Mashine za kunyolea ndevu n.k zinaitwa Al Shabab

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Nilienda dukani kwa ajili ya kununua vitu mbalimbali vya dukani na kuona mashine ya kunyolea kama zile za Bic au gillete inaitwa Al Shabab ipo dukani. Ninajiuliza swali je zinatengenezwa na kundi la Al shabab la Somalia au imetokea tu majina kufanana?. Na kama zinatengenezwa na kundi hilo kwanini zimeruhusiwa kuingizwa TZ?.
 
al shabab ni kijana mahiri,rijali, aliyekomaa(aliyebalehe na kuota ndevu) nk ndo maana halisi na ndio maana watengenezaji wa vinyoleo hivyo walichagua jina hilo lakini wale jamaa wamejibatiza tu na kwa kuwa ule msahafu haujaandikwa kizungu wala kiswahili lazima uone chenga
 
Shabaab kiarabu inamaanisha kijana,hili kundi lilikuwa la vijana(kama UVCCM au Bavicha) katika Islamic court union kilichokua kikitawala eneo kubwa la Somalia kwa amani kwa miaka mitatu kabla ya uvamizi wa Ethiopia kwa shinikizo la Marekani(waliolipia kila kitu) na kuirudisha tena nchi kwenye vita.<br>Kundi hili lilibadilika na kuwa la kijeshi kuwaondoa Ethiopia.
 
Back
Top Bottom