Mashinikizo yanamtesa JK

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Kufuatia hotuba ya JK leo kwa Taifa, ameonyesha wazi kuwa hivi sasa yuko katika wakati mgumu sana wa utendaji wake wa kazi. Amethibitisha kuwa anapata mashinikizo kutoka chama chake CCM, wabunge wake wa CCM, vyama vya upinzani na majukwaa mbalimbali ya kijamii.

Kutokana na mashinikizo hayo amekuwa anashindwa kutoa maamuzi muhimu kwa wakati akihofia upinzani anaoweza kukabiliana nao!

Je tutamsaidia namna gani ili Rais wetu aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi bila woga wala mashinikizo?
 
Kupitia mshauri wake mkuu ridhiwan, atakuwa anapambana na changamoto hizo...
 
Chakumsaidia ni kumshahuri awemkali na atimue wote wale wanaobabaisha katika utendaji wao wapo watu wanao wezakufanya kazi wazee wanamchanganya na vijana wapo wengi wenye uwezo!
 
Tatizo la JK anapenda kuwafurahisha kila mtu kwa wakati mmoja.
 
Cha kumshauri hapo awe mkali,sio kucheka muda wote,apige chini mara moja wanaofanya madudu
 
Kwa ufahamu wangu, urais ni taasisi kubwa ambayo ina watu wenye ufahamu wa viwango tofauti wa mambo mbalimbali. Na kwa kila jambo kuna watu wenye weledi huo ambao wanapaswa kumshauri rais afanye nini kuhusu jambo husika. Watu hao wanapaswa kufanya uchunguzi au tafiti ili kupata undani wa tatizo na kumshauri rais. Sasa kama rais wetu hana watu hao anafanyaje kazi zake?

Na jambo lingine ni kwamba, akishajua ukweli wa jambo lililo mbele yake anapaswa kutoa uamuzi pasipo kuangalia utamdhuru nani. Na anapaswa kuusimamia uamuzi wake kwa gharama ya kuchukiwa na kila mtu, lakini tu, mwisho wa siku ulete mrejesho uliochanya!

JK, huu ni wakati wa kutoa maamuzi magumu! Ili uweze kupata mafanikio ambayo hujawahi kuyapata, unapaswa kuchukua uamuzi mgumu ambao hujawahi kuufanya maishani mwako. Kazi ni kwako!
 
Kufuatia hotuba ya JK leo kwa Taifa, ameonyesha wazi kuwa hivi sasa yuko katika wakati mgumu sana wa utendaji wake wa kazi. Amethibitisha kuwa anapata mashinikizo kutoka chama chake CCM, wabunge wake wa CCM, vyama vya upinzani na majukwaa mbalimbali ya kijamii.

Kutokana na mashinikizo hayo amekuwa anashindwa kutoa maamuzi muhimu kwa wakati akihofia upinzani anaoweza kukabiliana nao!

Je tutamsaidia namna gani ili Rais wetu aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi bila woga wala mashinikizo?
toa mifano mkuu ili uelweke sidhani kama kushauliwa ni kushinikizwa
 
mwenye hotuba kamili tunaomba atuwekee hapa wengine tupo mbali hatukuweza kuipata live!!
 
imagine uko vitani au kwenye operating table halafu unapata kigugumizi cha maamuzi unatarajia nini?

Ina maana hana plan ya utekelezaji wa malengo yake au hata hayo malengo yenyewe hana?!
 
tatizo la jk anapenda kuwafurahisha kila mtu kwa wakati mmoja.

hapo ndipo tatizo linapoanzia.anatakiwa afumbe macho kwanza awatimuwe wote wasiojituma kazini
huko serikalini na aweke nidhamu katika chama chake.haiwezekani kila mtu akawa boss.ngos watasema
tu afanye vizuri au vibaya watasema tu in many cases huwa hawaridhiki.
 
...utamshauri nini mtu ambaye anashindwa kujua kati ya watu 300(wabunge wa ccm) na watanzaia millio 50 wapi ni wengi?...
 
Kikwete ni janga la kimataifa pamoja na ikulu yake. Kwa nchi za watu wenye akili timamu angekua yuko jela
 
Tatizo la JK anapenda kuwafurahisha kila mtu kwa wakati mmoja.

dah! Mimi hakunifurahisha hata kidogo!kwani ni watumishi wa kada zote wanapata ugumu huu wa maisha uliosababishwa na yeye mwenyewe!iweje aone hawa wa afya ndio wenye haki?? Ahahahaaaa! Kumbe nilazima kugoma ndipo tusikilizwe!!
 
Back
Top Bottom