alisema daktari huyo aliyekuwa nje ya jengo moja akizungumza na mwanamuziki huyo.

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Eddy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye Papii Kocha kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Sinza-Mapambano, Dar na kuwafunga kifungo cha maisha jela huku rufaa ya kesi yao ikiwekwa kiporo kwenye Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu iliyopo jijini Arusha.
 
Hali yake mbaya........., amekimbizwa muhimbili ......., uandishi wa habari siku hizi kanyanga tu. Mtu kaenda anatembea mwenyewe mnasema amekimbizwa.

Hana uchangamfu wake wa siku zote......., sasa anaumwa na yuko hospitali mnataka achangamkeje labda? Nyie mkiumwa huwa mnachangamka?
 
Ulikuwepo?

Nikutokana na hukumu ambayo mpaka leo kashindwa kupangua hoja maana yake ushahidi ulikuwa mzito sana.Halafu wapo watanzania wengi sana magerezani waliohukumiwa maisha mbona sioni watu wa kuwaonea huruma lakini Babu Seya kila siku utasikia masikini afya yake iko hivi iko vile ebo au kwasababu alikuwa mwanamziki hamtaki apewe anachostahili.

Nauliza tena na tena ungekuwa wewe ndio mzazi wa wale watoto waliodhalilishwa bado ungesema Babu seya atoke jela au kwakuwa si watoto wenu mnakenua midomo tu.
 
We kweli akili zako zimekaa kiunoni watu wamekataa rufaa zaidi ya mara tatu zote wanashindwa halafu unadai wamesingiziwa hata Baba yako alisingiziwa wewe ni mtoto wake.
Hapo ndo mwisho wa ufahamu wako ulipoishia sikulaum, nikikuuliza baba yangu kaingiaje hapa?

Anyway they are in prison good for you and your team! !

So long as sio mahakama ya mbinguni haina shida sana! !

Enjoy
 
Hapo ndo mwisho wa ufahamu wako ulipoishia sikulaum, nikikuuliza baba yangu kaingiaje hapa?

Anyway they are in prison good for you and your team! !

So long as sio mahakama ya mbinguni haina shida sana! !

Enjoy

Nikikuuliza akili za mbayu mbayu zimeingiaje utabaki unashangaa mara nyingi mtu upewa majibu kutokana na kauli zake,ungepinga hoja zangu kwa kauli za staa hakika Baba yako asingeingia hapa.
 
Back
Top Bottom